The Kingdom of God, Swahili Student Workbook
/ 4 5
UFALME WA MUNGU
1. Mgawanyo wa Biblia katika sehemu mbili zisizolingana:
a. Kutoka Mwanzo 1:1 hadi Mwanzo 3:15.
b. Kutoka Mwanzo 3:16 hadi mwisho wa kitabu, Ufunuo 22:21.
2. Katika hukumu ya Mungu dhidi ya nyoka katika Mwanzo 3:15, Bwana anatoa muundo wa msingi wa nguvu za kiroho katika ulimwengu, tamthilia ya Ufalme katika taswira.
2
3. Utambulisho wa wahusika wa tamthilia ya ufalme wa Mungu.
a. Mgogoro wa kudumu, usio na kikomo kati ya nyoka na mwanamke.
b. Uzao wa mwanamke – Masihi ajaye.
c. Uzao wa nyoka – uzao wa yule mwovu (nyoka).
d. Uzao wa mwanamke ungeponda kichwa cha nyoka, na nyoka angeponda kisigino cha Uzao huo.
B. Tremper Longman na Daniel Reid: picha ya Mungu kama Shujaa wa Kiungu imeanzia katika kitabu cha Mwanzo na kuendelea hadi kitabu cha Ufunuo.
Made with FlippingBook - Online catalogs