The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

/ 3 7

UFALME WA MUNGU

MAZOEZI

Isaya 14:12-17

Kukariri Maandiko

Kujiandaa kwa ajili ya darasa, tafadhali tembelea www.tumi.org/books ili kupata kazi ya kusoma ya wiki ijayo, au muulize mkufunzi wako.

Kazi ya usomaji

Mpendwa mwanafunzi, kumbuka kwamba utaulizawa kuhusu maudhui (yaliyomo kwenye video) ya somo hili wiki ijayo. Tafadhali hakikisha unatumia muda mwingi wiki ijayo kurejelea madokezo yako, hasa yale yanayolenga dhana kuu au mawazo makuu ya somo. Pia, tafadhali soma kurasa zilizoelekezwa na kuorodheshwa hapo juu, na ufanye muhtasari wa kila ulichosoma kwa aya isiyozidi moja au mbili kwa kila ulichosoma. Usiwe na wasiwasi kuhusu kutoa muhtasari wenye taarifa nyingi; andika kile tu unachodhani ndilo wazo kuu lililojadiliwa katika sehemu hiyo ya kitabu. Tafadhali wasilisha muhtasari huu darasani juma lijalo. (Tafadhali angalia Fomu ya Ripoti ya Usomaji mwishoni mwa somo hili). Katika somo letu linalofuata tutagundua jinsi Mungu alivyozindua utawala wa ufalme wake kupitia agano na Ibrahimu na kushughulika kwake na watu wake katika Agano la Kale. Ijapokuwa hatukumtii Mungu na tuliukataa utawala wake, Yeye hakutuacha bali amedhamiria kuusimamisha tena ufalme wake ndani yetu kwa ahadi ya Mwanawe, ambaye tunamjua kuwa ni Yesu wa Nazareti, Mwana wa Mungu.

Kazi Nyinginezo

1

Kuelekea Somo Linalofuata

Made with FlippingBook - Online catalogs