Theology of the Church, Swahili Student Workbook
/ 7 5
THEOLOJIA YA KANISA
Neema Pekee
Mchungaji anamshuhudia binti mmoja kuhusu Yesu na kumwalika kuhudhuria kanisani. Binti huyo anajibu, “Kwa sasa siko vizuri sana kufanya hivyo. Kiukweli ninavutiwa sana na dini na mambo mengine lakini ninataka kuweka maisha yangu sawa kwanza. Nikishaweka sawa baadhi ya vitu, basi nitakuja kanisani.” Mchungaji anapaswa kumwambia nini binti huyu?
3
Kushuka kwa ajili ya Bwana
Bendi mpya ya kusifu yenye maadhi ya jazi, fanki na roki inayojiita Selah imeibuka kanisani. Wameazimia kuipeleka sifa na kuabudu kwenye kiwango kipya kabisa cha nguvu katika kusanyiko, lakini wanafanya hivyo kwa aina ya sauti inayoendana na wimbo wa “ in your face ” wakiambatanisha na aina fulani ya onyesho ambalo lina wafuasi wengi hapo kanisani, kiasi kwamba hata baadhi ya watenda kazi wa kanisa, wanavutiwa nalo. Kundi hili la Selah linajipatia umaarufu mkubwa katika matamasha yao ya Jumamosi jioni, na limekuwa likitumiwa sana na Bwana katika baadhi ya huduma za uinjilisti hapo mjini. Hata hivyo, unapowasikiliza, wanaimba kama bendi za kidunia. Kiuhalisia, nyimbo zao nyingi hutumia mdundo wa nyimbo maarufu za muziki wa pop zilizowekewa tu maneno ya Kikristo. Baadhi ya watu wamekiri kwamba huwa wanaenda kwenye matamasha yao kwa ajili ya kucheza tu! Ungewashaurije Selah wanapojaribu kuonyesha kikamilifu upendo wao kwa Mungu katika ibada, kama mpiga ngoma wao ahamasishavyo “shuka kwa ajili ya Bwana”? Hakuna tunachoweza kufanya ili kutamani au kupata wokovu ikiwa haujatolewa kwetu kama zawadi ya bure kwa neema ya Mungu. Uzoefu huu wa neema ya Mungu hulifanya Kanisa kuwa jumuiya ambayo wajibu na furaha yao ni kumwabudu Mungu. Tunamtukuza Mungu katika ibada yetu kwa sababu ya tabia yake kamilifu – utakatifu wake wa pekee, uzuri wake usio na kikomo, utukufu na matendo yake yasiyo na kifani. Kwa neema ya Mungu katika Yesu Kristo, tumewekwa huru kumwabudu Mungu wa kweli, Mungu wa Utatu katika uweza wa Roho Mtakatifu. Zaidi ya hayo, Kanisa humwabudu Mungu kwa njia ya sifa na shukrani, kwa njia ya liturujia inayokazia Neno na sakramenti, na kwa utii na mfumo wake wa maisha kama jumuiya ya agano.
4
2
Marudio ya Tasnifu ya Somo
Made with FlippingBook flipbook maker