Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Kitabu cha Mwanafunzi
/ 8 9
U O N G O F U & W I T O
D. Ishara ya mwisho ya ndani ya uongofu inahusiana na uwezo wa kumsikiliza Yesu Kristo na kumfuata . Waamini wapya wanaitambua na kuifuata sauti ya Mwokozi.
1. Wale wanaomjua wataisikiliza sauti yake, wala hawataifuata sauti ya wageni (Yohana 10:1-6).
2. Ushirika na Mungu unategemea kuendelea kutembea katika nuru , na kupokea utakaso kupitia damu ya Yesu kwa ajili ya dhambi katika maisha ya mtu, 1 Yoh. 1:5-10.
3. Wale walio wa Mungu wanatamani kumfuata Mungu na kutafuta njia za kuitikia ipasavyo mapenzi yake yaliyonenwa na kufunuliwa, 1 Yohana 2:3-6.
3
II. Neno la Mungu Linazalisha Ndani ya Mkristo Ishara za Nje za Wokovu Ambazo Zinatoa Ushahidi wa Toba na Imani ya Kweli.
A. Uhusiano thabiti na utambulisho pamoja na Wakristo wengine – watu wa Mungu kama familia yake mpya na jamaa zake wapya.
1. Neno la Mungu ni mbegu inayozaa “kuzaliwa upya” katika familia ya Mungu .
a. Tusipozaliwa kutoka juu kwa “maji” na kwa Roho, hatuwezi kuingia katika Ufalme wa Mungu. (1) Yohana 1:12-13 (2) Yohana 3:5
b. Neno la Mungu ni “ mbegu ” na “ neno lililopandikizwa ” ambalo huzaa maisha mapya ndani yetu, Yakobo 1:18, 21.
Made with FlippingBook Digital Publishing Software