Theology of the Church, Swahili Student Workbook
1 8 4 /
THEOLOJIA YA KANISA
Theolojia ya Kanisa (muendelezo)
1. Kanisa linaweka imani yake:
a. katika Neno Hai (Yesu Masihi), b. ambaye amefunuliwa katika Neno lililoandikwa (Maandiko Matakatifu), c. na ambaye sasa yuko, akifundisha na kuweka katika vitendo Neno lake kwa Kanisa (kupitia huduma ya Roho Mtakatifu). 2. Kanisa linalinda amana ya imani, iliyotolewa na Kristo na mitume, kwa njia ya mafundisho yenye uzima na msaada wa Roho Mtakatifu anayekaa ndani ya washirika wake (2 Tim. 1:13-14). B. Kwa sababu ni jamii ya imani, Kanisa pia ni jamii ya neema. 1. Kanisa lipo kwa neema – kwa njia ya imani na si kwa wema au matendo ya kibinadamu (Gal. 2:21; Efe. 2:8). 2. Kanisa linatangaza, kwa imani, neema ya Mungu kwa wanadamu wote (Tito 2:11-15). 3. Kanisa linaishi kwa neema katika matendo na mahusiano yake yote (Efe. 4:1-7). C. Kanisa ni jamii ambamo Maandiko yanahubiriwa, yanafundishwa, yanatafakariwa na kukaririwa, kuaminiwa, na kutiiwa (Eze. 7:10; Yos. 1:8; Zab. 119; Kol. 3:16; 1 Tim. 4:13; Yak. 1:22-25; ) 1. Kanisa linahubiri Injili ya Ufalme, kama ilivyofunuliwa katika Maandiko, na kuwaita watu kwenye toba na imani inayoongoza kwenye utii (Mt. 4:17; 28:19-20; Mdo. 2:38-40). 2. Kanisa linajifunza na kutumia Maandiko kwa njia ya kufundisha, kukemea, kusahihisha na kuadibisha katika haki ili kwamba waamini wote wawe tayari kuishi maisha ya kimungu yanayodhihirishwa kupitia matendo mema (2 Tim. 3:16-17; 4.2). 3. Kanisa, kwa makusudi, hutafakari Maandiko katika mwanga wa ufahamu, mapokeo, na uzoefu, likijifunza na kufanya theolojia kama
Made with FlippingBook flipbook maker