Theology of the Church, Swahili Mentor Guide
2 3 2 /
THEOLOJIA YA KANISA
Mungu ni Mungu wa wanadamu wote, na kwa hiyo anaweza kutukuzwa kihalali na kwa njia ya ajabu kupitia muundo wa kitamaduni wa dhati wa watu wowote ambao wametubu, wameamini, na wanamfuata na kumpenda Mwana wa Mungu, Yesu Kristo kwa Imani na tumaini. Moja ya makosa makubwa ambayo yamefanywa na makusanyiko mengi ya kiibada na Wakristo wengi ni kuamini kwamba baadhi ya maonyesho ya kitamaduni ya ibada ndiyo ibada yenyewe , yaani, njia ambayo ibada zote kila mahali zinapaswa kuzingatiwa na kufanyika. Kuruhusu uhuru wa kutoa shukrani zetu za kina na sifa kwa Mungu ni sehemu muhimu ya huduma ya kiongozi katika kuwaongoza wengine katika uwepo wa Mungu. Wanatheolojia mara nyingi hugawanya neema katika makundi ya maelezo. Neema ya kawaida inarejelea utunzaji wa Mungu juu ya watu wote ambao kwa huo anategemeza maisha (pumzi, mvua, chakula), anatoa ufahamu wa maadili, anatoa utawala wa kiraia, na kuzuia uovu ili kutoa fursa kwa maisha na utamaduni wa mwanadamu kustawi. Neema maalum inarejelea neema ambayo kwayo Mungu huwakomboa, kuwatakasa, na kuwatukuza watu wake. Neema tangulizi inarejelea neema ambayo huja kabla ya juhudi au maamuzi yoyote ya kibinadamu na kufanya iwezekane kwa watu kutamani wokovu na kuitikia kwa imani. [Pelagius alifundisha kwamba] uwezo wa kutenda mema unakaa kiasili ndani ya hiari yenyewe, mbali na zawadi yoyote ya Mungu kwa asili ya mwanadamu, ili kwa kufuata kielelezo cha Kristo, njia ya wema ifunuliwe na watu kwa hiari zao wenyewe waweze kujiepusha na dhambi. Kwa hivyo hakuna haja ya utendaji wowote wa moja kwa moja wa Roho juu ya hiari ya mwanadamu ili kutenda mema, isipokuwa tu kwa Roho kufanya kazi kwa njia isiyo ya moja kwa moja kupitia dhamiri na akili. . . Kati ya mwaka 411 na 431B.K, si chini ya mabaraza ishirini na manne yalikabili suala la Upelagiani. Lilikuwa suala nyeti sana katika maisha ya ukomavu ya Augustine. . . . Mwitikio wa ukubalifu [wa Kanisa] uliboreshwa zaidi katika mabaraza ya Efeso (431) na Orange (529), ambayo yalisimamia suala la ulazima wa neema katika matendo yote yanayohusiana na wokovu. “Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi hamuwezi, msipokaa ndani yangu.” (Yn. 15:4; rej. 1 Kor. 12:3). ~ Thomas C. Oden. The Transforming Power of Grace . Nashville: Abingdon Press, 1993. uk. 110-111.
6 Ukurasa 49 Kipengele namba I-C
7 Ukurasa 50 Kipengele namba I-D-1
Made with FlippingBook - Share PDF online