Theology of the Church, Swahili Student Workbook
7 0 /
THEOLOJIA YA KANISA
C. Kupitia mtindo wetu wa maisha wa utiifu, kama washirika wa jumuiya ya agano la Mungu:
1. Maisha yetu pamoja kama waamini yanaweza kuwa tendo la ibada, kama vile ushirika wetu pamoja katika Kristo, Ebr. 10:24-25.
2. Tunapotunzana kwa upendo kama familia, na kutafuta kufanya mapenzi yake, maisha yetu wenyewe sisi kama watu wake yanaweza kuwa tendo la ibada kwa Mungu.
a. Rum. 12:1
2
b. 1 Kor. 10:31
Hitimisho
» Kanisa huabudu ili kumtukuza Mungu kwa sababu ya utakatifu wake wa pekee, uzuri wake usio na kikomo, utukufu wake usio na kifani, na kazi zake zisizo na kifani. » Ibada ya Mungu inahusiana na nafsi za Utatu: tunamwabudu Yehova Mungu pekee, kupitia Yesu Kristo, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. » Kanisa humwabudu Mungu kwa njia ya sifa na shukrani, kwa njia ya liturujia, ambayo inasisitiza Neno na sakramenti, na kwa utiifu wetu na mtindo wa maisha kama jumuiya ya agano.
Maswali yafuatayo yaliundwa ili kukusaidia kupitia maudhui ya sehemu ya pili ya video. Unapofanya marejeo ya kweli kuu za sehemu hii, utahitaji kuhakikisha kwamba unashika na kuelewa mawazo ya msingi yanayohusiana na wito wa Kanisa wa kuabudu. Zingatia hasa kusudi la kumwabudu Mungu, na utafute miunganiko iliyopo kati ya madhumuni ya ibada na kazi ya ibada. Jibu kwa uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana, tumia Maandiko!
Sehemu ya 2
Maswali ya Mwanafunzi na Majibu
Made with FlippingBook flipbook maker