Theolojia Katika Picha

/ 8 3

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Jinsi ya KUPANDA Kanisa (muendelezo)

Kanuni Kumi za Upandaji Kanisa

1. Yesu ni Bwana. (Mt. 9:37-38) Shughuli nzima ya upandaji kanisa hufanyika kwa ufanisi na kuzaa matunda chini ya ulinzi na nguvu za Bwana Yesu, ambaye mwenyewe ndiye Bwana wa mavuno. 2. Kuwahubiria Injili, Kuwaandaa, na Kuwawezesha watu ambao hawajafikiwa ili kuwafikia wengine. (1 The.1:6-8) Lengo letu la kuwafikia wengine kwa ajili ya Kristo si tu kwa kusudi la uongofu thabiti bali pia kwa ajili ya uzidishaji wenye ufanisi; wale wanaofikiwa lazima wafundishwe ili kuwafikia wengine pia. 3. Fungua milango kwa wote: yeyote anayetaka na aje. (Rum. 10:12) Hakuna mbinu inayopaswa kumkataza mtu au kikundi chochote kuingia katika Ufalme kwa imani kwa njia ya Yesu Kristo. 4. Usiegemee upande wowote wa kitamaduni: Njoo jinsi ulivyo! (Kol. 3:11) Injili haitoi maelekezo kwa mtafutaji yeyote kubadili utamaduni wake kama sharti la kuja kwa Yesu; wanaweza kuja jinsi walivyo. 5. Epuka mawazo ya ngome. (Mdo 1:8) Lengo la umisheni si kujenga ngome isiyopenyeka katikati ya jamii ambayo haijaokoka, bali ni kuanzisha kituo cha nguvu cha Ufalme ambacho kinazindua ushuhuda wa Yesu ndani na nje ya mipaka ya ulimwengu wake. 6. Endelea kuinjilisha ili kuepuka kudumaa. (Rum. 1:16-17) Endelea kutazama upeo wa macho ukiwa na maono ya Agizo Kuu akilini; kukuza mazingira ya ushuhuda thabiti kwa ajili ya Kristo. 7. Vuka vikwazo vya rangi, matabaka, jinsia na lugha. (1 Kor. 9:19-22) Tumia uhuru wako katika Kristo kutafuta njia mpya na za kuaminika za kuwasilisha ujumbe wa Ufalme kwa wale walio mbali zaidi na wigo wa kitamaduni wa kanisa la kimapokeo. 8. Heshimu utawala wa utamaduni pokezi. (Mdo. 15:23-29) Ruhusu Roho Mtakatifu aakisi maono na maadili ya Ufalme wa Mungu katika maneno, lugha, desturi, mitindo, na maisha ya wale ambao wamemkubali Yesu kama Bwana wao. 9. Epuka utegemezi. (Efe. 4:11-16) Usiwe mfadhili kupitiliza wala mchoyo kupita kiasi kwa kusanyiko linalokua; usidharau nguvu ya Roho Mtakatifu itendayo kazi katikati hata ya jumuiya ndogo ya Wakristo ili kuwawezesha kuifanya kazi ya Mungu katika jamii yao wenyewe.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software