Theolojia Katika Picha
/ 8 5
R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a
Kanuni Nyuma ya Unabii Dkt. Don L. Davis
1. Unabii unatoa kweli yenye uvuvio wa kiungu kuhusu Mungu, ulimwengu wake wote, na mapenzi yake. • Mungu ni nani na asili ya kilicho “halisi” ni nini? • Kweli ni nini, na tunawezaje kuijua? • Tulitoka wapi, kwa nini tuko hapa, na tunapaswa kuenenda jinsi gani? 2. Unabii unaanzia katika Roho Mtakatifu, ambaye ndiye chanzo chake. • Ni kipawa chake (Rum. 12:6; 1 Kor. 12:10; Efe. 4:8). • Nabii = “mtu wa Roho,” pneumatikos (1 Kor. 14:37 na Hos. 9:7) • Tumaini la Musa (Hes. 11:16, 29; taz. Lk. 10:1) 3. A ina mbalimbali na tofauti za ufunuo (Yer. 18:18, Sheria kutoka kwa kuhani, ushauri kutoka kwa wenye hekima, na neno kutoka kwa nabii). • Waliishi katika jumuiya na ushirika (vyama), baadhi walikuwa na ukaribu zaidi na maisha ya hekalu, wakati wengine walikuwa makuhani (rej. 2 Wafalme 2:3- ; Eze. 1:3; Yer. 1:1). • Wahenga na waalimu wa hekima walikuwa “wapokeaji na wapatanishi” wa kipawa cha kimungu (rej. Mwa. 41:38; 2 Sam. 14:20; 16:23; 1 Falm. 3:9, nk.). • Mwalimu mwenye hekima na nabii pia: Danieli. 4. Unabii haujihakiki wenyewe: ni lazima uhakikiwe kuwa ni halali. • Kulitokea na migogoro miongoni mwa manabii ndani ya Agano la Kale na Agano Jipya (rej. 1 Falm. 22; Yer. 23; 28 na 2 Kor. 11:4, 13; 1 Yoh. 4:1-3). • Madai ya kinabii lazima yakubaliane na Musa (Kum. 13:1-5) na Yesu (Mt. 7:15; 24:11; 2 Pet. 2:1). • Neno likitokea, limetoka kwa Bwana (Kumb. 18:15-22). • Unabii wote unapaswa kuchunguzwa ili kubaini thamani yake ya ukweli (1 The. 5:19-21). 5. Ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii (Ufu. 19:10). • Unabii unazungumza kuhusu mateso na utukufu wa Masihi (Luka 24:25-27; 44). • Maandiko ya kinabii yanalenga nafsi yake na kazi yake (Yoh. 5:39-40). • Mahubiri ya mitume yalimhusisha na ujumbe wao (Mdo. 3:12-18; 10:43; 13:27; Rum. 3:21-22; 1 Pet. 1:10-12; 2 Pet. 1:19-21).
Made with FlippingBook Digital Publishing Software