The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

/ 2 8 9

UFALME WA MUNGU

KIAMBATISHO CHA 40 Orodha ya Kuhakiki Huduma ya Kiroho Mch. Dkt. Don L. Davis

1. Wokovu : Je, mtu huyu ameiamini Injili, amemkiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozi, amebatizwa, na amejiunga rasmi na kanisa letu kama mshirika? 2. Uadilifu Binafsi : Je, anatembea na Mungu, anakua katika maisha yake binafsi, na kuonyesha upendo na uaminifu katika familia yake, kazini, na katikati ya jamii? 3. Kuandaliwa Katika Neno : Mtu huyu ameandaliwa vipi katika Neno la Mungu ili kuwashirikisha na kuwafundisha wengine? 4. Msaada kwa kanisa letu : Je, analisaidia kanisa kupitia uwepo wake, kuombea viongozi na washirika, na kutoa msaada wa kifedha kwa kanisa? 5. Utii kwa mamlaka : Je, mtu huyu anajitiisha kwa furaha kwa mamlaka ya kiroho? 6. Kubaini karama za kiroho : Ni karama gani, talanta, uwezo, au rasilimali gani maalum ambayo mtu huyu anayo kwa ajili ya huduma, na ni mzigo gani hasa alionao kwa ajili ya huduma sasa? 7. Upatikanaji wa sasa : Je, yuko wazi na tayari kupewa kazi au shughuli ambapo tunaweza kutumia huduma yake kuujenga Mwili? 8. Sifa miongoni mwa viongozi : Je, viongozi wengine wanahisije kuhusu utayari wa mtu huyu kwa ajili ya nafasi mpya ya uongozi? 9. Rasilimali zinazohitajika kutimiza majukumu : Iwapo atateuliwa kwa ajili ya jukumu hili, ni mafunzo gani hasa, fedha, rasilimali, na/au uwekezaji gani atahitaji ili kutimiza majukumu hayo? 10. Kuingizwa kazini rasmi : Ni lini na jinsi gani tutawajulisha wengine kwamba tumemteua mtu huyu kwa ajili kazi au shughuli hii? 11. Muda na kuripoti : Pia, ikiwa tunamweka mtu huyu katika jukumu/kazi hii, ataweza kuanza lini, na anapaswa kuhudumu kwa muda gani kabla hatujamtathmini? 12. Tathmini na kupewa kazi tena : Ni lini tutatathmini utendaji wa mtu huyu, na kuamua ni hatua zipi zinazofuata tunazopaswa kuchukua katika nafasi yake ya uongozi katika kanisa?

Made with FlippingBook - Online catalogs