The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

2 7 8 /

UFALME WA MUNGU

Ufalme Wako Uje: “Hadithi ya Utukufu wa Mungu” (muendelezo)

A. Kabla ya Wakati (Milele iliyopita), Zab. 90:1-3 1. Mungu katika Utatu wa milele, Zab. 102:24-27 2. Kusudi la Mungu la milele, 2 Tim. 1:9; Isa. 14:26-27

a. Kulitukuza jina lake katika uumbaji, Mit. 16:4; Zab. 135:6; Isa. 48:11 b. Kudhihirisha ukamilifu wake katika ulimwengu, Zab. 19:1 c. Kujitengenezea watu wake kwa ajili yake Yeye mwenyewe, Isa. 43:7, 21 3. Siri ya uovu: uasi wa Nyota ya Alfajiri ( Lusifa ), Isa. 14:12-20; Ezek. 28:13-17 4. Enzi na mamlaka, Kol. 2:15 B. Mwanzo wa Wakati (uumbaji), Mwa. 1-2 1. Neno la uumbaji la Mungu wa Utatu, Mwa. 1:3; Zab. 33:6, 9; 148:1-5 2. Uumbaji wa mwanadamu: Imago Dei , Mwa. 1:26-27 C. Janga la Wakati (Anguko na Laana), Mwa. 3 1. Anguko na Laana, Mwa. 3:1-9 2. Protoevangelium : Uzao ulioahidiwa, Mwa. 3:15 3. Mwisho wa Edeni na utawala wa mauti, Mwa. 3:22-24 4. Ishara za kwanza za neema, Mwa. 3:15, 21 D. Kufunuliwa kwa Wakati (Mpango wa Mungu ukifunuliwa kupitia watu wa Israeli) 1. Ahadi ya Abrahamu na agano la Yehova (Mababa); Mwa. 12:1-3; 15; 17; 18:18; 28:4. 2. Kutoka na agano la Sinai, Kutoka. 3. Ushindi dhidi ya watu wa Nchi ya Ahadi na kuchukuliwa, Yoshua hadi 2 Mambo ya Nyakati. 4. Mji, hekalu, na kiti cha enzi, Zab. 48:1-3; 2 Nya. 7:14; 2 Sam. 7:8-. a. Wajibu wa nabii, kutangaza Neno la Bwana , Kum. 18:15.

Made with FlippingBook - Online catalogs