Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Kitabu cha Mwanafunzi

/ 5 3

U O N G O F U & W I T O

C. Hukumu ya Mungu itakuwa kali na ya ulimwengu wote: Mungu Mwenyezi atawawajibisha watu wote sawasawa na mwitikio wao kwa mapenzi yake matakatifu.

1. Mungu atawahukumu Israeli na mataifa, Rum. 10 na 11.

2. Mungu atalihukumu Kanisa, 1 Pet. 4:17.

3. Mungu atamhukumu Shetani na malaika walioasi, Ufu. 20:10.

2

4. Mungu atawahukumu waovu waliokufa, Ufu. 20:11-15.

Hitimisho

» Neno la Mungu, kama chombo cha Roho Mtakatifu, linauthibitishia ulimwengu kwa habari ya dhambi, haki, na hukumu. » Kwa habari ya dhambi, Neno la Mungu hututhibitishia kuhusu kutotii kwetu Sheria ya Mungu na kushindwa kuoanisha maisha yetu na tabia na matakwa yake matakatifu. » Kuhusiana na haki, Neno la Mungu linafunua umbali kati ya Bwana kama Mungu mwenye haki isiyo na kikomo na haki yetu wenyewe, ambayo haikubaliki kwake.

Made with FlippingBook Digital Publishing Software