Theolojia Katika Picha
/ 2 5 7
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Mapokeo (muendelezo)
6. Mitume walipongeza pale ambapo kusanyiko linatumia mapokeo ili kubaki waaminifu kwenye “Neno la Mungu”. 1 Wakorintho 11.2 “Basi nawasifu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale mapokeo vile vile kama nilivyowatolea.” 2 Wathesalonike 2.15 “Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu.” 2 Wathesalonike 3.6 “Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu.”
Kiambatisho A
Waanzilishi wa Mapokeo: Ngazi Tatu za Mamlaka ya Kikristo
Kutoka 3.15 “Tena Mungu akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli maneno haya, BWANA, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu; hili ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote.”
1. Mapokeo yenye Mamlaka: Mitume na Manabii (Maandiko Matakatifu) Waefeso 2.19-21 Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. 20 Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. 21 Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. ~ Mtume Paulo Mungu alifunua kazi yake ya wokovu kwa wale ambao walitoa ushuhuda wao kwa kuona utukufu wake, kwanza katika Israeli, na kisha zaidi sana katika Yesu Kristo Masihi. Ushuhuda huu ni wa lazima kwa watu wote, kwa wakati wote, na kwa mahali popote, ni mapokeo yenye mamlaka ambayo kwayo mapokeo yote yanayofuata yanahukumiwa.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software