Theology of the Church, Swahili Student Workbook
/ 1 9 3
THEOLOJIA YA KANISA
Theolojia ya Kanisa (muendelezo)
B. Kanisa ni makao ya Mungu (Efe. 2:19-21): 1. Taifa lake 2. Watu wa nyumbani mwake 3. Hekalu lake.
C. Kanisa hukusanyika likitazamia kwa shauku uwepo wa Mungu (Efe. 2:22). 1. Kanisa sasa linakuja katika uwepo wa Mungu katika kila kusanyiko: a. Kama watu wa agano katika Agano la Kale, Kanisa hukusanyika katika uwepo wa Mungu (Kut. 18:12; 34:34; Kum. 14:23; 15:20; Zab. 132:7; Ebr. 12:18-24). b. Kanisa lililokusanyika linadhihirisha uhalisia wa Ufalme wa Mungu kwa kuwa mbele ya Mfalme (1Kor. 14:25). 2. Kanisa linatazamia kusanyiko la wakati ujao la watu wa Mungu wakati utimilifu wa uwepo wa Mungu utakapokuwa pamoja nao wote (Eze. 48:35; 2 Kor. 4:14; 1 The.3:13; Ufu. 21:13). D. Kanisa linategemea kwa kila namna uwepo wa Roho wa Kristo. 1. Bila uwepo wa Roho Mtakatifu hakuna Kanisa (Mdo. 2:38; Rum. 8:9; 1 Kor. 12:13; Gal. 3:3; Efe. 2:22; 4:4; Flp. 3:3). 2. Roho Mtakatifu huumba, huongoza, hutia nguvu, na kufundisha makusanyiko ya waamini (Yoh. 14:16-17, 26; Mdo. 1:8; 2:17; 13:1; Rum. 15:13, 19; 2 Kor. 3:18). 3. Roho Mtakatifu hutoa karama kwa Kanisa ili liweze kutimiza utume wake, likileta heshima na utukufu kwa Mungu (Rum. 12:4-8; 1Kor. 12:1-31; Ebr. 2:4). 4. Roho Mtakatifu analifungamanisha Kanisa pamoja kama familia ya Mungu na mwili wa Kristo (2 Kor. 13:14; Efe. 4:3).
Made with FlippingBook flipbook maker