Theolojia Katika Picha

/ 2 1 3

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Maandiko kuhusu Ufalme katika Agano Jipya (muendelezo)

Mathayo 26:29 - Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu. Marko 1:15 - Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili. Marko 4:11 - Akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuijua siri ya ufalme wa Mungu, bali kwa wale walio nje yote hufanywa kwa mifano. Marko 4:26 - Akasema, Ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama mtu aliyemwaga mbegu juu ya nchi. Marko 4:30 - Akasema, Tuulinganishe na nini ufalme wa Mungu? Au tuutie katika mfano gani? Marko 9:1 - Akawaambia, Amin, nawaambia, Pana watu katika hawa wasimamao hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata watakapouona ufalme wa Mungu umekuja kwa nguvu. Marko 9:47 - Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ulitupe; ni afadhali kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum. Marko 10:14-15 - Ila Yesu alipoona alichukizwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao. 15 Amin, nawaambieni, Ye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa. Marko 10:23-25 - Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu! 24 Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake. Yesu akajibu tena, akawaambia, Watoto, jinsi ilivyo shida wenye kutegemea mali kuingia katika ufalme wa Mungu! Marko 3:24 - Na ufalme ukifitinika juu ya nafsi yake, ufalme huo hauwezi kusimama Marko 6:23 - Akamwapia, Lo lote utakaloniomba nitakupa, hata nusu ya ufalme wangu.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software