Theology of the Church, Swahili Student Workbook

This is the Swahili edition of Capstone Module 3 Student Workbook.

Jiwe Walilolikataa Waashi Limekuwa Jiwe Kuu la Pembeni

Theoloji ya Kanisa

THE URBAN

MINISTRY INSTITUTE huduma ya WORLD IMPACT, INC.

u

b

c

a

h

i t

a

K

M

i

z

w

n

a

u

f

n

a

Moduli ya 3 Huduma ya Kikristo

SWAHILI

KITABU CHA MWANAFUNZI

Theolojia ya Kanisa

Moduli ya 3

Huduma ya Kikristo

Ufunuo Kivuli wa Kanisa katika Mpango wa Mungu

Kanisa katika Ibada

Kanisa kama Shahidi

Kanisa katika Kazi

Mtaala huu ni matokeo ya maelfu ya masaa ya kazi iliyofanywa na taasisi ya The Urban Ministry Institute (TUMI) na haupaswi kudurufu bila idhini ya taasisi hiyo. TUMI inatoa idhini kwa yeyote anayehitaji kutumia vitabu hivi kwa ajili ya faida ya ufalme wa Mungu, kwa kutoa leseni za kudurufu za gharama nafuu. Tafadhali thibitisha kwa Mkufunzi wako ikiwa kitabu hiki kimepewa leseni ipasavyo. Kwa taarifa zaidi kuhusu TUMI na taratibu zetu za utoaji leseni, tembelea www.tumi.org na www.tumi.org/license .

Moduli ya 3 ya Capstone: Theolojia ya Kanisa – Kitabu cha Mwanafunzi ISBN: 978-1-62932-372-5 © 2005, 2011, 2013, 2015. The Urban Ministry Institute. Haki zote zimehifadhiwa. Toleo la kwanza 2005, Toleo la pili 2011, Toleo la tatu 2013, Toleo la nne 2015. © 2025 Kiswahili. Kimetafsiriwa na Samuel Gripper na Eresh Tchakubuta Hairuhusiwi kunakili, kusambaza na/au kuuza vitabu hivi, au matumizi mengine yoyote pasipo idhini, isipokuwa kwa matumizi yanayo ruhusiwa kwa mujibu wa sheria ya Haki Miliki ya Mwaka 1976 au kwa idhini ya maandishi kutoka kwa mmiliki. Maombi ya idhini yatumwe katika maandishi kwa taasisi ya: The Urban Ministry Institute, 3701 E. 13th Street, Wichita, KS 67208. The Urban Ministry Institute ni huduma ya World Impact, Inc. Nukuu zote za Maandiko, isipokuwa kama imeonyeshwa vinginevyo, zimechukuliwa kutoka katika SWAHILI BIBLE UV050(MCR) series® Haki Miliki © 1997, iliyochapishwa na The Bible Society of Tanzania. Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote za kimataifa zimehifadhiwa.

Yaliyomo

Muhtasari wa Kozi Kuhusu Wakufunzi Utangulizi wa Moduli

3 5 7

Mahitaji ya Kozi

15

Somo la 1 Ufunuo Kivuli wa Kanisa katika Mpango wa Mungu

1

45

Somo la 2 Kanisa katika Ibada

2

81

Somo la 3 Kanisa kama Shahidi

3

117

Somo la 4 Kanisa katika Kazi

4

151

Viambatisho

/ 3

THEOLOJIA YA KANISA

Kuhusu Wakufunzi

Mchungaji Dkt. Don L. Davis ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya The Urban Ministry Institute na ni Makamu wa kwanza wa Rais wa World Impact. Alisoma katika Chuo cha Wheaton College na Chuo cha Uzamili cha Wheaton na kuhitimu kwa ufaulu wa kiwango cha juu, yaani Summa Cum Claude, katika ngazi ya Shahada (1988) na Shahada ya Uzamili (1989) katika Masomo ya Biblia na Theolojia ya Utaratibu. Alipata Shahada yake ya Uzamivu katika Masuala ya Dini (Theolojia na Maadili) katika chuo kikuu cha Iowa School of Religion. Akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi na Makamu wa Rais Mwandamizi wa World Impact , anasimamia mafunzo ya wamishenari wa mijini, wapanda makanisa, na wachungaji wa majiji, na kufanya uwezeshaji kupitia fursa za mafunzo kwa watendakazi Wakristo wa mijini katika uinjilisti, ukuaji wa kanisa, na umisheni wa upainia. Pia anaongoza Mpango wa Mafunzo huria kwa wale wanaosoma wakiwa mbali, vilevile anawezesha Mafunzo ya Kiuongozi kwa mashirika na madhehebu kadhaa kama Prison fellowship, The Evangelical Free Church of America na The Church of God in Christ. Dkt. Davis, ambaye ametunukiwa tuzo nyingi za ualimu na za kitaalamu, amewahi kuwa profesa na Mkuu wa vitivo katika taasisi kadhaa za kitaalamu zenye hadhi ya juu, baada ya kuhadhiri na kufundisha kozi za dini, theolojia, falsafa, na mafunzo ya Biblia katika taasisi za elimu ya juu kama vile Chuo cha Wheaton, Chuo Kikuu cha St. Ambrose, Programu ya Shahada ya Uzamili ya Theolojia ya Chuo Kikuu cha Houston, Kitengo cha Dini cha Chuo Kikuu cha Iowa, na Taasisi ya Mafunzo ya Ibada ya Robert E. Webber. Ameandika idadi kubwa ya vitabu, mitaala, na nyenzo za kujifunzia ili kuwaandaa viongozi wa mijini, ikijumuisha mtaala wa mafunzo wa Capstone (hii ni programu mama ya TUMI yenye moduli 16 za hadhi ya mafunzo ya seminari, yanayotolewa kupitia mfumo wa elimu ya masafa), Mizizi Mitakatifu: Kidokezo cha Namna ya Kurejesha Mapokeo Makuu , ambayo inaangazia namna makanisa ya mijini yanavyoweza kufanywa upya kupitia kugundua upya imani halisi, sahihi ya kihistoria; na Mweusi na Mwanadamu: Kumgundua Upya M.L. King kama Nyenzo ya Theolojia na Maadili ya Weusi . Dkt. Davis pia ameshiriki katika mihadhara ya kitaalamu kama the Staley Lecture series, makongamano ya kufanywa upya kama Promise Keeper Rallies na miungano ya kithiologia kama The University of Virginia Lived Theology Project Series. Vilevile alipokea tuzo ya heshima ya mwanafunzi mashuhuri ( Alumni Fellow Award ) kutoka Chuo Kikuu cha Iowa cha Sanaa na Sayansi za Kiliberali mnamo 2009. Dkt. Davis pia ni mwanachama wa The Society of Biblical Literature, na The American Academy of Religion .

4 /

THEOLOJIA YA KANISA

Mchungaji Terry Cornett (B.S., M. A., M.A.R.) ni Mkuu wa Taaluma wa Heshima wa The Urban Ministry Institute huko Wichita, Kansas. Ana digrii kutoka Chuo Kikuu cha Texas huko Austin, Chuo cha Uzamivu cha Wheaton, na Chuo cha Theolojia ya C. P. Haggard katika Chuo Kikuu cha Azusa Pacific. Terry alihudumu kwa miaka 23 kama mmishenari wa mjini chini ya World Impact kabla ya kustaafu mwaka wa 2005. Wakati huo alihudumu Omaha, Los Angeles, na Wichita ambako alihusika katika huduma za upandaji makanisa, elimu, na mafunzo ya uongozi.

