Theolojia Katika Picha

/ i x

R e p r e s e n t a n d o l a t e o l o g í a

Utangulizi

Ni vigumu kukanusha thamani ya michoro, alama, vielelezo na chati katika kurahisisha uwasilishaji wa mada ngumu za kitheolojia. Nani hapendi picha na michoro inapotolewa kuelezea masuala magumu ya kimaadili na ya kitheolojia? Kwa njia nyingi, sisi ni viumbe tulioumbiwa uwezo wa kutengeneza taswira, tumezoea ishara na sitiari tunapowasiliana na wengine katika maisha yetu ya kila siku. Ule msemo wa kale, “Picha ina thamani ya maneno elfu moja,” huthibitika kuwa kweli katika mazungumzo ya kila siku na vile vile katika ushairi, sayansi, au kazi nyingine yoyote ya kiakili. Mara nyingi zaidi, mimi hupata ugumu hatimaye kuelewa umuhimu wa wazo hadi nitoe mfano, kuchora, au kuashiria wazo hilo kwa namna moja au nyingine. Michoro na sitiari nzuri ni zana zilizo tayari kuwakilisha na kufupisha dhana na kategoria muhimu za somo lolote au nyanja yoyote ya kitaaluma. Matumizi ya michoro na picha yanaweza kutusaidia sana tunapotafuta kuelewa maana za kina za dhana changamano au ngumu kueleweka au dhana za kiroho. Bila shaka, juhudi zote kama hizo katika kupanga mawazo na dhana kupitia picha na chati zina tabia ya kurahisisha maana na thamani ya kweli inayowasilishwa. Hata hivyo, kuonyesha mawazo magumu kwa njia ya vielelezo na picha ni njia muhimu na yenye manufaa ya kutusaidia kutazama na kuelewa jambo ambalo ni changamano sana na gumu kuelewa. Ingawa mchoro wakati mwingine unaweza kutolewa kama kibadala duni cha maelezo fasaha ya hoja kuhusu wazo au dhana, tamathali za semi, michoro, au alama nzuri, mara nyingi vinaweza kuwa zana ya kutusaidia kupata ufahamu bora zaidi wa fumbo au siri fulani. Manabii na mitume mara nyingi walitumia taswira na mafumbo ili kuwasaidia watu wa Mungu kuelewa namna Mungu alivyolitazama jambo fulani au hali fulani, au kuelewa maana ya fumbo fulani au dhana ambayo Mungu alikuwa akiiwasilisha kwao. Kwa mfano, mitume walitumia lugha za picha za mambo ya kawaida na ya maisha ya kila siku ili kutusaidia kuelewa vizuri zaidi mafumbo ya Mungu. Fikiria mifano inayohusiana na Kanisa: ni familia ya Mungu, mwili wa Kristo, na hekalu la Roho Mtakatifu. Ili kujua kwa ufasaha kanisa ni nini, lazima uzame katika maana ya familia, jinsi mwili unavyofanya kazi, na kile kinachojumuishwa katika kusudi la hekalu. Kwa kweli, bila picha hizo, hutapata kuelewa au kufahamu kikamilifu maana na mantiki halisi ya Kanisa na kile ambacho linapaswa kufanya ulimwenguni. Ninakupa wewe msomaji picha, jedwali na michoro hii kwa unyenyekevu na kwa tahadhari fulani. Vilichorwa ili kuwasaidia wanafunzi wangu kushughulika na maana za kweli na mafumbo mazito ya Biblia. Kutokana na maoni chanya kutoka kwa wanafunzi wangu, naweza kusema kwamba vilithibitika kuwa ya manufaa kwa wengi. Ni maombi yangu kwamba kwa kutolewa huku kwa hiari kwa picha na michoro hii pia itathibitika kuwa ya manufaa katika masomo na tafakuri yako. Nina uhakika kwamba

Made with FlippingBook Digital Publishing Software