Theolojia Katika Picha
/ 1 3 1
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kuhubiri na Kufundisha Yesu wa Nazareti kama Masihi na Bwana Ndio Moyo wa Huduma Yote ya Kibiblia Don L. Davis Wafilipi 3:8 - Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo [Masihi] Yesu , Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo [Masihi]. Matendo 5:42 - Na kila siku, ndani ya hekalu na nyumbani mwao, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema za Yesu kwamba ni Kristo [Masihi] . 1 Wakorintho 1:23 - bali sisi tunamhubiri Kristo [Masihi], aliyesulibiwa ; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi 2 Wakorintho 4:5 - Kwa maana hatujihubiri wenyewe, bali Kristo [Masihi] Yesu ya kuwa ni Bwana ; na sisi wenyewe kuwa tu watumishi wenu kwa ajili ya Yesu. 1 Wakorintho 2:2 - Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo [Masihi], naye amesulibiwa. Waefeso 3:8 - Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika [Masihi]. Wafilipi 1:18 - Yadhuru nini? Lakini kwa njia zote, ikiwa ni kwa hila, au ikiwa ni kwa kweli, Kristo [Masihi] anahubiriwa ; na kwa hiyo nafurahi, naam, nami nitafurahi. Wakolosai 1:27-29 - ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo [Masihi] ndani yenu, tumaini la utukufu 28 ambaye sisi tunamhubiri habari zake tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo [Masihi] . 29 Nami najitaabisha kwa neno lilo hilo, nikijitahidi kwa kadiri ya kutenda kazi kwake atendaye kazi ndani yangu kwa nguvu.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software