/ 5

THEOLOJIA YA KANISA

Utangulizi wa Moduli

Salamu, marafiki wapendwa, katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Kanisa la Mwenyezi Mungu katika Yesu Kristo ni mojawapo ya mada zenye kuburudisha na muhimu zaidi katika Maandiko yote. Yesu wa Nazareti, kupitia kifo chake, kuzikwa, na ufufuo wake, ameinuliwa kuwa kichwa juu ya watu wake wapya, wale walioitwa kumwakilisha duniani na kutoa ushahidi wa Ufalme wake ambao tayari upo japo haujakamilika bado. Kuelewa jukumu la Kanisa katika mpango wa ufalme wa Mungu ni muhimu kwa kila eneo la maisha ya ufuasi wa kibinafsi na wa kusanyiko; hakuna ufuasi au wokovu mbali na tendo la Mungu la kuokoa kupitia Kanisa. Kufahamu kile ambacho Mungu anafanya ndani ya na kupitia watu wake kunampa kiongozi wa watu wa Mungu uwezo wa kumwakilisha kwa hekima na heshima. Tunakualika kwa shauku kujifunza kuhusu Kanisa ili kufahamu kikamilifu asili ya huduma ulimwenguni leo. Somo la kwanza, Ufunuo Kivuli wa Kanisa katika Mpango wa Mungu , linaangazia jinsi Kanisa lilivyofunuliwa tangu awali katika kusudi kuu la Mungu la kujiletea utukufu kwa kuokoa jamii mpya ya wanadamu kupitia agano lake na Ibrahimu. Utaona jinsi Kanisa linavyofunuliwa kwa namna ya kivuli katika kufunuliwa kwa mpango wake wa neema ya wokovu ili kuwajumuisha Mataifa katika kazi yake kwa njia ya Kristo Yesu, na utajifunza pia kuhusu nia ya Mungu ya kujitengenezea watu wa kipekee, laos wa Mungu. Pia utagundua utajiri wa wokovu na maana ya wokovu, nini maana ya kuokolewa kutoka katika upotevu na kutengwa na Mungu kunakosababishwa na dhambi. Kupitia muungano wetu na Kristo tunaunganishwa na “watu wa Mungu” wanaorithi Ufalme aliouahidi. Kuunganishwa na Kristo ni kuunganishwa na watu wake, wale ambao tumaini lao liko katika ahadi ya Mungu kuumba mbingu mpya na nchi mpya, yenye jamii mpya ya wanadamu chini ya utawala wa Mungu ambao utaondoa kabisa madhara ya dhambi na kifo duniani. Katika somo letu la pili, Kanisa katika Ibada , tutazingatia wokovu kama msingi wa ibada ya Kanisa. Tutaona kwamba wokovu unapatikana kwa neema ya Mungu pekee na kwamba wanadamu hawawezi kuupata kwa juhudi zao au kuustahili. Hivyo, kuabudu ni mwitikio sahihi kwa neema ya Mungu. Pia tutaanganzia baadhi ya mawazo yanayotokana na tafakari ya Kikristo kuhusu ibada ya Kanisa, ikijumuisha uchambuzi mfupi wa maneno “sakramenti” na “maagizo” pamoja na maoni tofauti kuhusu Ubatizo na Meza ya Bwana katika muktadha wa ibada ya Kanisa. Zaidi ya hayo, tutagundua madhumuni ya kitheolojia ya ibada ya Kanisa, ambayo ni kumtukuza Mungu kwa sababu ya utakatifu wake wa pekee, uzuri wake usio na kikomo, utukufu wake usio na kifani na kazi zake zisizoweza

6 /

THEOLOJIA YA KANISA

kulinganishwa na chochote. Kwa kumkaribia Mungu wa Utatu kwa njia ya Yesu Kristo, Kanisa linaabudu kwa njia ya sifa na shukrani, na kwa njia ya Liturujia inayojikita katika mkazo wa Neno na Sakramenti. Kanisa pia humwabudu Mungu kupitia utii wake na mtindo wa maisha kama jumuiya ya agano. Somo la tatu linaitwa Kanisa kama Shahidi , na linaangazia utume wa Kanisa. Katika somo hili tutashughulikia vipengele muhimu zaidi vya fundisho la uteule jinsi linavyotumika kuhusiana na Yesu Kristo kama mteule wa Mungu, kuhusiana watu wake wateule Israeli na Kanisa, na kuhusiana na waamini binafsi. Tutamwona Yesu Kristo kama Mteule wa Mungu, Yule ambaye kupitia kwake Mungu anaokoa watu kutoka katika ulimwengu kwa ajili yake mwenyewe, na kuchunguza kwa ufupi vipengele na ufafanuzi wa dhana ya watu waliochaguliwa na Mungu kama inavyofafanuliwa kupitia Israeli kama watu wa Mungu na kupitia Kanisa la Yesu Kristo. Kanisa kama chombo cha Mungu cha Utume wake Mkuu, tutaona vipengele vitatu muhimu ndani yake: Kanisa linatoa ushahidi linapowahubiria waliopotea, linapobatiza waamini wapya katika Kristo, yaani, kuwajumuisha kama washiriki katika Kanisa, na linapowafundisha washirika wake kushika mambo yote ambayo Kristo aliamuru. Hatimaye, katika somo la nne, Kanisa katika Kazi , tutaona vipengele mbalimbali vya Kanisa. Tutaangazia kipekee jinsi tunavyoweza kugundua kusanyiko halisi la Kikristo kwa kuzingatia vigezo fulani ambavyo vimethibitishwa kuwa ishara za kweli za matendo na mtindo wa maisha wa Kanisa. Tutazingatia alama za Kanisa kulingana na Kanuni ya Imani ya Nikea, na vile vile kulingana na mafundisho ya Vuguvugu la Matengenezo. Pia tutalitazama Kanisa kwa msingi wa Kanuni ya Vincent, ambayo ni mwongozo muhimu wa kuelewa na kutathmini mapokeo na mafundisho yanayodai kuwa ya lazima kwa Wakristo. Tutamalizia kozi hii kwa kukazia huduma ya Kanisa kupitia taswira mbalimbali za Kanisa zilizotajwa katika Agano Jipya, taswira ya nyumba ya Mungu (familia ya Mungu), kupitia taswira ya mwili wa Kristo na Hekalu la Roho Mtakatifu (wakala wa Ufalme wa Mungu). Pia tutaangalia kupitia dhana ya Jeshi la Mungu jinsi Kanisa linavyopigana katika vita vya Mwana-Kondoo. Taswira hizi zinatoa ufahamu mkubwa wa jinsi tunavyopaswa kuuelewa utambulisho wa Kanisa na kazi yake ulimwenguni leo. Bila shaka, Kanisa la Yesu Kristo ni wakala wa Mungu kwa ajili ya Ufalme wake, na watu wa uwepo wake. Kujifunza kwako moduli hii na Neno la Mungu kuzae ndani yako upendo wa kina kwa watakatifu wa Mungu na kujitoa kwa dhati kuishi kwa ajili ya kulijenga Kanisa! Mungu akubariki sana unapojifunza Neno lake Takatifu kwa bidii!

~Mchungaji Dr. Don L. Davis

/ 7

THEOLOJIA YA KANISA

Mahitaji ya Kozi

• Biblia (kwa madhumuni ya kozi hii, Biblia yako inapaswa kuwa tafsiri [mf. BHN, SUV, NEN, SRUV, au NIV, NASB, RSV, KJV, NKJV, n.k. ikiwa utatumia Biblia ya Kiingereza], na sio Biblia iliyofafanuliwa [mf. The Living Lible, The Message]). • Kila moduli katika Mtaala wa Capstone imeainisha vitabu vya kiada ambavyo vinatakiwa visomwe na kujadiliwa katika muda wote wa kujifunza moduli husika. Tunakuhimiza kusoma, kutafakari, na kufanya kazi husika pamoja na wakufunzi wako, wasimamizi, na wanafunzi wenzako. Kutokana na uhaba wa vitabu unaoweza kujitokeza kwa sababu kadha wa kadha (k.m., kushindwa kuchapisha vitabu vya kutosha), tunaweka orodha yetu ya vitabu rasmi vya Capstone vinavyohitajika kwenye tovuti yetu. Tafadhali tembelea www.tumi.org/books ili kupata orodha ya vitabu vinavyohitajika kwa ajili ya moduli hii. • Daftari na kalamu kwa ajili ya kuchukua maelezo na kufanyia kazi za darasani. • Allen, Roland. The Spontaneous Expansion of the Church . Grand Rapids: Eerdmans, 1962. • Costas, Orlando. The Church and Its Mission: A Shattering Critique from the Third World . Wheaton: Tyndale Press, 1974. • Green, Michael. Evangelism in the Early Church . Grand Rapids: Eerdmans, 1970. • Richards, Lawrence. A New Face for the Church . Grand Rapids: Zondervan, 1970.

