The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

/ 4 1

UFALME WA MUNGU

Kuzinduliwa kwa Utawala wa Mungu

SOMO LA 2

Karibu katika jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma kwako, kujifunza, majadiliano, na matumizi ya maudhui katika somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kuonyesha kwa kutumia Maandiko kwamba tangu Anguko, utawala wa Mungu umezinduliwa katika ulimwengu huu wa sasa. • Kueleza jinsi Mungu anavyoleta utawala wake ulimwenguni kwa makusudi kabisa, kwanza, katika mwelekeo wake mwenyewe kama Shujaa juu ya adui zake. • Kuonyesha namna ambavyo Mungu alitekeleza kuzinduliwa kwa Ufalme wake kupitia ahadi ya agano ya ukombozi aliyopewa Abramu, na kupitia historia ya uhusiano na utendaji wa Mungu pamoja na taifa la Israeli, watu wake wa agano. • Kuelezea namna ambavyo Yesu wa Nazareti ulimwenguni anawakilisha uwepo wa Ufalme uliodhihirishwa katika umwilisho wake (kuvaa mwili), kifo, ufufuo, na kupaa kwake. • Kukariri kifungu kinachohusiana na kuzinduliwa kwa utawala wa Mungu. Soma Marko 1:14-15 . Sote tunapenda kusikia mambo yakitangazwa. Tunapenda kusikia habari njema, hasa inapohusu kupata zawadi, kupokea baraka, kupata kitu ambacho umekitamani sana. Yesu aliposema maneno haya katika Marko, alikuwa ametoka tu kuanza kutangaza Habari Njema. Baada ya kubatizwa na Yohana Mbatizaji na kustahimili majaribu ya shetani nyikani, Yesu anaenda Galilaya. Marko anatupa makisio ya wakati kwa maneno haya: Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani. Kwa hiyo, ilikuwa ni mapema katika huduma ya Yesu, muda baada ya tangazo ambalo Yohana Mbatizaji alikuwa amelitoa kuhusu Yesu kama Mpakwa-Mafuta ajaye. Yesu, katika wakati huu muhimu katika historia ya wokovu anakuja akitangaza, na kuzindua kiuhalisia (kuanza rasmi) mahubiri na huduma yake ya Ufalme. Yesu alitambua umuhimu wa wakati huo, akidokeza kwamba “wakati umetimia,” yaani, wakati ulionenwa na manabii kwamba utawala wa Mungu ulikuwa umefika. Bila mbwembwe, bila tarumbeta, fataki, au makusanyiko makubwa na misafara ya waheshimiwa, Mesihi anatangaza kwamba Ufalme Umesikia Tangazo?

Malengo ya Somo

2

Ibada

Made with FlippingBook - Online catalogs