Theology of the Church, Swahili Student Workbook

/ 5

THEOLOJIA YA KANISA

Utangulizi wa Moduli

Salamu, marafiki wapendwa, katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Kanisa la Mwenyezi Mungu katika Yesu Kristo ni mojawapo ya mada zenye kuburudisha na muhimu zaidi katika Maandiko yote. Yesu wa Nazareti, kupitia kifo chake, kuzikwa, na ufufuo wake, ameinuliwa kuwa kichwa juu ya watu wake wapya, wale walioitwa kumwakilisha duniani na kutoa ushahidi wa Ufalme wake ambao tayari upo japo haujakamilika bado. Kuelewa jukumu la Kanisa katika mpango wa ufalme wa Mungu ni muhimu kwa kila eneo la maisha ya ufuasi wa kibinafsi na wa kusanyiko; hakuna ufuasi au wokovu mbali na tendo la Mungu la kuokoa kupitia Kanisa. Kufahamu kile ambacho Mungu anafanya ndani ya na kupitia watu wake kunampa kiongozi wa watu wa Mungu uwezo wa kumwakilisha kwa hekima na heshima. Tunakualika kwa shauku kujifunza kuhusu Kanisa ili kufahamu kikamilifu asili ya huduma ulimwenguni leo. Somo la kwanza, Ufunuo Kivuli wa Kanisa katika Mpango wa Mungu , linaangazia jinsi Kanisa lilivyofunuliwa tangu awali katika kusudi kuu la Mungu la kujiletea utukufu kwa kuokoa jamii mpya ya wanadamu kupitia agano lake na Ibrahimu. Utaona jinsi Kanisa linavyofunuliwa kwa namna ya kivuli katika kufunuliwa kwa mpango wake wa neema ya wokovu ili kuwajumuisha Mataifa katika kazi yake kwa njia ya Kristo Yesu, na utajifunza pia kuhusu nia ya Mungu ya kujitengenezea watu wa kipekee, laos wa Mungu. Pia utagundua utajiri wa wokovu na maana ya wokovu, nini maana ya kuokolewa kutoka katika upotevu na kutengwa na Mungu kunakosababishwa na dhambi. Kupitia muungano wetu na Kristo tunaunganishwa na “watu wa Mungu” wanaorithi Ufalme aliouahidi. Kuunganishwa na Kristo ni kuunganishwa na watu wake, wale ambao tumaini lao liko katika ahadi ya Mungu kuumba mbingu mpya na nchi mpya, yenye jamii mpya ya wanadamu chini ya utawala wa Mungu ambao utaondoa kabisa madhara ya dhambi na kifo duniani. Katika somo letu la pili, Kanisa katika Ibada , tutazingatia wokovu kama msingi wa ibada ya Kanisa. Tutaona kwamba wokovu unapatikana kwa neema ya Mungu pekee na kwamba wanadamu hawawezi kuupata kwa juhudi zao au kuustahili. Hivyo, kuabudu ni mwitikio sahihi kwa neema ya Mungu. Pia tutaanganzia baadhi ya mawazo yanayotokana na tafakari ya Kikristo kuhusu ibada ya Kanisa, ikijumuisha uchambuzi mfupi wa maneno “sakramenti” na “maagizo” pamoja na maoni tofauti kuhusu Ubatizo na Meza ya Bwana katika muktadha wa ibada ya Kanisa. Zaidi ya hayo, tutagundua madhumuni ya kitheolojia ya ibada ya Kanisa, ambayo ni kumtukuza Mungu kwa sababu ya utakatifu wake wa pekee, uzuri wake usio na kikomo, utukufu wake usio na kifani na kazi zake zisizoweza

Made with FlippingBook flipbook maker