Vitabu na Nyenzo Zingine Zinazohitajika

Vitabu vya Kusoma

8 /

THEOLOJIA YA KANISA

Muhtasari wa Mfumo wa Kutunuku Matokeo na Uzito wa Gredi

Mahitajai ya Kozi

Mahudhurio na Ushiriki Darasani

30% alama 90 10% alama 30 15% alama 45 15% alama 45 10% alama 30 10% alama 30

Majaribio

Kukariri Maandiko

Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko

Kazi ya Huduma

Kazi za Usomaji na za Kufanyia Nyumbani

Mtihani wa Mwisho

10% alama 30 Jumla: 100% alama 300

Mambo ya Kuzingatia katika Utoaji Maksi

Kuhudhuria kila kipindi ni moja ya masharti ya msingi ya kozi hizi. Kukosa kipindi kutaathiri matokeo yako. Ikiwa una dharura isiyoepukika itakayokulazimu kukosa kipindi, tafadhali mjulishe mkufunzi wako mapema. Ukikosa kipindi ni jukumu lako kutafuta taarifa kuhusu kazi na mazoezi yaliyotolewa, na kuongea na mkufunzi wako pale inapobidi kufanya na kukabidhi kazi kwa kuchelewa. Sehemu kubwa ya mafunzo yanayohusiana na kozi hii hufanyika kupitia mijadala. Kwa sababu hiyo, unahimizwa na kutarajiwa kushiriki kikamilifu katika kila kipindi cha kozi hii. Kila kipindi kitaanza na jaribio fupi kuhusu mawazo ya msingi yaliyofundishwa katika somo lililopita. Njia nzuri zaidi ya kujiandaa na majaribio haya ni kupitia Kitabu cha Mwanafunzi na daftari uliloandikia maelezo ya somo hilo lililopita. Kukariri Neno la Mungu ni kipaumbele cha msingi kwa maisha na huduma yako kama mwamini na kiongozi katika Kanisa la Yesu Kristo. Kozi hii ina mistari ya Biblia michache, lakini yenye umuhimu mkubwa katika jumbe zake. Katika kila kipindi utahitajika kukariri na kunukuu (kwa mdomo au kuandika) mistari ya Biblia uliyopewa na mkufunzi wako. Neno la Mungu ni zana yenye nguvu ambayo Mungu anaitumia ili kuwaandaa watumishi wake kwa kila kazi ya huduma aliyowaitia (2 Tim. 3:16-17). Ili kutimiza matakwa ya kozi hii, lazima uchague kifungu cha Biblia na kufanya uchambuzi wa kina (yaani, eksejesia au ufafanuzi wa Maandiko). Kazi yako iwe na kurasa tano (ziliyochapwa kwa kuacha nafasi mbili kati ya mistari au kuandikwa vizuri kwa mkono), na kushughulikia mojawapo ya vipengele vinne vya Kanisa vinavyozungumziwa katika masomo manne ya kozi hii. Ni shauku na matumaini yetu kwamba utashawishika kikamilifu na kuamini juu ya uwezo wa Maandiko kuleta badiliko na athari chanya katika maisha yako na ya wale unaowahudumia.

Mahudhurio na Ushiriki Darasani

Majaribio

Kukariri Maandiko

Kazi za Ufafanuzi wa Maandiko

/ 9

THEOLOJIA YA KANISA

Unapoendelea kujifunza kozi hii, uwe huru kuongeza mistari kadhaa katika uchambuzi wako (takriban mistari 4-9) kuhusu jambo ambalo ungependa kujifunza kwa kina. Maelezo yote kuhusiana na kazi hii yametolewa katika ukurasa wa 10-11, na yatajadiliwa katika sehemu ya utangulizi ya kozi hii. Matarajio yetu ni kwamba wanafunzi wote watatumia mafunzo haya kivitendo katika maisha yao na katika majukumu yao ya kihuduma. Mwanafunzi atakuwa na jukumu la kufikiria namna ya kufanya mafunzo ya huduma kwa vitendo kwa kutumia kanuni alizojifunza katika mazingira halisi ya huduma. Maelezo ya namna ya kufanya mafunzo kwa vitendo yanapatika katika ukurasa wa 12, na yatajadiliwa katika kipindi cha utangulizi wa kozi. Mkufunzi wako anaweza kutoa kazi za darasani na kazi za nyumbani za aina mbalimbali wakati wa vipindi vya masomo au anaweza kuziandika katika Kitabu cha Mwanafunzi ulichonacho. Ikiwa una swali lolote kuhusu kile kinachohitajika kuhusiana na kazi hizi au muda wa kuzikusanya, tafadhali muulize mkufunzi wako. Ni muhimu kwa kila mwanafunzi kusoma maeneo yote ambayo inampasa kusoma katika vitabu husika vya kozi hii au katika Maandiko Matakatifu ili kujiandaa kwa ajili ya mijadala darasani. Tafadhali hakikisha unajaza na kukabidhi kwa Mkufunzi wako “Fomu ya Ripoti ya Usomaji” iliyomo katika Kitabu cha Mwanafunzi, kila wiki. Kutakuwa pia na fursa ya kupata alama za ziada endapo utasoma zaidi ya ulivyoagizwa. Mwishoni mwa kozi, Mkufunzi wako atakupa mtihani wa mwisho utakaofanyia nyumbani. Katika mtihani huu hautaruhusiwa kutumia vitabu vyako vya kozi hii isipokuwa Biblia. Utaulizwa swali ambalo litakusaidia kutafakari juu ya yale uliyojifunza katika kozi na namna yanavyoathiri mfumo wako wa fikra na utendaji wako katika huduma. Utakapokabidhiwa mtihani wa mwisho, mkufunzi wako atakupa taarifa zaidi kuhusu tarehe za kukamilisha na kukabidhi mtihani wako na kazi nyinginezo.

Kazi ya Huduma

Kazi za Darasani na za Nyumbani

Kazi za Usomaji

Mtihani wa Mwisho wa Kufanyia Nyumbani

Gredi za Ufaulu

Mwishoni mwa kozi hii, gredi zifuatazo zitatolewa na kuhifadhiwa kwenye mbukumbu za kila mwanafunzi: A – Kazi Bora D – Inaridhisha B – Nzuri sana F – Hairidhishi (Feli) C – Nzuri I – Isiyokamilika

1 0 /

THEOLOJIA YA KANISA

Matokeo ya mwisho wa kozi yatatolewa katika mfumo wa gredi kwa kutumia skeli ya kutunuku matokeo kwa mtindo wa herufi zenye alama chanya na hasi, kisha alama za gedi yako ya ufaulu katika kazi mbali mbali zitajumlishwa na kugawanywa kwa idadi ya kazi na vipimo vingine husika ili kupata wastani wa matokeo yako ya mwisho. Kuchelewesha au kushindwa kabisa kukabidhi kazi zako kutaweza kuathiri matokeo yako. Hivyo, ni vyema kupangilia shughuli na muda wako mapema na kuwasiliana na mkufunzi wako endapo kutakuwa na changamoto yoyote. Kama sehemu ya ushiriki wako katika moduli ya Theolojia ya Kanisa , utahitajika kufanya ufafanuzi (uchambuzi wa kina) wa mojawapo ya vifungu vifuatavyo vya Neno la Mungu:  Warumi 12:3-8  Wagalatia 3:22-29  1 Wakorintho 12:1-27  Waefeso 2:11-22  Waefeso 4:1-16  1 Petro 2:9-10 Madhumuni ya kazi hii ni kukupa fursa ya kufanya uchunguzi wa kina wa andiko mojawapo muhimu kuhusu Kanisa. Unaposoma kwa kina, kutafakari, na kujifunza juu ya mojawapo ya vifungu hivi, matumaini yetu ni kwamba utaweza kuelewa na pia kuonyesha jinsi kifungu hiki kinavyoangazia au kuweka wazi kipengele fulani cha maono ya Mungu kwa watu wake. Na bila shaka, katika kulielewa Kanisa vyema, maombi yetu ni kwamba utakuwa na ufanisi zaidi katika kuhusianisha kweli hizi na mwenendo wako binafsi wa ufuasi, uongozi wako katika kanisa lako, na huduma yako mjini. Hii ni kazi ya kujifunza Biblia, na ili kufanya kazi ya eksejesia , ni lazima udhamirie kuelewa maana ya andiko husika katika muktadha wake. Ukishajua andiko lilimaanisha nini kwa wasomaji wake wa kwanza, unaweza kupata kanuni zinazotuhusu sisi sote leo, na kuzihusianisha kanuni hizo na maisha. Mchakato wa hatua tatu rahisi unaweza kukuongoza katika jitihada zako binafsi za kujifunza kifungu cha Biblia: 1. Je, Mungu alikuwa akisema nini kwa watu katika muktadha wa asili wa andiko husika? 2. Ni kanuni gani ambazo andiko hili linafundisha ambazo ni kweli kwa watu wote kila mahali, ikiwa ni pamoja na sisi leo? Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko (Eksejesia)

