Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
This is the Swahili version of Capstone Module 1 Mentor Guide.
Jiwe Walilolikataa Waashi Limekuwa Jiwe Kuu la Pembeni
THE UR BAN
Uongofu & Wito
MI N I S T R Y I NS T I TUT E h u d uma y a WOR L D IMPAC T , I NC .
Mwongozo wa Mkufunzi
Moduli ya 1 Masomo ya Biblia
SWAHILI
M W O N G O Z O W A M K U F U N Z I
Uongofu & Wito
Moduli ya 1
Masomo ya Biblia
Neno Linaloumba
Neno Linalothibitisha
Neno Linalogeuza
Neno Linaloita
Mtaala huu ni matokeo ya maelfu ya masaa ya kazi iliyofanywa na taasisi ya The Urban Ministry Institute (TUMI) na haupaswi kudurufu bila idhini ya taasisi hiyo. TUMI inatoa idhini kwa yeyote anayehitaji kutumia nyenzo hizi kwa ajili ya faida ya ufalme wa Mungu, kwa kutoa leseni za kudurufu za gharama nafuu. Tafadhali tafuta uthibitisho wa Mkufunzi wako ikiwa kitabu hiki kimepewa leseni ipasavyo. Kwa taarifa zaidi kuhusu TUMI na taratibu zetu za utoaji leseni, tembelea www.tumi.org na www.tumi.org/license .
Moduli ya 1 ya Mtaala wa Capstone: Uongofu na Wito – Mwongozo wa Mkufunzi ISBN: 978-1-62932-369-5 © 2005, 2011, 2013, 2015. The Urban Ministry Institute. Haki Zote Zimehifadhiwa. Toleo la kwanza 2005, Toleo la Pili 2011, Toleo la Tatu 2013, Toleo la Nne 2015. © 2024 Toleo la Kiswahili. Kimetafsiriwa na Mch. Eresh Tchakubuta na Samuel Gipper. Tunatambua na kuheshimu utumishi uliotukuka wa Mtume K. E. Kisart kwa kujitolea kwake bila kukatishwa tamaa kuwafundisha viongozi katika Injili. Hairuhusiwi kunakili, kusambaza na/au kuuza vitabu hivi, au matumizi mengine yoyote pasipo idhini, isipokuwa kwa matumizi yanayo ruhusiwa kwa mujibu wa sheria ya Haki Miliki ya Mwaka 1976 au kwa idhini ya maandishi kutoka kwa mmiliki. Maombi ya idhini yatumwe katika maandishi kwa taasisi ya: The Urban Ministry Institute , 3701 E. 13th Street, Wichita, KS 67208. Taasisi ya The Urban Ministry Institute ni huduma ya World Impact, Inc Nukuu zote za Maandiko, isipokuwa kama imeonyeshwa vinginevyo, zimechukuliwa kutoka katika SWAHILI BIBLE UV050(MCR) series® Haki Miliki © 1997, iliyochapishwa na The Bible Society of Tanzania . Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote za kimataifa zimehifadhiwa.
Yaliyomo
Muhtasari wa Kozi
3 5 7
Kuhusu Mkufunzi
Utangulizi wa Moduli
Mahitaji ya Kozi
15
Somo la 1 Neno Linaloumba
1
43
Somo la 2 Neno Linalothibitisha
2
73
Somo la 3 Neno Linalogeuza
3
101
Somo la 4 Neno Linaloita
4
131
Viambatisho
167
Kufundisha Mtaala wa Capstone
177
Mwongozo wa Mkufunzi – Somo la 1
183
Mwongozo wa Mkufunzi – Somo la 2
191
Mwongozo wa Mkufunzi – Somo la 3
199
Mwongozo wa Mkufunzi – Somo la 4
/ 3
U O N G O F U & W I T O
Kuhusu Mkufunzi
Mchungaji Dkt. Don L. Davis ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya The Urban Ministry Institute na ni Makamu wa kwanza wa Rais wa World Impact. Alisoma katika Chuo cha Wheaton College na Chuo cha Uzamili cha Wheaton na kuhitimu kwa ufaulu wa kiwango cha juu, yaani Summa Cum Claude, katika ngazi ya Shahada (1988) na Shahada ya Uzamili (1989) katika Masomo ya Biblia na Theolojia ya Utaratibu. Alipata Shahada yake ya Uzamivu katika Masuala ya Dini (Theolojia na Maadili) katika chuo kikuu cha Iowa School of Religion. Akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi na Makamu wa Rais Mwandamizi wa World Impact , anasimamia mafunzo