Theolojia Katika Picha
1 0 2 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kiini na Chimbuko: Ukristo Ni Yesu Kristo (muendelezo)
• Kwetu sisi tunaoamini, utukufu wa Mungu wenyewe unang’aa katika uso wa Yesu, 2 Kor. 4:6. • Utimilifu wa Uungu, uzuri wa utukufu wa Mungu unaonekana waziwazi zaidi katika utu na kazi ya Yesu Kristo (Kol. 2:9) - Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili. E. Ukristo ni Kristo, yaani kuwa na mahusiano na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo, ambaye tunaamini aliishi, akafa, na kufufuka ili kutuleta katika uhusiano sahihi na Mungu. • Sio maadili na kutenda mema (tunaishi vyema baada ya kukutana na Kristo) • Sio maisha ya familia tu (tunakuwa vile Mungu anataka tuwe baada ya kumjua Kristo) • Sio masomo ya kidini na liturujia (dini zingine zina maadili mema, programu nzuri za ibada, mafundisho ya kujitolea, na vitabu vingi vitakatifu).
Yesu Ndiye Njia Pekee ya Kumwendea Mungu
Msafiri alichukua mwongozo wa kumpeleka katika eneo la jangwa. Wale watu wawili walipofika kwenye ukingo wa jangwa, msafiri, alipotazama mbele, aliona mbele yake mchanga usio na alama za chochote kilichopita hapo, si nyayo za watu wala wanyama, njia au alama ya aina yoyote. Akamgeukia kiongozi wake, na kuuliza kwa sauti ya mshangao, “Njia iko wapi?” Kwa jicho la karipio, kiongozi alijibu, “Mimi ndimi barabara.”
Maandiko Yanaelekeza Kwa Kristo
Mara tano katika Agano Jipya Maandiko yanamtaja Yesu kuwa kusudi la kuandikwa kwa Maandiko Matakatifu. Yeye ndiye sababu ya hadithi, iliyogawanywa katika nusu mbili zisizolingana (Mwa. 1:1-3:15, na Mwa. 3:16 - Ufu. 21). Ukitazama sehemu yoyote ya Biblia, utamwona hapo. Kuna nakala ya shaba ya Azimio la Uhuru iliyochongwa moja kwa moja kwenye sleti ya shaba, iliyofanywa kwa usahihi wa kina na maelezo ya kupendeza. Ukirudi nyuma kidogo na kulitazama chapisho hilo la Azimio, hata hivyo, unaweza kuona taswira ya George Washington ikitokea kwenye maandishi. Ilifanyika
Made with FlippingBook Digital Publishing Software