Theology of the Church, Swahili Mentor Guide

/ 2 2 9

THEOLOJIA YA KANISA

Kanisa katika Ibada

MAELEZO YA MKUFUNZI 2

Karibu kwenye Mwongozo wa Mkufunzi wa Somo la 2, Kanisa kwenye Ibada . Lengo la somo hili ni kuwasaidia wanafunzi kulielewa Kanisa kama jumuiya ya watu ambao wameipokea neema ya Mungu na ambao wanaiitikia neema hii kwa kushiriki katika ibada kama wajibu wao na furaha yao. Sehemu ya kwanza itajikita katika ukweli kwamba wokovu ni kwa neema kwani hapa ndio mahali pa kuanzia kwa habari ya mwitikio wa ibada. Pia itazungumza kuhusu Meza ya Bwana na ubatizo kama njia mbili muhimu zaidi ambazo kupitia hizo Kanisa hutambua, huishi, na kuitikia neema ya Mungu. Kwa kuwa kuna tofauti halali za kimtazamo na kitafsiri kuhusu asili ya Meza ya Bwana na ubatizo kati ya waamini wa kiinjili, tafadhali uwe tayari kukabiliana na hali ya kutoelewana kati ya wanafunzi wako kuhusu kile ambacho Biblia inafundisha na uwe tayari kuongoza majadiliano ambayo ni ya haki, yenye afya na ambayo yatawasaidia wanafunzi kusitawisha kile wanachoamini kwa kuzingatia Maandiko matakatifu na theolojia ya madhehebu yao. Sehemu ya pili itaangazia theolojia ya ibada ya Kikristo na mambo muhimu ambayo yanapaswa kujumuishwa katika ibada ya Kanisa. Wazo kuu ni kustahili kwa Mungu na wazo linalotokana na hilo kwamba Kanisa ni watu walioitwa kumpa utukufu anaostahili. Hata hivyo, mkazo wa Kanisa katika Ibada hauko juu ya Kanisa lenyewe. Katika ibada yake kwa Mungu, Kanisa huzingatia nafsi ya Mungu na kazi ya Mungu. Kanisa linamwabudu Mungu kwa sababu ya ukuu wa asili wa nafsi yake. Tunamtukuza Mungu kwa sababu ya utakatifu wake wa pekee, uzuri wake usio na kikomo, utukufu wake usio na kifani na kazi zake zisizoweza kulinganishwa na chochote. Kama Mungu Mmoja, wa kweli, na aliye hai wa Utatu, Kanisa linamwabudu Mungu kupitia Yesu Kristo. Hakuna awezaye kumwendea Mungu ila kwa imani katika Yesu Kristo, kwa nguvu za Roho Mtakatifu. Hatimaye, Kanisa humpa Mungu ibada yake kwa njia ya sifa na shukrani na kwa kutekeleza ratiba yake ya ibada (yaani, liturujia), ambayo inasisitiza kuhubiriwa kwa Neno na sakramenti. Kwa maana moja, yote tunayofanya kama waamini ni aina ya ibada kwa Mungu, na hivyo tunaweza pia kumtukuza Mungu kupitia utii wetu na mtindo wa maisha kama jumuiya ya agano. Kwa kuwa lengo la somo hili ni ibada, hakikisha kwamba unadumisha “mioyo yenye uchangamfu” na pia “akili safi” kuhusu masuala haya. Wanafunzi wanapaswa kuongozwa katika shukrani na sifa hai wakati wa masomo haya

 1 Ukurasa 45 Utangulizi wa Somo

Made with FlippingBook - Share PDF online