Theology of the Church, Swahili Student Workbook

/ 1 1 9

THEOLOJIA YA KANISA

MIFANO YA REJEA

Sio Ibada Halisi ya Kanisa

Katika kusanyiko la hivi majuzi la kikundi seli cha kanisa jipya lililopo katika mtaa wa jiji fulani, mjadala ulitokea na hoja ikiwa kama kukutana nyumbani tu kunatosha kuwa kanisa la kweli. Baadhi ya washiriki waliokuwa wakienda kwenye ibada za kawaida za kanisa wamejisikia vibaya kidogo kukutana majumbani na kuita mikutano hiyo na waamini “ibada ya kanisa.” Mjadala huu umekua na kuwa mjadala mkubwa zaidi kuhusu kile kinachofanya ibada ya kanisa kuwa halali. Kama ungekuwa sehemu ya mjadala huu, ungesema nini kuhusu sifa na vigezo vya kweli vya “ibada halisi ya kanisa”?

1

Injili Kamili, Kamili Zaidi, na Kamili Kuliko Zote

Katika migawanyiko yote na madhehebu mbalimbali ambayo yanazungumza juu ya sifa za ushirika wa “injili kamili”, kuna vigezo vingi vinavyotumiwa kufafanua maana ya kanisa halali. Kulingana na ufahamu wako ulivyo sasa, kama ungetaja tu sifa tano za kanisa la kweli, zingekuwa zipi? Fikiria kwa muda. Kwa nini umechagua sifa hizo tano? Je, kuna chochote ambacho kinaweza kuwa kimesahaulika kwenye orodha yako?

2

4

Sisi Pekee ndilo Shirika la Yehova

Baada ya mazungumzo magumu pamoja na Mashahidi wa Yehova asubuhi moja, dada mmoja Mkristo mpendwa ametatizika kuhusu mazungumzo hayo. Mashahidi wa Yehova walidai mambo mawili ambayo yalikaa akilini mwake. Kwanza, walidai kwamba Mungu anaweza kuwa na Kanisa moja tu halali na la kweli—mashirika haya yote yanayodai kuwa ya Mungu hayawezi yote kuwa sahihi. Pili, walidai kwamba kwa sababu ya mgawanyiko na mkanganyiko mkubwa katika mafundisho na mapokeo ya makanisa (ya Katoliki, Kiprotestanti, Kianglikana, na Othodoksi), hawawezi kuwa wa kweli. Misimamo pekee yenye maana ni misimamo safi na inayoeleweka ya Mashahidi wa Yehova, pamoja na mapokeo yao yasiyo ya ubaguzi wa rangi na yasiyo ya kitaasisi. Je, ungemjibuje huyu dada mpendwa anapojaribu kuelewa tofauti zote kati ya mapokeo mbalimbali yanayodai kumwakilisha Mungu na kuwa ni ya Kikristo?

3

Made with FlippingBook flipbook maker