Theology of the Church, Swahili Student Workbook
/ 5 9
THEOLOJIA YA KANISA
Yesu yuko katika sakramenti hii ila si kimwili bali kiroho. . . . Watu wake wanampokea sio kwa mdomo bali kwa imani; hawapokei mwili na damu yake kama vitu vya kimwili, bali mwili wake uliovunjwa na damu yake iliyomwaga. Kwa jinsi hiyo unganiko linaashiriwa . . . ni unganiko la kiroho na la ajabu kwa sababu ya kujiliwa na Roho Mtakatifu. Ubora wa sakramenti hii kama njia ya neema haupo katika ishara wala ibada, wala mhudumu, au neno, lakini upo katika matokeo ya kutembelewa na Roho Mtakatifu. ~ Charles Hodge. Systematic Theology . Abridged edition. Grand Rapids: Baker, 1992. uk. 496-498.
a. Kol. 3:1
2
b. Yn. 16:7
Ingawa mapokeo mengi ya Kipentekoste ni ya kiUkumbusho, mwanazuoni wa Kipentekoste Gordon Fee anatetea maoni sawa na ya Calvin anaposema: “Kwa kweli, mtu atakuwa hajakosea sana kuuona uwepo wa Roho Mtakatifu katika Meza ya Bwana kama namna ya Paulo ya kuuelewa uwepo halisi. Mfano wa Israeli kula ‘chakula cha Roho,’ na ‘kinywaji cha Roho’ katika 1 Wakorintho 10:3-4 walau unaliruhusu wazo hilo.”
~ Gordon Fee. Paul, the Spirit and the People of God. Peabody, MA: Hendrickson Publishers, 1996. uk. 154.
4. Mtazamo wa kiUkumbusho unaamini kwamba mkate na divai ni ishara tu ya mwili na damu ya Kristo na hutusaidia kukumbuka yale aliyotufanyia.
a. Tofauti na mitazamo mitatu ya kwanza ambayo huitazama meza ya Bwana kama sakramenti, Mtazamo wa kiUkumbusho huitazama meza ya Bwana kama agizo.
Made with FlippingBook flipbook maker