Theolojia Katika Picha

8 0 /

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Jinsi ya KUPANDA Kanisa (muendelezo)

IV. Lea

1 Wathesalonike 2:5-9 - Maana hatukuwa na maneno ya kujipendekeza wakati wo wote, kama mjuavyo, wala maneno ya juujuu ya kuficha choyo; Mungu ni shahidi. 6 Hatukutafuta utukufu kwa wanadamu, wala kwenu, wala kwa wengine tulipokuwa tukiweza kuwalemea kama mitume wa Kristo; 7 bali tulikuwa wapole katikati yenu, kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake mwenyewe. 8 Vivyo hivyo nasi tukiwatumaini kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapa, si Injili ya Mungu tu, bali na roho zetu pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu. 9 Maana, ndugu, mnakumbuka taabu yetu na masumbufu yetu; kwa kuwa mchana na usiku tulifanya kazi tusije tukamlemea mtu wa kwenu awaye yote, tukawahubiri hivi Injili ya Mungu. A. Kuza ufuasi wa mtu binafsi na wa kikundi. B. Jaza majukumu muhimu katika kanisa: tambua na utumie karama za Roho. Matendo 20:28 - Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe. Matendo 20:32 - Basi, sasa nawaweka katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliotakaswa. Tito 1:4-5 - kwa Tito, mwanangu hasa katika imani tuishirikiyo. Neema na iwe kwako na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Mwokozi wetu. 5 Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuweka wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru. A. Hawilisha uongozi kwa viongozi wenyeji ili waweze kujitawala, kujitegemeza na kujizidisha (Teua wazee na wachungaji). B. Kamilisha maamuzi kuhusu ushirikiano wa kimadhehebu au ushirikiano na taasisi nyingine. C. Lipe kanisa mamlaka ya kujiendesha. D. Kuza ushirika na World Impact na makanisa mengine ya mijini kwa ajili ya ushirika, msaada, na huduma ya umisheni. V. Kipindi cha Mpito

Wezesha

Made with FlippingBook Digital Publishing Software