Theology of the Church, Swahili Student Workbook

/ 4 9

THEOLOJIA YA KANISA

• Kutofautisha kati ya neema na rehema. • Kutambua na kuukabili uzushi wa Pelagiani. • Kueleza tofauti kati ya neno “sakramenti” na neno “agizo.” • Kutaja na kueleza kwa ufupi mitazamo mikuu minne ya Kikristo kuhusu Meza ya Bwana.

I. Sola Gratia (Neema Pekee)

Muhtasari wa Video ya Sehemu ya 1

A. Neema ni sifa muhimu ya jinsi Mungu alivyo.

Uf. 22:21 Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi nyote. Amina.

2

1. Kut. 34:6-7

2. Yn. 1:14

3. Efe. 1:6

4. Ebr. 10:29

B. Neema ni kibali tusichostahili. Mungu anapokuwa wa neema kwetu hututendea kwa upendo ingawa hatuna sababu ya kudai au kutarajia fadhili hizo.

C. Tofauti kati ya “neema” na “rehema.”

1. Rehema ni Mungu kutunyima na kukizuia kile tunachostahili.

2. Neema ni Mungu kutupa kile tusichostahili.

Made with FlippingBook flipbook maker