Theolojia Katika Picha
/ 2 2 3
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Maandiko kuhusu Ufalme katika Agano la Kale (muendelezo)
Zaburi 22:27-28 – Miisho yote ya dunia itakumbuka, Na watu watamrejea Bwana; Jamaa zote za mataifa watamsujudia. 28 Maana ufalme una Bwana, Naye ndiye awatawalaye mataifa. Zaburi 45:6 – Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele, Fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili. Zaburi 47:7-8 – Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote, Imbeni kwa akili. 8 Mungu awamiliki mataifa, Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu. Zaburi 103:17-19 – Bali fadhili za Bwana zina wamchao Tangumilele hata milele, Na haki yake ina wana wa wana; 18 Maana, wale walishikao agano lake, Na kuyakumbuka maagizo yake ili wayafanye. 19 Bwana ameweka kiti chake cha enzi mbinguni, Na ufalme wake unavitawala vitu vyote. Zaburi 105:13 – Wakatanga-tanga toka taifa hata taifa, Toka ufalme mmoja hata kwa watu wengine. Zaburi 145:9-13 – Bwana ni mwema kwa watu wote, Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote. 10 Ee Bwana, kazi zako zote zitakushukuru, Na wacha Mungu wako watakuhimidi. 11 Wataunena utukufu wa ufalme wako, Na kuuhadithia uweza wako. 12 Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu, Na utukufu wa fahari ya ufalme wake. 13 Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote, Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote. Isaya 2:2-5 – Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi. 3 Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu. 4 Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe. 5 Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya Bwana.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software