Theology of the Church, Swahili Student Workbook

1 9 8 /

THEOLOJIA YA KANISA

Theolojia ya Kanisa (muendelezo)

2. Matendo haya mema ni kiini cha kusudi jipya na utambulisho mpya ambao tunapewa wakati wa kuzaliwa upya. “Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.” (Efe. 2:10). 3. Kazi hizi za huduma hufunua tabia ya Mungu kwa ulimwengu na kuwaongoza watu kumpa sifa (Mt. 5:16; 2 Kor. 9:13). B. Utumishi ndio mbinu ya Mkristo katika kujenga mahusiano, rasilimali, na huduma. 1. Jamii ya Kanisa hutumika kwa kufuata kielelezo cha Kristo ambaye alikuja “si kutumikiwa bali kutumika” (Mt. 20:25-28; Lk. 22:27; Flp. 2:7). 2. Jamii ya Kanisa hutumika kulingana na amri ya Kristo na mitume (Mk. 10:42-45; Gal. 5:13; 1 Pet. 4:10). 3. Jamii ya Kanisa hutumikia, kwanza kabisa, “mdogo zaidi kati ya hawa” kulingana na maagizo ya mafundisho ya Kristo (Mt. 18:2-5; Mt. 25:34-46; Lk. 4:18-19). C. Utoaji na ukarimu ni ishara pacha za utumishi wa Ufalme. 1. Utoaji husababisha mtu kujitoa nafsi yake na mema yake kwa ajili ya kumtangaza na kumtii Kristo na utawala wa Ufalme wake. 2. Ukarimu husababisha kumtendea mgeni, mfungwa, na adui kama mmoja wa watu wako mwenyewe (Ebr. 13:2). 3. Ishara hizi ni tunda la kweli la toba (Luka 3:7-14; Lk 19:8-10; Yak. 1:27). D. Uwakili ni ukweli wa msingi ambao unatawala jinsi Kanisa linavyotumia rasilimali ili kufanya “Kazi za Huduma.” 1. Rasilimali zetu (muda, fedha, mamlaka, afya, cheo, n.k.) si mali yetu bali ni ya Mungu.

Made with FlippingBook flipbook maker