Theology of the Church, Swahili Student Workbook

5 2 /

THEOLOJIA YA KANISA

B. Maana ya “sakramenti”

1. Sakramenti kwa kawaida hufafanuliwa kama “ishara ya nje na inayoonekana ya neema ya ndani na ya kiroho.” Wale wanaotumia neno sakramenti huona ubatizo na Meza ya Bwana kama njia ambayo kwayo neema ya Mungu hutujilia.

2. Ingawa Wakatoliki na Waothodoksi wana sakramenti nyingi, Waprotestanti kwa kawaida wamehifadhi neno sakramenti kwa ajili ya ubatizo na Meza ya Bwana pekee. Sakramenti hizi mbili zina nafasi ya pekee katika historia ya Kanisa kama “njia muhimu ya neema” kwa sababu zilianzishwa moja kwa moja kwa amri ya Yesu. Wale wanaofafanua Meza ya Bwana na ubatizo kama sakramenti wanasema kwamba vinapopokelewa kwa imani, Mungu kwa neema anafanya kazi ndani yetu ili kutimiza ahadi zake.

2

C. Maana ya “maagizo”

1. Kuna mapokeo mengi ya kanisa yanayoielewa Meza ya Bwana na ubatizo kama maagizo, badala ya sakramenti. Neno “agizo” linamaanisha “amri iliyoidhinishwa” na kwa hiyo Meza ya Bwana na ubatizo hufanywa kwa kutii amri ya Kristo. Badala ya kuwa njia ambayo neema ya Mungu hutujia, makanisa haya yanamsimamo kwamba katika ubatizo na Meza ya Bwana tunakumbuka na kuishuhudia neema ya Mungu ambayo tayari tumepokea.

2. Kut. 12:14 (BHN) – Vizazi hata vizazi mtaadhimisha tukio hilo kwa sikukuu kubwa kwa heshima yangu mimi Mwenyezi - Mungu. Hilo litakuwa agizo la milele kwenu.”

3. Lengo la maagizo mengi ya Agano la Kale lilikuwa kuwasaidia watu kukumbuka kutii kwa njia ya amri au sherehe ya kidini. Katika Agano Jipya, ubatizo na Meza ya Bwana ni ushuhuda wa wazi wa neema

Made with FlippingBook flipbook maker