Dhumuni

Mpangilio na Muundo

/ 1 1

THEOLOJIA YA KANISA

3. Ni kitu gani Roho Mtakatifu ananiagiza kufanya kupitia kanuni hii, leo, katika maisha na huduma yangu? Baada ya kuwa umeyajibu maswali haya katika kujifunza kwako kibinafsi, hapo sasa utakuwa tayari kuendelea kuandika ulichokigundua katika kazi uliyopewa . Angali hapa chini mfano wa muhtasari wa kazi yako: 1. Eleza kile unachoamini kuwa ndio mada kuu au wazo kuu la andiko ulilochagua. 2. Eleza kwa muhtasari maana ya andiko hilo (unaweza kufanya hivi katika aya mbili au tatu, au, ukipenda, kwa kuandika ufafanuzi mfupi wa mstari kwa mstari juu ya kifungu husika). 3. Eleza kanuni kuu moja hadi tatu au maarifa ambayo kifungu hiki kinatoa kuhusu Yesu Kristo na kazi yake. 4. Eleza jinsi kanuni moja, kadhaa, au zote zinaweza kuhusiana na yafuatayo: Kwa msaada au mwongozo, tafadhali uwe huru kusoma vitabu vya rejea vya kozi hii na/au vitabu vya mafafanuzi ( commentaries ), na kutumia maarifa yaliyomo katika vyanzo hivyo katika kazi yako. Unapotumia maarifa au mawazo ya mtu mwingine kujenga hoja zako, hakikisha unatambua kazi za waandishi husika kwa kutaja vyanzo vya taarifa hizo. Astahiliye heshima apewe heshima yake. Tumia marejeleo ya ndani ya maandishi ( in-text-refences ), tanbihi ( footnotes ), au maelezo ya mwisho ( endnotes ). Njia yoyote utakayochagua kutaja rejea zako itakubalika, ilimradi 1) utumie njia hiyo moja katika kazi nzima, na 2) uonyeshe pale unatumia mawazo ya mtu mwingine, na umtambue mwandishi husika kwa kumtaja. (Kwa maelezo zaidi, angalia katika Kiambatisho cha Namna ya Kuandika Kazi Yako: Mwongozo wa Kukusaidia Kutambua Waandishi wa Vitabu vya Rejea ). Kabla hujakabidhi kazi yako, hakikisha inasifa zifuatazo: • Imeandikwa au kuchapwa vizuri na inasomeka na kueleweka. a. Kiroho chako binafsi na namna unavyotembea na Kristo b. Maisha na huduma yako katika kanisa lako la mahali pamoja c. Hali au changamoto katika jamii yako kwa ujumla.

• Ni uchambuzi wa mojawapo ya vifungu hapo juu. • Imekusanywa kwa wakati (haijacheleweshwa). • Ina urefu wa kurasa 5.

1 2 /

THEOLOJIA YA KANISA

• Inafuata muhtasari au mpangilio uliotolewa hapo juu, na imeandikwa kwa namna ambayo msomaji ataweza kuelewa. • Inaonyesha jinsi kifungu husika kinavyohusiana na maisha na huduma leo. Usiruhusu maagizo haya yakuogopeshe; hii ni kazi ya kujifunza Biblia! Unachohitaji kuonyesha katika kazi hii ni kwamba ulisoma andiko husika, umeeleza kwa muhtasari maana yake, ukaweza kupata kanuni chache muhimu kutoka katika andiko hilo, na kuzihusianisha na maisha na huduma yako mwenyewe. Kazi ya ufafanuzi inabeba alama 45 na inawakilisha 15% ya jumla ya maksi zako, hivyo hakikisha kwamba unaifanya kazi yako kuwa bora na yenye maarifa ya kutosha ya Neno la Mungu. Neno la Mungu li hai na linafanya kazi, na hupenya hadi kwenye kiini cha maisha yetu na mawazo ya ndani kabisa (Ebr. 4:12). Mtume Yakobo anaweka msisitizo zaidi juu ya kuwa watendaji wa Neno la Mungu, sio wasikiaji tu, tukijidanganya wenyewe. Tunahimizwa kulifanyia kazi, kulitii. Anaongeza kusema kwamba kupuuza nidhamu hii ni sawa na sisi kujitazama sura zetu za asili katika kioo na mara tunapoondoka tunasahau asili yetu (sis ni nani) na tulichokusudiwa kuwa. Katika kila hali, mtendaji wa Neno la Mungu atabarikiwa katika kila atendalo (Yak. 1:22-25). Shauku yetu ya dhati ni kwamba uweze kutumia maarifa unayojifunza kwa vitendo, ukiihusianisha elimu hii na masuala na mahitaji halisi katika maisha yako binafsi, na huduma yako ndani ya kanisa lako na kupitia kanisa lako. Kwa hivyo, sehemu hii muhimu ya kukamilisha moduli hii itakuhitaji kubuni kazi ya huduma kwa vitendo ili kukusaidia kushirikisha wengine baadhi ya maarifa ambayo umejifunza katika kozi hii. Andiko la 1 Petro 2:9-10 linalielezea Kanisa kama taifa, ukuhani, na watu. Hakuna neno lolote kati ya haya linaloturuhusu kuuelewa wokovu wetu kama suala la mtu binafsi lisilohusiana na kusanyiko. Lengo la kazi hii ya huduma kwa vitendo ni kukusaidia kuimarisha ujuzi wako katika kuelezea uhusiano kati ya wokovu na Kanisa. Tafadhali kamilisha kila moja ya hatua zifuatazo: Tambua na uelezee kwa ufupi kwa maandishi hali fulani katika uzoefu wako wa zamani au wa sasa ambapo mtu unayemjua anadai kwamba hafikirii Kanisa kuwa ni sehemu muhimu ya maisha yake ya kiroho. (Unaweza kutumia jina la kubuni kwa ajili ya mtu huyu ikiwa ungependelea kuficha utambulisho wake). Namna hii ya kuliupuuzia Kanisa inajidhihirisha katika maneno yake; “Sijisikii kama ni Kazi ya Huduma

Utoaji Maksi

Dhumuni

Mpangilio na Muundo

Hatua ya Kwanza

/ 1 3

THEOLOJIA YA KANISA

lazima niende kanisani ili kumwabudu Mungu!” Au inaweza kujionyesha katika tabia yake; anadai kuwa ni mkristo mzuri lakini mahudhurio yake kanisani ni ya mara chache sana. Andika mfano wa barua kwa mtu huyu ukianisha kwa maneno yako mwenyewe sababu ambazo zinakufanya uamini kwamba ameelewa vibaya kile ambacho Biblia inafundisha kuhusu wokovu na Kanisa. Maudhui ya barua hiyo yanapaswa kutokana na theolojia ambayo umejifunza katika kozi hii, na yaonyeshe ufahamu wako wa theolojia hiyo. Lengo la barua hii ni kuhamishia mawazo na dhana za kitheolojia katika uzoefu wa kivitendo. Hili si “andiko la kitheolojia,” bali ni wasilisho la mafundisho ya kibiblia ya kweli kwa mtu ambaye anaonyesha kuwa na uelewa potofu wa Maandiko au ameamua kwa makusudi kuyaasi Maandiko. Kabidhi nakala ya barua kwa mwalimu wako. Kisha, tafakari katika maombi ikiwa Mungu anaweza kukuruhusu umfikie mtu uliyeandika habari zake (ikiwa ni jambo lililopo sasa) na umtumie barua hiyo au kuzungumza naye ana kwa ana kuhusu wokovu wake na maisha ya kanisa. Kazi ya huduma inabeba alama 30 ambazo zinawakilisha 10% ya jumla ya maksi zako, hivyo hakikisha unashirikisha yale uliyojifunza kwa ujarisi na ripoti yako iwe yenye kueleweka vizuri.

