The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

/ 6 5

UFALME WA MUNGU

Masihi aliyewaalika. Baada ya kukataa aina ya ufalme ambayo Yesu aliwatangazia, anasema sasa tuko katika enzi ya Kanisa ambayo inakuja kati ya wakati wa ofa ya ufalme ambayo Yesu aliitoa, na wakati wa Ujio wa Pili, ambapo Israeli hatimaye itakubali ofa ya ufalme wa Mungu, na Ufalme wa Daudi utawekwa katika siku zijazo. Sasa, hakuna udhihirisho wa Ufalme uliopo, kila kitu kinachohusika na Ufalme ni cha baadaye. Ungemwambia nini mwanafunzi huyu? Je, maoni yake yanaonekana kuwa na usahihi wowote? Tangu Anguko, Mungu ametafuta kukomesha na kupindua athari zake kwa kuleta utawala wake katika ulimwengu huu wa sasa. Alianza kudhihirisha utawala wake kwa uthabiti kwa kuchukua msimamo kama Shujaa juu ya maadui zake. Kupitia ahadi yake ya agano kwa Abrahamu, Mungu aliazimia kuleta Mzao ulimwenguni ambao ungeponda kichwa cha nyoka na kubariki familia zote za dunia. Ahadi hii ilifanywa upya kwa mababa, katika Israeli, kwa kabila la Yuda na ukoo wa Daudi. Hatimaye, katika Yesu wa Nazareti na kazi zake, utawala wa ufalme wa Mungu umezinduliwa kwa maana ya mwisho katika ulimwengu huu. Kama Christus Victum , alitukomboa kutoka katika nguvu za shetani, dhambi na kifo, na kama Christus Victor , amefufuka kutoka kaburini na kupaa mbinguni kama Bwana wa wote. Ingawa haujatimizwa kikamilifu, Ufalme umekuja katika nafsi ya Yesu Kristo. Ikiwa una nia ya kufuatilia baadhi ya mawazo ya somo hili Mungu kama Shujaa wa Kiungu , unaweza kujaribu vitabu vifuatavyo: Dawson, John. Taking Our Cities for God . 2nd. ed. Altamonte Springs: Charisma House, 2001. Lind, Millard. Yahweh is a Warrior: The Theology of Warfare in Ancient Israel . Scottsdale: Herald Press, 1980. Uhusiano wa maana za ushindi wa Yesu una umuhimu mkubwa kwa kila nyanja ya huduma yetu. Sasa ni wakati wa kujaribu kukazia theolojia hii ya juu kwa kuhusianisha elimu hii na mazingira halisi ya huduma kwa vitendo, ambayo utaifikiria na kuiombea katika wiki hii yote ijayo. Roho Mtakatifu anakudokeza nini hasa kuhusiana na utawala wa Mungu, na changamoto yake leo? Ni hali gani inakuja akilini unapofikiria kuhusu ukweli wa kuzinduliwa kwa utawala wa Mungu na maisha yako na huduma yako leo? Jipe muda wa kutafakari mbele za Bwana juu ya mambo haya, naye atakufunulia kweli hizi na kukujulisha kile unachopaswa kufanya kutokana na kile anachokufunulia.

Marudio ya Tasnifu ya Somo

2

Nyenzo na Bibliografia

Kuhusianisha Somo na Huduma

Made with FlippingBook - Online catalogs