Theology of the Church, Swahili Student Workbook

1 0 0 /

THEOLOJIA YA KANISA

2. Ibada ya ubatizo inapata umuhimu wake kutokana na uhusiano wake wa toba na imani ya mwamini katika Bwana Yesu.

a. Ubatizo ni ishara ya nje na uthibitisho wa maungamo wa ndani ya mwamini wa imani katika Yesu Kristo kama Mwokozi na Bwana. Kwa njia ya imani na ubatizo, mwamini sasa anakuwa mali ya Yesu kama Bwana wa wote.

b. Paulo anatumia lugha ya “umiliki” kuzungumzia uhusiano mpya na Kristo kwa njia ya imani na ubatizo. (1) 1 Kor. 1:12 (2) Gal. 3:27 (3) Rej. 1 Kor. 3:23

3

c. Ubatizo unaonekana kwamba siku zote ulikuja kufuatia ungamo la imani katika huduma ya mitume (Mdo 8:12).

d. Paulo anaweka wazi kwamba japokuwa aliwabatiza wachache huko Korintho, Mungu hakumwita kubatiza bali kuhubiri habari njema za Yesu Kristo. Ubatizo sio sababu bali ni matokeo ya imani inayookoa katika Yesu Kristo.

(1) 1 Kor. 1:13-17 (2) Mdo 16:14-15

3. Imani ya kweli inapaswa kuambatanishwa na kubatizwa katika maji kama ishara ya utii na utambulisho wa mtu pamoja na Kristo na watu wake.

4. Athari kubwa ya ubatizo ni jinsi unavyomuunganisha mwamini mpya pamoja na Yesu Kristo katika kifo chake, kuzikwa, kufufuka, na maisha mapya.

Made with FlippingBook flipbook maker