The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

7 2 /

UFALME WA MUNGU

Uvamizi wa Utawala wa Mungu Sehemu ya 1

YALIYOMO

Mch. Dkt. Don. L. Davis

Kusudi la sehemu hii ni kuonyesha jinsi Kanisa la Yesu Kristo, kama mwili na wakala wake, lenyewe lilivyo kituo (mahali na/au muktadha) wa wokovu wa Mungu, wa uwepo utiao nguvu wa Roho Mtakatifu, na wa madhihirisho ya kweli ya maisha na ushuhuda wa Ufalme. Lengo letu la sehemu hii ya kwanza ya Uvamizi wa Utawala wa Mungu ni kukuwezesha kuona kwamba: • Kanisa la Yesu Kristo ni kituo (mahali au muktadha) wa wokovu wa Mungu. • Kanisa ni mahali pa uwepo wa Roho Mtakatifu unaotia nguvu. • Kanisa ni mahali pa shalom halisi ya ufalme wa Mungu. • Ndiyo, Ufalme wa Mungu unavamia enzi hii kupitia uwepo na utendaji wa Kanisa la Yesu Kristo! Maoni ya jumla kuhusu Kanisa: • Ufalme wa Mungu (utawala na mamlaka yake) unavamia ulimwengu kupitia Kanisa la Yesu Kristo. • Jumuiya ya Mungu wa Utatu: watu wa Mungu (2 Kor. 6:16), mwili wa Kristo, pamoja na Yesu kama kichwa chake (Efe. 1:22-23), na hekalu la Roho Mtakatifu (1 Kor. 3:16-17). • Maana mbili za Ekklesia : 1) Muungano wa waamini wote wa kweli katika Kristo, walio hai na waliokufa. Wakati mwingine dhana hii inajulikana kama “Kanisa la Ulimwengu.” I. Kanisa ndio kituo na uwanja wa wokovu wa Mungu.

Muhtasari wa Sehemu ya 1

3

Muhtasari wa Sehemu ya 1 ya Video

Made with FlippingBook - Online catalogs