Theolojia Katika Picha
2 8 6 /
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Mifano ya Matamko ya Kimadhahebu kuhusu “Ubatizo katika Roho Mtakatifu” (muendelezo)
Uzoefu huu pia unajulikana kwa maneno mbalimbali yanayowakilisha awamu zake tofauti, kama vile “ukamilifu wa Kikristo,” “upendo mkamilifu,” “usafi wa moyo,” “ubatizo wa Roho Mtakatifu,” “utimilifu wa baraka,” na “Utakatifu wa Kikristo.” Tunaamini kwamba kuna tofauti kubwa kati ya moyo safi na ukomavu wa tabia. Ya kwanza hupatikana mara moja, kama matokeo ya utakaso kamili; ya pili ni matokeo ya kukua katika neema. Tunaamini kwamba neema ya utakaso kamili inajumuisha msukumo wa kukua katika neema. Hata hivyo, msukumo huu lazima uendelezwe kwa uangalifu, na uangalizi wa karibu utolewe kwa mahitaji na mchakato wa ukuaji wa kiroho na kule kufanywa kuwa bora katika kumfanania Kristo katika tabia na utu. Pasipo jitihada za makusudi kama hizo ushuhuda wa mtu unaweza kuharibika na neema yenyewe itakazongwa na hatimaye kupotea. Kanisa la Assemblies of God Imetolewa kutoka katika Ushahidi ya Nje ya Kimwili ya Ubatizo katika Roho Mtakatifu (The Initial Physical Evidence of Baptism in the Holy Spirit), http://ag.org/top/position_papers/0000_index.cfm Neno ubatizo katika Roho Mtakatifu limechukuliwa kutoka katika Maandiko. Yohana Mbatizaji alikuwa wa kwanza kulitumia muda mfupi kabla ya Yesu kuanza huduma Yake ya hadharani. Alisema, “Yeye [Yesu] atawabatiza kwa Roho Mtakatifu” (Mathayo 3:11). Mwishoni mwa huduma Yake duniani, Yesu alirejelea maneno ya Yohana (Matendo 1:5); na Petro, katika kuripoti matukio katika nyumba ya Kornelio, pia alirudia kauli hiyo (Matendo 11:16). Ubatizo katika Roho (unaorejelewa pia humu kama Ubatizo) hutokea baadae na ni tofauti na kuzaliwa upya. Maandiko yanaweka wazi kuwa kuna tukio ambalo Roho Mtakatifu huwabatiza waumini katika mwili wa Kristo (1 Wakorintho 12:13), na kuna tukio ambalo Kristo huwabatiza waumini katika Roho Mtakatifu (Mathayo 3:11). Haya hayawezi kumaanisha tukio lile lile kwa kuwa wakala anayebatiza na jambo ambalo muhusika anabatizwa kwalo ni tofauti katika kila tukio. Utofauti wa matukio hayo unaonyeshwa katika sehemu kadhaa. Kisa cha wanafunzi wa Efeso ni mfano. Baada ya kusema kwamba walikuwa wamepokea ubatizo wa Yohana pekee (Matendo 19:3), Paulo alieleza kwamba walipaswa kumwamini Kristo Yesu. Kisha wanafunzi hawa wakabatizwa kwa maji, na kisha Paulo akaweka mikono juu yao na Roho Mtakatifu akaja juu yao. Muda ulikuwa mfupi kati ya wanafunzi hawa kumwamini Kristo na kuja kwa Roho Mtakatifu juu yao, lakini ulikuwa ni muda wa
Ubatizo wa Roho kama tendo lenye
Hatua Nyingi: Mtazamo wa Makanisa ya Kipentekoste
Made with FlippingBook Digital Publishing Software