Theolojia Katika Picha

/ 2 0 7

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

“Lazima Umtumikie Mtu Fulani!”

Zaidi ya nusu ya mifano aliyoichagua Yesu inaelezea mtu ambaye yuko chini ya mamlaka ya mwingine. Mara nyingi neno lililochaguliwa ni mshiriki mmoja wa jozi ya jukumu linalojulikana, kama vile mtoto (kwa baba, pater ), mtumishi (kwa bwana, kyrios ), au mwanafunzi (kwa mwalimu, didaskalos ). Picha nyingine za wale walio chini ya mamlaka ni pamoja na mchungaji ( poimen ) anayechunga kundi la mwingine, mfanyakazi ( ergates ) na mwenye shamba ( oikodespotes ), mtume ( apostolos ) aliyetumwa na mkuu wake, na kondoo ( probaton ) kutii sauti ya mchungaji. Inafurahisha kuona kwamba ingawa wanafunzi wanaandaliwa kwa ajili ya uongozi wa kiroho katika Kanisa, Yesu anaweka mkazo zaidi juu ya wajibu wao kwa mamlaka ya Mungu, kuliko mamlaka ambayo wao wenyewe watayatumia. Kuna maelekezo mengi zaidi kuhusu jukumu la kufuata kuliko kuhusu jukumu la kuongoza [msisitizo ni wangu]. ~ David Bennett, The Metaphors of Ministry , uk. 62.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software