Hatua ya Pili

Hatua ya Tatu

Utoaji maksi

/ 1 5

THEOLOJIA YA KANISA

Ufunuo Kivuli wa Kanisa katika Mpango wa Mungu

SOMO LA 1

Karibu katika jina la uweza la Yesu Kristo! Baada ya kusoma, kujifunza, kujadili, na kutumia maarifa ya somo hili, utaweza: • Kueleza jinsi Kanisa lilivyofunuliwa awali katika mpango wa Mungu uliotukuka, yaani, azimio la Mungu kujitukuza mwenyewe kupitia jamii mpya ya wanadamu kupitia agano ambalo alilifanya na Abrahamu. • Kufafanua Maandiko na dhana muhimu zinazohusiana na ufunuo wa awali wa Kanisa katika mpango wa Mungu wa neema ya wokovu unaoendelea kujifunua, lengo lake la kufunua siri kuu ya kuwajumuisha mataifa katika Kristo Yesu. • Kufafanua na kuelezea kwa kina jinsi Kanisa lilivyofunuliwa awali katika mpango wa Mungu katika Maandiko, kwamba tangu mwanzo, dhamira ya Mungu ilikuwa kujitengenezea watu wa kipekee, laos wa Mungu. • Kutoa tafsiri ya kibiblia ya wokovu na kuelewa jinsi inavyohusiana na ushirika katika Kanisa. • Kukariri kifungu cha Biblia kinachoelezea Kanisa kwa muktadha wa uhusiano wake na watu wa Mungu wa Agano la Kale. Soma 1 Petro 2:9-10. Neno «kanisa» linaweza kuleta picha mbalimbali akilini mwetu. Kwa watu wengi, wanaposikia neno «kanisa,» wanawaza jengo lenye msalaba juu yake. Lakini sivyo Mtume Petro alivyofikiria kuhusu Kanisa. Kwa Petro, Kanisa ni kundi la kipekee la watu waliochaguliwa na Mungu kumtumikia na kuliwakilisha Jina lake duniani. Katika mistari hii, Petro anatumia lugha ile ile ambayo Mungu alitumia kwa wana wa Israeli katika Kutoka 19:5-6 alipowaambia: “Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu, nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli.” Petro, akijua kuwa anaongea na Kanisa ambalo linajumuisha Wamataifa, anaongeza haraka: “ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata Taifa Takatifu

Malengo ya Somo

1

Ibada

1 6 /

THEOLOJIA YA KANISA

rehema, bali sasa mmepata rehema.” Kanisa ni watu waliochaguliwa na Mungu, makuhani wake wanaomwabudu, na kati ya mataifa yote, Kanisa sasa ni taifa la Mungu linaloishi duniani kulingana na maadili ya Ufalme wa Mungu. Jukumu letu ni kuishi kwa namna ambayo yeyote anayetaka kujua jinsi dunia inayoongozwa na Mungu inavyoonekana, anaweza kujua kwa kuliangalia Kanisa. Huu ni upendeleo wa ajabu na wito wa hali ya juu. Baada ya kukiri na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (iliyopo kwenye viambatisho), omba maombi yafuatayo: Mungu wa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo, asante sana kwa kutujumuisha sisi sote tuliomwamini Yesu kama watoto wa Ibrahimu na warithi wa ahadi ulizompa. Baba, tusaidie kukuwakilisha vyema katika dunia hii ya dhambi. Tusaidie kuwa tofauti na mataifa yanayotuzunguka ili tuangaze kama mji ulioko juu ya mlima. Tusaidie kufanya matendo mema yanayowawezesha watu kuuelewa moyo wako na kukutukuza wewe, Baba yetu wa mbinguni. Na zaidi ya yote, tusaidie kutangaza kwa ujasiri habari njema za Yesu ili kila mtu apate fursa ya kuwa miongoni mwa watu wako uliowachagua. Tunaomba haya kupitia Yesu Kristo Bwana wetu, anayemiliki pamoja nawe na Roho Mtakatifu, Mungu mmoja, milele na milele. Amina.

Kanuni ya Imani ya Nikea na maombi

1

Hakuna jaribio katika somo hili.

Jaribio

Hakuna Maandiko ya kukariri katika somo hili.

Mapitio ya Kukariri Maandiko

Hakuna kazi za kukabidhi katika somo hili.

Kazi za Kukabidhi

MIFANO YA REJEA

Muda Mwingi Umetumika kwa ajili ya Wakati Ujao

Baada ya semina ambayo mchungaji alikuwa akifundisha kuhusu siku za mwisho, mmoja wa waamini alitoa maoni baadaye katika maegesho ya magari, akisema: “Sielewi kabisa kwa nini tunahitaji kutumia muda mwingi sana kuzungumzia mambo ya ile picha kubwa. Hii ndiyo sababu Kanisa linachosha watu wengi – hatujui jinsi ya kuwekea mkazo mambo yanayotokea leo. Kila kitu ni ndoto

1

/ 1 7

THEOLOJIA YA KANISA

za mbinguni, paradiso ya siku za baadaye, kusudi fulani la kiungu kuhusu kile ambacho Mungu atafanya siku moja. Sielewi kwa nini tunapaswa kila mara kuzungumzia mambo haya ya ile picha kubwa. Ninahitaji kujikita katika kile ninachopaswa kufanya leo!” Je, ungemjibuje muumini aliyelemewa kwa njia hii?

Utambulisho

Chukua kipande cha karatasi na chora seti ya alama au picha ndogo ambazo zingemsaidia mtu asiyejua chochote kuhusu wewe apate kuelewa wewe ni nani na ni mambo gani yanayokushughulisha. Kisha fuata maelekezo ambayo Mkufunzi wako atakupa kabla ya kuwaonyesha wengine picha hizo.

2

1

Waliokolewa na Waliopotea

Maandiko yanazungumza mara nyingi juu ya watu “waliokolewa” na “waliopotea.” Kwa mtu ambaye hajawahi kusikia Injili, lugha hii inaweza kuwa ngumu kuelewa. Maswali ya msingi yanayoweza kujitokeza ni: “Tumeokolewa dhidi ya nini?” na “Unamaanisha nini unaposema kuwa nimepotea?” Je, ungemjibuje mtu anayekuuliza maswali haya?

3

Ufunuo Kivuli wa Kanisa katika Mpango wa Mungu Sehemu ya 1

YALIYOMO

Mchungaji Dkt. Don L. Davis

Kanisa limefunuliwa kwa namna ya kivuli katika mpango wa Mungu uliotukuka kwa ajili yake mwenyewe; amekusudia kujitukuza mwenyewe kwa kuwakomboa wanadamu wapya kupitia agano ambalo alifanya na Ibrahimu. Limefunuliwa pia katika mchakato wa kufunuliwa kwa mpango wake wa neema ya wokovu, ambao unajumuisha kusudi la ajabu la kuwahusisha mataifa katika makusudi yake ya Ufalme. Hatimaye, Kanisa limetabiriwa katika picha iliyofunuliwa na Maandiko ya Mungu ya kuumba kwa ajili yake watu wa kipekee, yaani laos wa Mungu.

Muhtasari wa Sehemu ya 1

1 8 /

THEOLOJIA YA KANISA

Lengo letu katika sehemu hii ya kwanza ya Ufunuo Kivuli wa Kanisa katika Mpango wa Mungu ni kukuwezesha kuona kwamba: • Kanisa lilifunuliwa tangu awali katika kusudi kuu la Mungu la kujitukuza mwenyewe kupitia jamii mpya ya wanadamu watakaoishi pamoja naye milele. • Kanisa lilifunuliwa awali katika ahadi ya Mungu ya kuwajumuisha Wamataifa katika mpango wake wa ukombozi kwa ulimwengu. • Kanisa lilifunuliwa awali katika jitihada za Mungu za kujitengenezea watu ( laos ) watakaoishi kwa ajili yake kama watu wake wa pekee. • Mungu anafanya kazi kupitia historia ya wanadamu ili kujichagulia watu wake kutoka katika mataifa yote duniani.

1

I. Kanisa la Yesu Kristo lilifunuliwa awali katika mpango wa Mungu uliotukuka: Kujiletea utukufu kupitia jamii mpya ya wanadamu, kulingana na tangazo la awali la Injili katika Agano na Ibrahimu.

Muhtasari wa Sehemu ya Kwanza ya Video

A. Kusudi kuu la Mungu ni kuliletea heshima Jina lake.

1. Uumbaji wote ulifanyika kwa mapenzi yake na kwa nguvu zake, na kwa ajili ya utukufu wake.

a. Kut. 20:11

b. Isa. 40:26-28

c. Yer. 32:17

2. Mwandishi wa Zaburi anasema kwamba ilikuwa kwa utukufu wake Mungu alipochagua na kutekeleza mpango wake wa ukombozi kwa watu wake Israeli na kuwashinda adui zake katika mpango wake, Zab. 135:8-12.

