Theolojia Katika Picha

/ 2 1 5

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g Ă­ a

Maandiko kuhusu Ufalme katika Agano Jipya (muendelezo)

Luka 9:11 - Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa. Luka 9:27 - Nami nawaambia kweli, Wapo katika hawa wanaosimama hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata wauone kwanza ufalme wa Mungu. Luka 9:60 - Akamwambia Waache wafu wawazike wafu wao; bali wewe enenda ukautangaze ufalme wa Mungu. Luka 9:62 - Yesu akamwambia, Mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu. Luka 10:11 - Hata mavumbi ya mji wenu yaliyogandamana na miguu yetu tunayakung’uta juu yenu. Lakini jueni hili, ya kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia. Luka 11:2 - Akawaambia, Msalipo, semeni, Baba [yetu uliye mbinguni], Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.] Luka 11:17-18 - Naye akajua mawazo yao, akawaambia, Kila ufalme uliofitinika wenyewe kwa wenyewe hufanyika ukiwa; na nyumba juu ya nyumba huanguka. 18 Basi, ikiwa Shetani naye amefitinika juu ya nafsi yake, ufalme wake utasimamaje? Kwa kuwa ninyi mnasema kwamba mimi natoa pepo kwa Beelzebuli. Luka 11:20 - Lakini, ikiwa mimi natoa pepo kwa kidole cha Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia. Luka 12:31-32 - Bali utafuteni ufalme wa Mungu, na hayo mtaongezewa. 32 Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme. Luka 13:18 - Kisha alisema, Ufalme wa Mungu umefanana na nini? Nami niufananishe na nini? Luka 10:9 - waponyeni wagonjwawaliomo, waambieni, UfalmewaMungu umewakaribia.

Luka 13:20 - Akasema mara ya pili, Niufananishe na nini ufalme wa Mungu?

Luka 13:28-29 - Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje. 29Nao watakuja watu toka mashariki na magharibi, na toka kaskazini na kusini, nao wataketi chakulani katika ufalme wa Mungu.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software