The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

/ 6 3

UFALME WA MUNGU

³ Kifo cha Yesu kilivunja nguvu za shetani na wafuasi wake, na pia kulipa adhabu ya dhambi zetu. Akiwa dhabihu kuu na Kuhani Mkuu, Yesu amelipa yote kwa ajili ya wanadamu, kama Christus Victum. ³ Ufufuo wa Yesu ulitokea: ishara ya cheo chake cha Uwana wa kiungu, utimilifu wa agano la Daudi, uthibitisho kwamba Mungu ametusamehe dhambi zetu, na ishara ya limbuko ya wale wote ambao siku moja watafufuliwa kuingia katika uzima wa milele kwa njia ya imani katika yeye. ³ Kupaa kwa Yesu mkono wa kuume wa Baba ni ishara inayoonekana ya mamlaka na ukuu wa Yesu, kama Kichwa cha Kanisa, Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Mungu, kama Bwana wa kazi ya mavuno ya utume, na kama Bwana Mshindi katika yote, ambaye hivi karibuni atakuja na kuukamilisha Ufalme. Sasa ndio wakati wa wewe kujadili pamoja na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu Ufalme wa Mungu uliozinduliwa na kutimizwa leo. Maana za Yesu kuudhihirisha Ufalme hazina idadi na ni muhimu, na bila shaka utakuwa na maswali kuhusu umaana wa kazi yake katika maisha na huduma yako. Je, una maswali gani hasa kwa kuzingatia maudhui ambayo umejifunza hivi punde? Labda baadhi ya maswali yaliyopo hapa chini yanaweza kukusaidia kuunda maswali yako mwenyewe, mahususi na muhimu zaidi. * Je, kweli tunaweza kutaja wakati ambapo Baba aliamua kupindua na kutangua matukio ya uasi wa Shetani na kutotii kwa Adamu na Hawa? * Ikiwa Ufalme tayari upo kwa kiwango fulani leo, kwa nini ulimwengu bao si wa haki na unaonewa sana? Hasa zaidi, kwa nini maskini bado wanaonewa, kunyanyaswa, na kupuuzwa ikiwa Mwaka wa Yubile umekwishatangazwa tayari? * Je, ahadi mahususi kuhusu Ufalme halisi wa kimwili zitatimizwa, au zinapaswa kueleweka kwa njia ya kiroho tu? * Kwa nini inaonekana kana kwamba ibilisi angali ana nguvu na mamlaka ikiwa Yesu alimshinda kabisa pale Kalvari msalabani? Je, sisi kama waamini tunaweza kutumia mamlaka haya makubwa kwa kiasi gani, na tunawezaje kufanya hivyo? * Jiji lina nafasi gani kuhusiana na Ufalme wa Mungu leo? Ikiwa Ufalme tayari upo kwa namna fulani, hilo linamaanisha nini kwetu katika huduma ya mijini?

2

Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Wanafunzi

Made with FlippingBook - Online catalogs