/ 1 9

THEOLOJIA YA KANISA

B. Agano la Mungu na Ibrahimu: Kupitia yeye, jamaa zote za dunia zitabarikiwa, Mwa. 12:1-3. Andiko hili linafunua kwa uwazi kwamba:

1. Kupitia uzao wa Ibrahimu, jamaa zote za dunia zitabarikiwa.

2. Ahadi hii itatimizwa kwa kazi ya Mungu ya kiungu kupitia ukoo wa Ibrahimu.

1

C. Agano hili lilidhihirisha mpango wa Mungu uliotukuka wa kujichagulia watu kutoka duniani kote kwa ajili yake, wakiwemo Wamataifa, wote wakikombolewa kupitia Mwanawe, Yesu Kristo, Gal. 3:6-9. Andiko hili lina maana kadhaa muhimu kuhusu jinsi Kanisa lilivyofunuliwa kupitia agano la Ibrahimu.

1. Imani ya Abrahamu ilihesabiwa kuwa haki.

2. Waamini wanaunganishwa na ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu.

3. Maandiko yaliona mbele kwamba Mungu angewahesabia mataifa haki kwa imani katika agano la Ibrahimu.

II. Kanisa lilifunuliwa tangu awali kupitia mpango wa Mungu unaoendelea kufunuliwa: Katika Yesu Kristo, Mungu amefunua siri yake kwa ulimwengu wote kuhusu nia yake ya kujitengenezea watu kwa utukufu wake miongoni mwa Wayahudi na mataifa. Maandiko matatu yanayoonyesha wazi wazi ufunuo wa siri ya Mungu ya kuwakomboa mataifa kupitia ahadi yake kwa Ibrahimu.

2 0 /

THEOLOJIA YA KANISA

A. Andiko la Kwanza: Siri iliyofichwa kwa vizazi vingi sasa imefunuliwa kupitia manabii na mitume, Rum. 16:25-27. Andiko hili linaonyesha mambo kadhaa muhimu:

1. Siri hii: ni mahubiri ya Injili ya Yesu Kristo.

2. Mahubiri haya ya Yesu Kristo ni kulingana na ufunuo wa siri iliyokuwa imefichwa kwa miaka mingi.

1

3. Siri hii imefunuliwa kupitia mitume na manabii kwa mataifa yote kwa ajili ya kuwaleta katika utii wa imani.

B. Andiko la Pili: Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu kama ufunuo wa siri ya Mungu, Kol. 1:25-29. Maelezo muhimu tunayojifunza kuhusu siri hii ni:

1. Siri iliyokuwa imefichwa kwa vizazi na kwa miaka mingi sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake.

2. Mungu ameweka wazi miongoni mwa mataifa utajiri wa utukufu wa siri hii.

3. Siri hii ni Kristo ndani yenu, yaani mataifa, ambalo ni tumaini letu la utukufu.

C. Andiko la Tatu: Ufunuo wa siri ya ujumuishwaji wa mataifa katika Kanisa, Efe. 3:4-12. Siri ya Imani katika Kristo:

/ 2 1

THEOLOJIA YA KANISA

1. Haikufunuliwa kwa vizazi vya zamani lakini sasa imefunuliwa kwa mitume watakatifu wa Kristo na manabii kwa njia ya Roho.

2. Ni kwamba mataifa ni warithi wenza, washirika wa mwili mmoja, na washiriki wa ahadi katika Yesu Kristo kupitia imani katika Injili.

3. Kupitia huduma ya kitume, siri ya Mungu imewekwa wazi: kwamba kupitia Kanisa, Mungu angewajulisha watawala na wenye mamlaka katika ulimwengu wa roho hekima hii kuu ya Mungu.

1

III. Kanisa lilifunuliwa kupitia Taifa la Israeli, ambapo Mungu ametupatia picha ya watu wake wa pekee, Laos wa Mungu, 2 Kor. 6:16; 2 Thes. 2:13-14.

A. Israeli ni chombo ambacho kupitia hicho Masihi angekuja.

1. Israeli ni jina alilopewa Yakobo baada ya pambano lake kuu la maombi na malaika, Mwa. 32:28.

2. Hili ndilo jina la jumla walilopewa wazawa wa Yakobo.

a. Makabila kumi na mawili yanaitwa “Waisraeli.”

b. “Wana wa Israeli,” Yosh. 3:17; 7:25; Amu. 8:27; Yer. 3:21.

c. “Nyumba ya Israeli,” Kut. 16:31; 40:38.

2 2 /

THEOLOJIA YA KANISA

3. Ukoo huu wa kimwili wa Ibrahimu ulichaguliwa kwa msingi wa uaminifu wa Mungu kwa agano lake na Abrahamu, Kum. 7:6-8.

4. Uchaguzi wa Mungu na agano lake na Abrahamu, Isaka, na Yakobo viliendelea kwa kizazi chao. Masihi alipaswa kuja kupitia taifa la Israeli, na kupitia yeye, wokovu kwa ulimwengu wote.

a. Kutoka 19:5-6

1

b. Kumb. 14:2

c. Kumb. 26:18-19

d. Yohana 4:22

5. Israeli inatambulika kama watu wa Mungu: taz. Kut. 15:13, 16; Hes. 14:8; Kum. 32:9-10; Isa. 62:4; Yer. 12:7-10; Hosea 1:9-10.

6. Watu wa mataifa walifunuliwa awali kama watu wa Mungu, Rum. 9:24-26.

B. Picha ya Israeli kama watu wa Mungu sasa inatumika kwa Kanisa kama jamii ya kifalme ya agano la Mungu.

1. Kanisa, kama watu wapya wa Mungu, Wayahudi na mataifa, sasa wamekuwa watu wa Mungu, 1 Pet. 2:9-10.

a. Kanisa la Mungu halitambuliki kwa njia ya tohara bali kwa uumbaji mpya kupitia imani katika Yesu, 2 Kor. 5:17 (rej. Fil. 3:2-3).

/ 2 3

THEOLOJIA YA KANISA

b. Kanisa la Mungu halihusiani kwa misingi ya utaifa, bali kwa msingi wa agano jipya lenye msingi wake katika imani ndani ya Kristo, lililotiwa muhuri na Roho Mtakatifu na ambalo Roho anakaa ndani yake, 2 Kor. 3:3-18.

2. Ahadi walizopewa waisraeli sasa limepewa Kanisa.

a. 2 Kor. 6:16-18

1

b. Kutoka 29:45

c. Mambo ya Walawi 26:12

3. Ingawa Kanisa limepewa nafasi maalum, Israeli haijaachwa wala uteuzi wake haujafutwa.

a. Kama Zakaria alivyotangaza kutimizwa kwa agano katika Kristo, Luka 1:67-79, ndivyo Paulo anavyosisitiza kwamba Neno la Mungu bado linasimama, Rom. 9:6.

b. Mungu Mwenyezi hajawakataa watu wake, Rumi. 11:1.

c. Israeli, ambayo imeitwa na Mungu, itaokolewa kwa kuwa “karama na wito wa Mungu haviwezi kubatilishwa,” Rumi. 11:25-26, 29.

d. Neema ya Mungu ni msingi wenye uhakika kwamba Israeli itaokolewa, Rumi. 9:27-29; Isa. 1:24-26.