ya wamishenari wa mijini, wapanda makanisa, na wachungaji wa majiji, na kufanya uwezeshaji kupitia fursa za mafunzo kwa watendakazi Wakristo wa mijini katika uinjilisti, ukuaji wa kanisa, na umisheni wa upainia. Pia anaongoza Mpango wa Mafunzo huria kwa wale wanaosoma wakiwa mbali, vilevile anawezesha Mafunzo ya Kiuongozi kwa mashirika na madhehebu kadhaa kama Prison fellowship, The Evangelical Free Church of America na The Church of God in Christ. Dkt. Davis, ambaye ametunukiwa tuzo nyingi za ualimu na za kitaalamu, amewahi kuwa profesa na Mkuu wa vitivo katika taasisi kadhaa za kitaalamu zenye hadhi ya juu baada ya kuhadhiri na kufundisha kozi za dini, theolojia, falsafa, na mafunzo ya Biblia katika taasisi za elimu ya juu kama vile Chuo cha Wheaton, Chuo Kikuu cha St. Ambrose, Programu ya Shahada ya Uzamili ya Theolojia ya Chuo Kikuu cha Houston, Kitengo cha Dini cha Chuo Kikuu cha Iowa, na Taasisi ya Mafunzo ya Ibada ya Robert E. Webber. Ameandika idadi kubwa ya vitabu, mitaala, na nyenzo za kujifunzia ili kuwaandaa viongozi wa mijini, ikijumuisha mtaala wa mafunzo wa Capstone (hii ni programu mama ya TUMI yenye moduli 16 za hadhi ya mafunzo ya seminari, yanayotolewa kupitia mfumo wa elimu ya masafa), Mizizi Mitakatifu: Kidokezo cha Namna ya Kurejesha Mapokeo Makuu , ambayo inaangazia namna makanisa ya mijini yanavyoweza kufanywa upya kupitia kugundua upya imani halisi, sahihi ya kihistoria; na Mweusi na Mwanadamu: Kumgundua Upya M.L. King kama Nyenzo ya Theolojia na Maadili ya Weusi . Dkt. Davis pia ameshiriki katika mihadhara ya kitaalamu kama the Staley Lecture series, makongamano ya kufanywa upya kama Promise Keeper Rallies na miungano ya kithiologia kama The University of Virginia Lived Theology Project Series. Vilevile alipokea tuzo ya heshima ya mwanafunzi mashuhuri ( Alumni Fellow Award ) kutoka Chuo Kikuu cha Iowa cha Sanaa na Sayansi za Kiliberali mnamo 2009. Dkt. Davis pia ni mwanachama wa The Society of Biblical Literature, na The American Academy of Religion .
/ 5
U O N G O F U & W I T O
Utangulizi wa Moduli
Salamu, wapendwa marafiki, katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Kama wanafunzi wa Yesu Kristo, tunathibitisha imani yetu ya kina katika nguvu ya Neno la Mungu linaloumba, linalothibitisha, linalogeuza na kuita watu katika utumishi. Ili kuelewa baraka ya ajabu ya uongofu na wito, tutahitaji kutathmini kwa kina nafasi ya Neno la Mungu katika Kanisa. Somo letu la kwanza, Neno Linaloumba , linachunguza asili ya Maandiko Matakatifu kama Neno la Mungu. Tutaona kwamba uadilifu kamili wa Mungu mwenyewe ni msingi wa kuaminika kwa Maandiko kusikoweza kutiliwa shaka. Zaidi ya hayo, tutaangazia jinsi Mungu alivyoumba ulimwengu kupitia Neno lake, na jinsi anavyojihusianisha kikamilifu na Neno katika Yesu Kristo. Sisi kama vyombo ambavyo Roho Mtakatifu hutumia kuumba maisha mapya ndani ya wale wanaoamini, tunathibitisha kuwa sisi ni wanafunzi wa kudumu wa Neno la Yesu. Kama washirika wa Kanisa, tunapokea Neno pamoja katika kusanyiko, Neno lile lile linalotupatia kusudi kuu la ulimwengu ulioumbwa, ambalo ni utukufu wa Mwenyezi Mungu. Katika somo linalofuata, Neno Linalothibitisha , tutaangalia jinsi Neno la Mungu linavyothibitisha juu ya dhambi, haki, na hukumu. Neno linafundisha kwamba dhambi imeenea katika ulimwengu wote