Theology of the Church, Swahili Student Workbook

/ 8 1

THEOLOJIA YA KANISA

Kanisa kama Shahidi

SOMO LA 3

Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma kwako, kujifunza, majadiliano, na matumizi ya maudhui ya somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kuelezea vipengele muhimu zaidi vya fundisho la “uchaguzi” (au uteuzi) jinsi linavyomhusu Yesu Kristo kama Mtumishi Mteule wa Mungu. • Kuelezea jinsi uchaguzi wa Mungu unavyohusiana na watu wake wateule Israeli pamoja na Kanisa. • Kuelezea uhusiano wa uchaguzi wa Mungu kwa waamini binafsi “katika Kristo,” yaani, kuhusiana na Kristo wanaposhikamana naye kwa imani. • Kuelezea jinsi Agizo Kuu linavyotoa muhtasari wa jumla wa ushuhuda wa Kanisa wenye sehemu tatu ulimwenguni ili kufanya wanafunzi. • Kufafanua jinsi Kanisa linavyotimiza agizo la Kristo kwa kutii wito wa Yesu wa kuwafikia waliopotea kwa Injili, kwa kuwabatiza waamini wapya katika Kristo (kuwajumuisha kama washirika katika Kanisa), na kwa kuwafundisha waongofu wa kweli kushika mambo yote ambayo Kristo aliamuru. Soma Marko 16:14-20. Kuna jambo la maana sana kuhusu maneno ya mwisho. Unamwambia nini mtu ambaye unamwona kwa mara ya mwisho? Hakika utachagua maelekezo yako kwa uangalifu mkubwa. Katika maneno ya mwisho ambayo Yesu aliwaambia wanafunzi wake kabla ya kupaa mbinguni, alikuwa wazi kabisa. Anawaambia, kipaumbele kikuu kwenu ni kuhubiri habari njema za Yesu kwa kila mtu ulimwenguni. Na kisha, akijua kwamba watakutana na nyakati za mateso na kutoamini, anaongeza kwamba wanapohubiri Injili wanapaswa kumtegemea Roho Mtakatifu (rej. Mdo. 1:8) ili kuwalinda na kuthibitisha mahubiri yao kwa madhihirisho ya wazi wazi ya nguvu za Mungu. Kanisa limechukua maneno hayo ya mwisho kwa uzito. Kila karne tangu Yesu kupaa Injili imepelekwa maeneo mapya ya ulimwengu—kwa makundi mapya ya watu, kwa lugha na tamaduni mpya—na imesababisha ukuaji thabiti na mara nyingi wa kuvutia wa Kanisa kiasi kwamba leo watu wengi zaidi wanamkiri Yesu kama Bwana kuliko wakati wowote katika historia ya wanadamu. Tunaweza kumshukuru Mungu kwa yale Hubiri Injili

Malengo ya Somo

3

Ibada

Made with FlippingBook flipbook maker