2 4 /

THEOLOJIA YA KANISA

Hitimisho

» Kanisa lilifunuliwa katika kusudi kuu la Mungu: azma yake ya kujiletea utukufu kwa ajili ya nafsi yake mwenyewe kupitia jamii mpya ya wanadamu kwa njia ya agano lake na Abrahamu. » Kanisa lilifunuliwa awali katika kufunuliwa kwa siri kuu ya kujumuishwa kwa mataifa katika Kristo Yesu. » Kanisa lilifunuliwa awali katika picha ya Mungu ya watu wake, laos wa Mungu. Tafadhali chukua muda wa kutosha kujibu maswali haya na mengineyo ambayo yametokana na video. Kuanzia hapa, lazima tuwe wazi kabisa kuhusu mapenzi ya Mungu ya kuleta utukufu na heshima kwa nafsi yake, na jinsi jambo hilo linavyohusiana na kusudi lake kuu la kuwakomboa watu kutoka duniani kote kwa ajili yake. Mungu anatoa ishara ya wazi kuhusu kusudi lake la milele kupitia agano lake na Ibrahimu, ufunuo wa siri kuhusu ushiriki wa mataifa katika Habari Njema, na uumbaji wa watu wake, picha ya jamii mpya ya wanadamu itakayokuja. Kuwa wazi na ufupishe majibu yako, kadri inavyowezekana tumia Maandiko kuunga mkono hoja zako! 1. Ni kwa njia gani Mungu alifanya agano na Ibrahimu ili kwamba, kupitia kwake, familia zote za dunia zipate kubarikiwa? 2. Maandiko yanashuhudia nini kuhusu kusudi kuu la Mungu juu ya uumbaji wake, ufunuo wake mwenyewe, na ukombozi wake kwa wengine kwa ajili yake? Kwa nini Mungu aliumba ulimwengu? 3. Ni aina gani ya siri inayozungumziwa katika Warumi 16, Waefeso 3, na Wakolosai 1 kuhusu kusudi la Mungu la ukombozi? 4. Nini kinachoonyeshwa na Mungu kuhusu kusudi lake kwa mataifa linapokuja suala la kusudi lake la kuvuta watu kutoka duniani kote kwa ajili yake? Ni jinsi gani kusudi hili linaonyeshwa katika agano ambalo Mungu alifanya na Abrahamu? 5. Ni kwa njia gani Israeli ni chombo na njia ya Mungu kumleta Masihi duniani? Jinsi gani Israeli inaonyesha kupitia uhusiano wake na Mungu picha ya wazi ya watu wa Mungu, Kanisa?

1

Sehemu ya 1

Maswali kwa Wanafunzi na Majibu

/ 2 5

THEOLOJIA YA KANISA

6. Mitume walihusianishaje ahadi ya Mungu kwa Israeli na Kanisa la Mungu katika Kristo Yesu? Toa mifano. 7. Kanisa kupitia Kristo limepewa nafasi maalum katika mpango wa wokovu wa Mungu. Sasa, basi, Israeli ina nafasi gani kama watu wa Mungu? Je, Mungu ameiacha Israeli au kufuta uteuzi wake? Eleza.

Ufunuo Kivuli wa Kanisa katika Mpango wa Mungu Sehemu ya 2: Wokovu: Kujiunga na Watu wa Mungu

1

Mch. Terry Cornett

Kwa sababu ya dhambi, kila mwanadamu yuko katika hali inayoweza kuonekana kuwa ya kukata tamaa. Tunahitaji kuokolewa kwa haraka kutoka katika dhambi na madhara yake, lakini asili yetu ya dhambi inatufanya tusitamani wokovu wa Mungu wala kuwa na njia yoyote ya kurudishwa kwake. Cha kushangaza, Mungu alikataa kutuacha kama maadui wake. Mtume Paulo anafundisha kwamba ingawa tulikuwa tumefungiwa katika dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu. Injili ni habari njema kwamba Mungu ametoa neema ya wokovu ambayo inaweza kutufanyia yale ambayo hatuwezi kuyafanya sisi wenyewe. Kuelewa neema hii ndiyo msingi wa kutambua jukumu la Kanisa kama jamii ya waabudu. Lengo letu kwa ajili ya sehemu hii, Wokovu: Kujiunga na Watu wa Mungu , ni kukuwezesha: • Kutoa tafsiri ya kitheolojia ya wokovu. • Kuelezea madhara ya kutengwa na Mungu. • Kueleza faida zinazokuja kwetu kupitia umoja wetu na Kristo. • Kuelewa jinsi tendo la Kutoka ( Exodus ) linavyotumika kama (kivuli) mfano wa wokovu katika Kikristo. • Kuelewa kwamba kuingizwa katika Kanisa (watu wa Mungu) si kitu cha ziada kinachoongezwa baada ya wokovu bali ni jambo muhimu katika maana ya msingi kuokolewa.

Muhtasari wa Sehemu ya Pili

2 6 /

THEOLOJIA YA KANISA

I. Maana ya Wokovu

Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video

A. Neno la Kiyunani linalotafsiriwa kama wokovu katika Agano Jipya ni soteria . Linamaanisha kuokoa, kukomboa, au kumfanya mtu kuwa salama.

1. Rum. 1:16

2. 1 Thes. 5:9

1

3. 1 Pet. 1:9

B. Tafsiri ya Wokovu: Kwa mimi kama mtu binafsi, kuokolewa kunamaanisha kwamba: Kupitia kuunganishwa na Kristo, nimeokolewa kutoka katika upotevu na kutengwa na Mungu kulikosababishwa na dhambi, na hivyo kujiunga na “watu wa Mungu” wanaorithi Ufalme aliouahidi.

II. Wokovu wa kibiblia unamaanisha kuokolewa kutoka katika upotevu/kutengwa kulikosababishwa na dhambi.

A. Dhambi imemtenga mwanadamu na Mungu.

1. Mwa. 3:8

2. Isa. 59:2

3. Kol. 1:21

/ 2 7

THEOLOJIA YA KANISA

B. Kutengwa na Mungu kulikosababishwa na dhambi kunamaanisha kwamba wanadamu wamepotea. Wanadamu hawapo tena pale wanapopaswa kuwa, bali wamepotoka mbali na Mungu kama kondoo waliopotea. Katika Luka 15, Yesu alielezea hali ya mwanadamu iliyosababishwa na dhambi kwa kutumia dhana ya upotevu kabisa. Anasimulia hadithi zinazoonyesha kwamba wanadamu ni kama:

1. Mwana aliyepotea

1

2. Kondoo aliyepotea

3. Sarafu iliyopotea

Luka 19:10 Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kilichopotea.

C. Matokeo matatu ya kutengwa na Mungu ni Kifo, Utumwa, na Hukumu.

1. Kwa kuwa Mungu ndiye chanzo cha uzima wote, upotevu/kutengwa kunakosababishwa na dhambi kumeleta matokeo ya kifo, kama inavyoonyeshwa wazi katika kisa cha Adamu na Hawa.

a. Mwa. 2:16-17

b. Luka 15:24

c. Ona pia Warumi 5:12, Efe. 2:1

2. Kwa kuwa Mungu ndiye chanzo cha uhuru na ulinzi, upotevu/ kutengwa kwetu naye kumesababisha utumwa wetu chini ya dhambi na shetani.

2 8 /

THEOLOJIA YA KANISA

a. Yoh. 8:34

b. Rum. 6:20-21

c. Kol. 1:13

3. Kwa kuwa Mungu ndiye chanzo cha wema wote, upotevu wetu na kutengwa naye pamoja na matendo yetu maovu kumesababisha adhabu na hukumu.

1

a. Rum. 2:5-6 ( Ona pia Efe. 2:3)

b. Yoh. 3:36

III. Njia pekee ya watu kuokolewa ni kwa kuunganishwa na Kristo, na kupitia Yeye kuunganishwa na Mungu Baba.

A. Umoja na Kristo:

1. 2 Kor. 5:17

2. Yohana 15:5

3. Gal. 2:19b-20

4. Rum. 6:5

/ 2 9

THEOLOJIA YA KANISA

B. Umoja na Kristo una kipengele cha kisheria (kimahakama): Mungu aliweka hasira na hukumu yake juu ya Kristo ambaye alikufa badala yetu. Kupitia umoja na Kristo, tunashiriki katika kifo chake msalabani na hivyo, Mungu anazitambua dhambi zetu kuwa zimelipiwa gharama, na kwa neema anazisamehe.

1. Isa. 53:5

2. Ebr. 9:28

1

3. Kol. 2:13-14

Kwa kuwa imani ni tendo la kuamini katika Kristo na kuwa umoja na Kristo, huku kuhesabiwa haki si ujanja au kujifanya, kana kwamba Mungu anatangaza kuhusu sisi jambo ambalo halipo. Badala yake, kwa sababu ya umoja wetu na Kristo kwa njia ya imani (na kwa njia hiyo Kristo akiwa ndani yetu), Mungu anatangaza kile kilicho kweli. Ndiyo, Mungu anawehasabia haki wasiokuwa na haki, lakini ni pale tu wanapokuwa waamini katika Kristo na hivyo wameunganishwa na Yeye. Hivyo basi, mwenye dhambi anavikwa haki ya Kristo na kwa namna fulani anajulikana kuwa mwenye haki, lakini hili linatokea kwa njia ya imani inayomuunganisha mtu na Yesu Kristo... Hii haimanishi kwamba sisi si wenye dhambi tena, maana kwa kweli ndani yetu wenyewe sisi ni wenye dhambi. Lakini katika Kristo, sisi ni wenye haki kabisa! ~ J. Rodman Williams. Renewal Theology . Toleo la 2. Grand Rapids: Zondervan, 1996. uk. 74.

