Theology of the Church, Swahili Student Workbook

/ 1 3 9

THEOLOJIA YA KANISA

d. Kanisa linahusu kazi za kutangaza. Kupitia juhudi zetu za uinjilisti, mafundisho, uchapishaji, upandaji makanisa, na huduma tunashuhudia kwamba utawala wa Mungu na mamlaka yake umekuja katika Yesu, na kwamba Mungu anawaagiza watu wote watubu na kupokea neema yake katika Kristo (Mdo. 17:30-31).

B. Kisha, kama askari wa Mwana-Kondoo, tunafanya kazi kuharibu kazi ya shetani.

1. Kwa mara nyingine tena, ningesema kwamba ushuhuda wa jumla wa Agano Jipya unaonyesha kweli hii kuu kwamba Kanisa katika enzi hii ya sasa ni Kanisa la Kivita, linalofanya vita na maadui wa Mungu ili kudhoofisha na kuharibu kazi ya shetani.

a. Efe. 6:12-13

b. 1 Yoh. 3:8

4

c. 1 Yoh. 4:6

d. Yoh. 14:12

Je, tunawezaje kudhoofisha na kuharibu kazi ya Shetani duniani?

2. Tunaharibu kazi yake kwa kuwahubiria waliopotea Habari Njema kwa ujasiri.

a. Kulingana na Warumi 1:16-17, Injili ndiyo dunamis au uweza wa Mungu wa kuwaokoa wale wote wanaoamini, naam, hata kuvunja nguvu za udanganyifu wa shetani juu ya maisha yao.

Made with FlippingBook flipbook maker