na ina asili ya uharibifu. Neno la Mungu pia huthibitisha kuhusu haki, likiifunua haki kamilifu ya Mungu na kutotosheleza kwetu kimaadili. Na, linathibitisha kwa habari ya hukumu, likifundisha kwamba Mungu atawahukumu kwa hukumu yake ya haki Israeli na mataifa, Kanisa, Shetani na malaika zake, na waovu wote waliokufa. Neno la Mungu pia hututhibitishia juu ya kweli—ya Yesu Kristo, Ufalme wa Mungu, na uadilifu wa Neno lake kupitia wajumbe wake, manabii na Mitume. Somo la tatu, Neno Linalogeuza , linazingatia nguvu ya Neno la Mungu kuleta maisha mapya ndani ya mwamini. Neno hili linalobadilisha kwa maneno mengine ni Injili ya Yesu; ni habari njema ya wokovu ambayo inatufanya “tuzaliwe mara ya pili,” tupitie tendo la kuoshwa kwa kuzaliwa upya, na kufanywa upya na Roho Mtakatifu. Neno huzaa ndani yetu sisi tunaoamini ishara thabiti za uwezo wa Mungu wa kufanya upya. Neno hili hili ambalo huzalisha maisha mapya, pia hututegemeza, hutupatia lishe ya kiroho, husababisha ukuaji wetu, na hutuwezesha kujilinda dhidi ya uongo wa shetani. Hatimaye, somo la nne, Neno Linaloita , linachunguza dhana ya ( metanoia ), yaani, toba kwa Mungu, na imani (pistis ). Imani katika Yesu Kristo ndiyo njia ambayo
6 /
U O N G O F U & W I T O
Mungu humkomboa na kumwokoa mwamini na adhabu, nguvu, na uwepo wa dhambi. Tunapogeuka kutoka dhambini na kumgeukia Mungu katika Kristo, Neno hutuongoza kupokea asili mpya ya Mungu (kuzaliwa upya) na kuingizwa (kuasiliwa) katika kusanyiko la watu wa Mungu (yaani laos ya Mungu) kwa neema kwa njia ya imani pekee. Neno linalotuita kuingia katika wokovu pia linatuita kwenye uanafunzi (kama watumwa wa Yesu), kwenye uhuru (kama watoto waliokombolewa) na utume (kufanya wanafunzi kupitia ushuhuda wetu na matendo yetu mema). Kwa kweli, Maandiko Matakatifu ni Neno linalofaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema (2 Tim. 3:16-17). Mungu akubariki unapochunguza utajiri wa Neno lake alilolivuvia kwa pumzi yake, linaloumba, linalothibitisha, linalogeuza na linaloita!
- Mch. Dkt. Don L. Davis
/ 7
U O N G O F U & W I T O
Mahitaji ya Kozi
• Biblia (kwa madhumuni ya kozi hii, Biblia yako inapaswa kuwa tafsiri [mf. BHN, SUV, NEN, SRUV, au NIV, NASB, RSV, KJV, NKJV, n.k. ikiwa utatumia Biblia ya Kiingereza], na sio Biblia iliyofafanuliwa [mf. The Living Lible, The Message ]). • Kila moduli katika mtaala wa Capstone imeainisha vitabu vya kiada ambavyo vinatakiwa visomwe na kujadiliwa katika muda wote wa kujifunza moduli husika. Tunakuhimiza kusoma, kutafakari, na kufanya kazi husika pamoja na wakufunzi wako, wasimamizi, na wanafunzi wenzako. Kutokana na uhaba wa vitabu unaoweza kujitokeza kwa sababu kadha wa kadha (k.m., kushindwa kuchapisha vitabu vya kutosha), tunaweka orodha yetu ya vitabu rasmi vya Capstone vinavyohitajika kwenye tovuti yetu. Tafadhali tembelea www.tumi.org/books ili kupata orodha ya vitabu vinavyohitajika kwa ajili ya moduli hii. • Daftari na kalamu kwa ajili ya kuchukua maelezo na kufanyia kazi za darasani. • Fee, Gordon D. na Douglas Stuart. How to Read the Bible for All its Worth . Grand Rapids: Zondervan, 1982. • Montgomery, J. W. mh. God’s Inerrant Word . Minneapolis: Bethany, 1974. • Packer, J. I. “Fundamentalism” and the Word of God . London: IVP, 1958. • Sproul, R. C. Knowing Scripture . Downers Grove: IVP, 1977.