C. Umoja na Kristo una kipengele cha kiroho: Kwa sababu roho zetu zimeunganishwa na Roho wake, maisha ya Yesu yanatiririka kupitia kwetu na kutushindia dhidi ya ufisadi na kifo.

1. Rum. 8:10-11

2. Kol. 3:3-4

3 0 /

THEOLOJIA YA KANISA

D. Umoja na Kristo una kipengele cha ukombozi: Kwa sababu tumeunganishwa na mshindi aliyemshinda shetani, hatuwezi tena kushindwa na yule muovu. Kristo anatuweka huru kutoka katika utumwa wa maovu.

1. Yoh. 8:34-36

2. Luka 11:20-22

1

3. Kol. 2:15

4. Yak. 4:7

IV. Wokovu unamaanisha kwamba tumeunganishwa na “Watu wa Mungu” ambao wanarithi Ufalme aliowaahidia.

Kwa maelezo zaidi kuhusu jambo hili muhimu tazama kiambatisho chenye kichwa “Wokovu kama Kujiunga na Watu wa Mungu.”

A. Kwa sababu Kristo ni Mwana wa Mungu, umoja wetu naye unatuunganisha na familia ya Mungu.

1. Efe. 1:5.

2. Ebr. 2:11-13

3. Gal. 4:6

B. Baadhi ya vitu ambavyo Mungu amewaahidia watu wake ni Pamoja na:

1. Ufalme usioweza kutikiswa.

/ 3 1

THEOLOJIA YA KANISA

a. Luka 12:32

b. Ebr. 12:27

2. Mbingu mpya na nchi mpya isiyo na uovu wala maumivu.

a. 2 Pet. 3:13

1

b. Ufu. 21:1-5

3. Mwili mpya usioharibika na utakaoishi milele.

a. Luka 18:29-30

b. 1 Kor. 15:50-57

4. Haki ya kukaa katika uwepo wa Mungu katika Yerusalemu Mpya.

a. Ufu. 21:2-3

b. Ufu. 22:3-4

5. Haki ya kutawala pamoja na Mungu katika utawala mpya.

a. 2 Tim. 2:12

3 2 /

THEOLOJIA YA KANISA

b. Ufu. 22:5

6. Ujira wa uaminifu katika maisha haya ya sasa.

a. 2 Tim. 4:8

b. Yak. 1:12

1

c. Ufu. 2:10

7. Miujiza mipya isiyoweza kufikirika ambayo inazidi maelezo au uelewa.

a. 1 Kor. 2:9

b. 1 Yoh. 3:2

Kuokolewa katika maana ya kibiblia ni kushiriki katika uzoefu huu kama sehemu ya watu wa Mungu waliochaguliwa kupokea hayo. Mbingu mpya na nchi mpya hazitakaliwa na watu wa taifa fulani, bali na jamii mpya ambayo Mungu ameiita kutoka duniani. Mtu yeyote ambaye hachukui nafasi yake miongoni mwa watu wa Mungu wanaporithi baraka hizi anahesabiwa kuwa “amepotea.”

C. Paulo na Petro wote wanauelezea wokovu kama tendo la kuwa sehemu ya “watu wa Mungu.”

1. 1 Pet. 2:10

2. Efe. 1:18-23

/ 3 3

THEOLOJIA YA KANISA

Hivyo, Mungu siyo tu anawaokoa watu binafsi na kuwaandaa kwa ajili ya kwenda mbinguni; bali anaunda watu kwa ajili ya Jina lake, ambao Mungu anaweza kukaa kati yao na ambao katika maisha yao pamoja wataakisi maisha na tabia ya Mungu. Mtazamo huu wa wokovu ni wa kina kwa Paulo. ~ Gordon D. Fee. God’s Empowering Presence . Peabody: Hendrickson, 1994. uk. 872.

D. Maandiko ya Agano la Kale yalijenga msingi wa kuelewa kwamba wokovu ni kuunganishwa na watu wa Mungu.

1

1. Wokovu kutoka Misri (Kutoka):

Labda picha bora kabisa ya wokovu katika Biblia ni hadithi ya Kutoka ambapo wana wa Israeli wanakombolewa kutoka utumwani nchini Misri. Tangu enzi za awali katika historia ya Kanisa, hadithi ya Kutoka ilieleweka kama hadithi inayofafanua ufahamu wa Kikristo wa wokovu. Angalia jinsi hadithi ya Kutoka

a. Watu watumwa wanaoishi katika mateso bila matumaini (Waisraeli katika Misri),

b. Wanaitwa na Mungu kwa uchaguzi wake wa neema kupitia shujaa ambaye Mungu anamtuma (Musa),

c. Wanaokolewa na ghadhabu ya Mungu kwa njia ya damu (Mwana kondoo wa Pasaka),

inavyotoa taswira ya maana halisi ya kuokolewa.

d. Wanaokolewa kutoka kwa mfalme mwovu kupitia nguvu kuu za Mungu (ushindi dhidi ya Farao na majeshi yake),

e. Wanakombolewa kwa kupita katika maji (Bahari ya Shamu),

f. Wanaundwa kuwa taifa takatifu (Israeli) wanaotii mapenzi ya Mungu (Torati),

g. Wanapewa jukumu la kuwa mashahidi kwa mataifa (Kutoka 19:5-6),

3 4 /

THEOLOJIA YA KANISA

h. Na mwishowe, wanaletwa katika nchi ya ahadi (Kanaani) yenye mji mkuu wenye utukufu (Yerusalemu), ambamo wanaishi kwa amani chini ya Mfalme mkuu (Daudi).

2. Wokovu kutoka dhambini:

a. Watu watumwa wanaoishi katika mateso bila matumaini (kila mwanadamu chini ya dhambi),

1

b. Wanaitwa na Mungu kwa uchaguzi wake wa neema kupitia Shujaa ambaye Mungu anatuma (Yesu),

c. Wanaokolewa na ghadhabu ya Mungu kwa njia ya damu (Yesu, Mwana-kondoo wa Mungu aliyechinjwa),

d. Wanaokolewa kutoka kwa mfalme mwovu kupitia nguvu kuu za Mungu (ushindi dhidi ya Shetani na majeshi yake ya mapepo),

e. Wanakombolewa kwa kupita katika maji (ubatizo),

f. Wanaundwa kuwa taifa takatifu (Kanisa) wanaotii mapenzi ya Mungu (amri za Kristo),

g. Wanapewa jukumu la kuwa mashahidi kwa mataifa (Mathayo 28:18-20),

h. Na mwishowe, wanaletwa katika nchi ya ahadi (uumbaji mpya) yenye mji mkuu wenye utukufu (Yerusalemu Mpya), ambamo wanaishi kwa amani chini ya Mfalme mkuu (Yesu).

/ 3 5

THEOLOJIA YA KANISA

3. Kuokolewa katika tendo la “Kutoka” kulimaanisha nini?

4. Kuokolewa kulimaanisha nini katika Agano Jipya?

a. Rum. 8:20-25

b. 2 Pet. 3:13

1

Hitimisho

» Kuokolewa kunamaanisha kuondolewa kutoka katika hali ya upotevu na kutengwa na Mungu kunakosababishwa na dhambi kwa kuunganishwa na Kristo na hivyo kujiunga na “watu wa Mungu” wanaorithi Ufalme aliouahidi. » Wokovu huu daima unahusisha tendo la mtu katika maisha yake kuokolewa kutoka katika hukumu ya Mungu juu ya dhambi na kupata uhuru kutoka katika utumwa wa dhambi. » Wokovu na Kanisa ni kama pande mbili za sarafu moja, kwa sababu kuokolewa, kwa maana yake halisi, kunamaanisha kuwa sehemu ya watu wa Mungu. Watu hupata wokovu mmoja mmoja, lakini hakuna anayeokolewa ili kuishi maisha ya wokovu peke yake. Kuunganishwa na Kristo daima kunahusisha kuunganishwa na watu wake. » Kanisa ni sehemu ya hadithi kubwa ya Mungu ambayo itapelekea mbingu mpya na nchi mpya pamoja na jamii mpya ya wanadamu chini ya utawala wa Mungu, hali ambayo itabatilisha kabisa athari za dhambi na mauti ulimwenguni. » Kuita watu kuokolewa ni kuwaalika washiriki katika ulimwengu huo mpya kwa imani katika Yesu atakayekuwa mtawala wake.

Made with FlippingBook flipbook maker