Theology of the Church, Swahili Student Workbook
/ 1 0 3
THEOLOJIA YA KANISA
2. Umuhimu wa kuhubiri na kufundisha Neno la Mungu kwa bidii na uwazi katika Kanisa unaweza kuonekana kwa sababu kadhaa.
a. Kwanza, Neno la Mungu linaweza kulisha na kukuza ukuaji wa kiroho wa mwili (2 Tim. 2:15).
b. Kadhalika, Neno linawatayarisha watu wa Mungu Kanisani kwa kila kazi njema ambayo Roho Mtakatifu anawaita kufanya (2 Tim. 3:15-17).
c. Hatimaye, Neno linawawezesha washirika kushiriki katika vita vya kiroho na kumshinda adui kama Upanga wa Roho (Efe. 6:16-17).
B. Jambo lingine, tunapofundisha Neno la Mungu, tunasaidia washirika binafsi wa makusanyiko yetu kutambua karama na wito wao kama washirika wa kusanyiko la watu wa Mungu waliopewa vipawa na karama na Mungu Mwenyewe.
3
1. Waamini wote wamepewa karama za Roho Mtakatifu ili zitumike kwa niaba ya Kanisa, kwa kufaidiana (1 Kor. 12:4-7).
2. Mungu ametoa wanaume na wanawake wenye vipawa maalum kwa Kanisa ili kuwakamilisha waamini kwa ajili ya kazi ya huduma (Efe. 4:11-13).
3. Kila mshirikia huchangia sehemu yake kwa ajili ya ukuaji wa jumla wa mwili na huduma, kwa utukufu wa Mungu (Efe. 4:15-16).
4. Tunapowafundisha Wakristo wapya kufanya yote ambayo Yesu ametoa na kuamuru, Wakristo wapya watatambua karama zao, watajifunza kuzitumia kwa manufaa na kuwajenga washirika wenzao ndani ya Kanisa (Rum. 12:4-8).
Made with FlippingBook flipbook maker