Theolojia Katika Picha

1 6 0 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Kutoa Utukufu kwa Mungu (muendelezo)

b. Sifa zitokanazo na mambo yote ni za Mungu na si zetu, Zab. 115:1. c. Tabia ya kuchukua sifa kwa kawaida hutokea tunapompa Mungu nafasi kwenye sehemu ndogo tu ya maisha yetu, badala ya kuona kwamba kila kitu tunachofanya kinaweza kumheshimu au kumvunjia Mungu heshima – kila kitu! Mwandishi Mkristo anayejulikana sana Keith Miller, anaeleza jambo hili vizuri: Haijaacha kunishangaza kwamba sisi Wakristo tumejenga aina ya mtazamo unaobagua mambo, ambao hutufanya kuhusika kwa kina na kwa dhati katika ibada na shughuli za kikanisa na bado tukaishi takriban kama wapagani kabisa [wasiomtambua Mungu] katika maisha ya kila siku ya shughuli zetu na hatujawahi kuligundua hilo.” B. Pili, tunaweza kumnyang’anya Mungu sifa na ibada anayostahili kwa kumpa mtu au kitu kingine utukufu tunaopaswa kumpa Yeye peke yake , Isa. 42:8. Nguvu tatu za dhambi na mbadala wa Mungu: fedha, ngono, na mamlaka (uchoyo, tamaa, na kiburi), 1 Yoh. 2:15-17; Kut. 20:2-3. Inawezekana kufanya ibada ya sanamu bila kufahamu, hata kwa Mkristo, yaani, kuabudu kwa muda kitu kingine kwa kukipa upendo na uaminifu. 1. Unaweza kumwabudu mungu wa anasa na starehe. 2. Watu wengi leo hii wanaabudu kwenye madhabahu ya choyo na mali. (Tunaishi katika utamaduni unaotukuza kupata, kununua, kuuza, kuchukua, kama mambo muhimu zaidi kwenye maisha yetu). Kati ya mwaka 1983 na 1988, Wamarekani walinunua oveni milioni 62 za microwave, magari na malori madogo milioni 88, seti za televisheni za rangi 105, deki za video milioni 63, simu milioni 31 zisizo na waya, na mashine za kujibu simu milioni 30. ~ Newsweek

3. Usimwabudu mungu wa michezo. 4. Usitoe dhabihu kwa mungu wa ndoa na familia.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software