Theolojia Katika Picha
1 6 2 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kutoa Utukufu kwa Mungu (muendelezo)
D. Nne, tunaweza kumwibia Mung utukufu unaomstahili kwa kumpa Mungu chini ya kile anachostahili , Mal. 1:6-8, 12-14. 1. Tunaweza kuwa wabahili katika kutoa sadaka zetu kwa Mungu, tukimpa makombo ya mavuno yetu na ya mioyo yetu , Mal. 3:8-10. 2. Tunaweza kumtoleoa Mungu dhabihu ambazo si kamilifu na zilizojaa mawaa , Mal. 1:8, 13. 3. Tunaweza kumtoleo Mungu matoleo ambayo yamechafuliwa, yaliyotiwa doa na dhambi na makosa maishani mwetu ambayo hayajaungamwa (inawezekana kuja kanisani wakati mambo yameharibika kabisa katika maisha yetu yote) Mal. 1:7. 4. Vielelezo a. Ugonjwa wa «Lolote la zamani litafaa.” b. Mungu hana tatizo. c. Kuna aina tatu za watu wanaoishi kwa ajili ya Bwana. Kuna aina tatu za Wakristo wanaoishi kwa ajili ya Bwana – gumegume , sifongo na sega la asali . Ili kupata chochote kutoka kwa gumegume lazima uipige nyundo. Wakristo wa gumegume humpa Mungu kidogo, na hapo ni baada ya kupigwa nyundo nyingi, ambapo kama matokeo unapata vipande vicheche tu. Ili kupata maji kutoka kwenye sifongo lazima uiminye na kwa kadri unavyotumia nguvu ndivyo unavyopata zaidi. Wakristo wa sifongo wanampa Mungu haki yake, lakini unapaswa kuwabana kila mara ili washiriki. Lakini sega la asali hufurika tu na utamu wake. Mkristo wa aina ya sega la asali amejaa moyo wa Mungu na hutoa tu kutokana na upendo kujitoa kwake kwake kwingi kwa Mungu wake. Ni aina gani ya maisha ya Kikristo unayoishi sasa hivi?
V. Wito Mkuu wa kila Mkristo ni Kumtukuza Mungu katika Vyote Tulivyo, Yote Tusemayo, na Yote Tifanyayo, 1 Kor. 10:31. A. Tunapaswa kumtukuza Mungu katika miili yetu, 1 Kor. 3:16, 17; 6:19-20.
1. Usafi wa kingono. 2. Afya ya kimwili.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software