The Kingdom of God, Swahili Student Workbook

8 4 /

UFALME WA MUNGU

IV. Kanisa ni wakala wa Ufalme wa Mungu kwa kuwa chombo cha Mungu cha ishara na maajabu ya kinabii.

A. Kanisa linaweza kutarajia ishara endelevu za uwepo na ubwana wa Kristo katika huduma na utume wa Kanisa.

1. Kitabu cha Matendo ya Mitume kinaeleza kile ambacho Yesu alianza kufanya na kufundisha, na ambacho aliendelea kufanya kupitia Kanisa lake, taz. Matendo 1:1.

2. Kanisa limepewa mamlaka ya kumwakilisha Kristo ulimwenguni, na kwa sababu hiyo kufanya vita dhidi ya nguvu za mapepo ambazo kwa sasa zinaushikilia ulimwengu katika hali ya utumwa, Mt. 16:18.

3

3. Maono ya Agano Jipya kuhusu Kanisa: Shujaa wa Mungu akifanya vita dhidi ya nguvu za giza hili la sasa, Efe. 6:10-18.

B. Roho Mtakatifu huthibitisha Neno la Kristo kwa ishara zinazofuatana nalo.

1. Kanisa, katika kutekeleza agizo lake, linakabiliana na nguvu za yule Mwovu, 1 Pet. 5:8.

2. Kanisa kama Shujaa wa Mungu, limeitwa kumkabili adui moja kwa moja, likifanya vita kwa Neno na imani dhidi ya watawala wa giza hili la sasa, Efe. 6:10-.

3. Ingawa Kanisa liko ulimwenguni, silaha za vita vyake si za ulimwengu bali ni zina nguvu katika kufanya vita dhidi ya ufalme wa Shetani, 2 Kor. 10:3-5.

Made with FlippingBook - Online catalogs