Theology of the Church, Swahili Student Workbook
1 3 6 /
THEOLOJIA YA KANISA
a. Tunafanya kazi mbali mbali dhidi ya magonjwa ya kimwili, utapiamlo, na ukosefu wa huduma ya kutosha kwa wanadamu walioumbwa kwa mfano wa Mungu.
b. Zaidi ya hayo, sisi kama waamini tunasimama dhidi ya mateso ya wanadamu na visababishi vingi vya mateso hayo, bila kujali ni wapi tunapokutana na watu wanaokandamizwa.
3. Kama watu tulioitwa kuleta uzima kwa waliovunjika, tunahakikishiwa kwamba Mungu mwenyewe atatambua kazi zetu, Zab. 41:1-2.
C. Hatimaye, tukiwa mabalozi wa Yesu Kristo, tunafanya kazi kudhihirisha utawala wa haki wa Ufalme.
1. Mungu huwaelekeza watu wake kuhusu ibada ya kweli na dhabihu ya kweli, Isa. 1:16-18.
4
2. Kama mabalozi wa Yesu, tunafanya kazi kwa bidii kupinga udhalimu na ukosefu wa haki katika ngazi yoyote ile, popote tunapogundua matendo hayo miongoni mwa watu.
3. Hali za maisha katika miji ya Amerika na kote ulimwenguni leo zinadhihirisha ukosefu wa haki, Mhubiri 4:1.
a. Tukiwa mabalozi wa utawala wa haki wa Yesu, tunapaswa kupiga kelele dhidi ya aina zote za uonevu wa kisiasa, kijamii, kidini, na kibinafsi.
b. Tunasimama kwa ajili ya wale ambao hawawezi kujitetea wenyewe, na kuwatetea wale ambao hawana sauti yoyote ya kuwakilisha haki zao kama binadamu, Mit. 31:8-9.
Made with FlippingBook flipbook maker