Theology of the Church, Swahili Student Workbook
/ 1 0 9
THEOLOJIA YA KANISA
* Je, yeyote anayetaka kuokolewa anaweza kuja kwa Kristo, au ni wateule pekee? * Je, waamini wote wameamriwa kwenda kufanya wanafunzi, au je, huu ni wito maalum kwa kundi fulani la waamini katika Kanisa? Tunajuaje kama tumeitwa kwenda, kubatiza, na kufundisha? * Kuna uhusiano gani kati ya uinjilishaji wa ulimwengu na kuwa Mkristo? Je, nifanye nini kuhusu watu waliopotea nje ya nchi, ikiwa ninaishi mjini na sina njia ya kuwafikia? * Roho Mtakatifu ana nafasi gani katika kuwashirikisha Habari Njema wengine? Je, ujumbe wa Agizo Kuu unahusiana vipi na maandiko mengine ambapo Yesu anaamuru mitume wake waende na kuwa mashahidi wake? * Ni nini humfanya mtu kuwa shahidi halali? Je, unaweza kuwa shahidi wa Mungu ingawa hujaenda chuo cha Biblia au seminari? Ni nani anayestahili kwenda, kubatiza, na kufundisha kwa ajili ya Mungu? Katika kujadili fundisho la uchaguzi na wanafunzi wengine, mmoja alitokea kutaja kwamba anaamini kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya wateule tu; wale ambao hawajachaguliwa kwa ajili ya wokovu hawakujumuishwa katika mpango wa Mungu wa wokovu. Alidai kwamba ikiwa Mungu anataka uokoke, utaokolewa. Ni wazi kwamba si kila mtu ataokolewa, kwa hiyo Mungu hakusudii kuokoa kila mtu, bali ni baadhi tu. Kwa hiyo, Kristo alikufa kwa ajili ya wale ambao Mungu anataka kuwaokoa. Je, unaichukuliaje hoja hii? Ni hoja inayoshawishi? Ikiwa jibu ni ndiyo, eleza kwa nini, na ikiwa jibu ni siyo, fafanua kwa nini. Baada ya kusoma kitabu kuhusu theolojia ya Matengenezo (Reformed), mwanafunzi mmoja ametatizika hasa kuhusu wazo alilokutana nalo katika kitabu hicho. Kwa lugha rahisi wazo lake ni hili: ukweli kwamba Mungu huwachagua wengine kuokolewa ina maana pia kwamba Mungu amewachagua wengine kwenda jehanamu. Kitabu hicho kilionekana kudai kwamba kuna baadhi ya watu ambao hawataweza na hawangeweza kumjia Kristo kwa sababu hawakuchaguliwa kuokolewa; Mungu hakuwazingatia, na kwa hivyo watakufa, bila Kristo na bila tumaini. Wazo hili limemsumbua mwanafunzi huyu, japo linaonekana kuwa na mantiki. Je, kuchagua baadhi na kutochagua wengine haimaanishi kwamba Ni Wateule Pekee Watakaomjia Yesu Mungu Amekuchagua kwa ajili ya Kuhukumiwa
3
MIFANO
1
4
Made with FlippingBook flipbook maker