Theology of the Church, Swahili Student Workbook

1 8 6 /

THEOLOJIA YA KANISA

Theolojia ya Kanisa (muendelezo)

B. Kanisa linashuhudia kwa: 1. Kufanya kazi kama ishara na kionjo cha Ufalme wa Mungu; Kanisa ni jamii inayoonekana ambamo watu wanaishi kwa kusudi la kuona kwamba: a. Yesu anatambuliwa kama Bwana (Rum. 10:9-10). b. Kweli na nguvu ya Injili inakua na kuzaa matunda katikati ya kila jamaa, kabila na taifa (Mdo. 2:47; Rum. 1:16; Kol. 1:6; Ufu. 7:9 10). c. Maadili ya Ufalme wa Mungu yanakubaliwa na kutekelezwa (Mt. 6:33). d. Amri za Mungu zinapewa utii duniani kama ilivyo mbinguni (Mt. 6:10; Yoh. 14:23-24). e. Uwepo wa Mungu unadhihirika na watu wanauishi (Mt. 18:20; Yoh. 14:16-21). f. Nguvu za Mungu zinadhihirishwa (1Kor. 4:20). g. Upendo wa Mungu unapokelewa na kutolewa bure (Efe. 5:1-2; 1 Yoh. 3:18; 4:7-8). h. Huruma ya Mungu inaonyeshwa katika kubebeana mizigo, kwanza ndani ya Kanisa, na kisha, katika huduma ya kujidhabihu kwa ulimwengu wote (Mt. 5:44-45; Gal. 6:2, 10; Ebr. 13:16). i. Ukombozi wa Mungu unapita udhaifu na dhambi ya mwanadamu ili kwamba hazina ya Ufalme iwe dhahiri licha ya kuwa ndani ya vyombo vya udongo (2 Kor. 4:7). 2. Kufanya ishara na maajabu yanayothibitisha Injili (Mk. 16:20; Mdo. 4:30; 8:6,13; 14:3; 15:12; Rum. 15:18-19; Ebr. 2:4). 3. Kukubali wito wa utume a. Kwenda ulimwenguni kote kuhubiri Injili (Mt. 24:14; 28:18-20; Mdo. 1:8, Kol. 1:6). b. Kueneza Injili na kufanya wanafunzi wa Kristo na Ufalme wake (Mt. 28:18-20; 2 Tim. 2:2).

Made with FlippingBook flipbook maker