Vitabu na Nyenzo Zingine Zinazohitajika
Vitabu vya Kusoma
8 /
U O N G O F U & W I T O
Muhtasari wa Mfumo wa Kutunuku Matokeo na Uzito wa Gredi
Mahitaji ya Kozi
Mahudhurio na ushiriki darasani . . . . . . . 30% Majaribio . . . . . . . . . . . . . . . . . 10% Mistari ya Kukumbuka . . . . . . . . . . . 15% Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko. . . . . . . . 15% Kazi ya Huduma kwa Vitendo. . . . . . . . 10% Usomaji na Kazi za Kufanyia Nyumbani. . . . 10% Mtihani wa Mwisho. . . . . . . . . . . . . 10%
alama 90 alama 30 alama 45 alama 45 alama 30 alama 30
alama 30 Jumla: 100% alama 300
Mambo ya Kuzingatia katika Utoaji Maksi
Kuhudhuria kila kipindi ni moja ya masharti ya msingi ya kozi hizi. Kukosa kipindi kutaathiri matokeo yako. Ikiwa una dharura isiyoepukika itakayokulazimu kukosa kipindi, tafadhali mjulishe mkufunzi wako mapema. Ukikosa kipindi ni jukumu lako kutafuta taarifa kuhusu kazi na mazoezi yaliyotolewa, na kuongea na mkufunzi wako pale inapobidi kufanya na kukabidhi kazi kwa kuchelewa. Sehemu kubwa ya mafunzo yanayohusiana na kozi hii hufanyika kupitia mijadala. Kwa hivyo, unahimizwa na kutarajiwa kushiriki kikamilifu katika kila kipindi cha kozi hii. Kila kipindi kitaanza na jaribio fupi kuhusu mawazo ya msingi yaliyofundishwa katika somo lililopita. Njia nzuri zaidi ya kujiandaa na majaribio haya ni kupitia Kitabu cha Mwanafunzi na daftari uliloandikia maelezo ya somo hilo lililopita. Kukariri Neno la Mungu ni kipaumbele cha msingi kwa maisha na huduma yako kama mwamini na kiongozi katika Kanisa la Yesu Kristo. Kozi hii ina mistari ya Biblia michache, lakini yenye umuhimu mkubwa katika jumbe zake. Katika kila kipindi utahitajika kukariri na kunukuu (kwa mdomo au kuandika) mistari ya Biblia uliyopewa na mkufunzi wako. Neno la Mungu ni zana yenye nguvu ambayo Mungu anaitumia ili kuwaandaa watumishi wake kwa kila kazi ya huduma aliyowaitia (2 Tim. 3:16-17). Ili kutimiza matakwa ya kozi hii, lazima uchague kifungu cha Biblia na kufanya uchambuzi wa kina (yaani, eksejesia au ufafanuzi wa Maandiko). Kazi yako iwe na kurasa tano ziliyochapwa kwa kuacha nafasi mbili kati ya mistari au kuandikwa vizuri kwa mkono na iweze kushughulikia mojawapo ya vipengele vine vya Neno la Mungu vilivyoangaziwa katika kozi hii. Ni shauku na matumaini yetu kwamba utashawishika kikamilifu na kuamini juu ya uwezo wa Maandiko kuleta badiliko
Mahudhurio na Ushiriki Darasani
Majaribio
Kukariri Mistari ya Biblia
Kazi za Ufafanuzi wa Maandiko
/ 9
U O N G O F U & W I T O
na athari chanya katika maisha yako na ya wale unaowahudumia. Unapoendelea katika kozi hii, kuwa wazi na tayari endapo utapata kifungu kirefu (takriban mistari 4-9) kuhusu mada ambayo ungependa kujifunza kwa undani zaidi. Maelezo yote kuhusiana na kazi hii yametolewa katika ukurasa wa 10-11, na yatajadiliwa katika sehemu ya utangulizi ya kozi hii. Matarajio yetu ni kwamba wanafunzi wote watatumia mafunzo haya kivitendo katika maisha yao na katika majukumu yao ya kihuduma. Mwanafunzi atakuwa na jukumu la kufikiria namna ya kufanya mafunzo ya huduma kwa vitendo kwa kutumia kanuni alizojifunza katika mazingira halisi ya huduma. Maelezo ya namna ya kufanya mafunzo kwa vitendo yanapatika katika ukurasa wa 12, na yatajadiliwa katika kipindi cha utangulizi wa kozi. Mkufunzi wako anaweza kutoa kazi za darasani na kazi za nyumbani za aina mbalimbali wakati wa vipindi vya masomo au anaweza kuziandika katika Kitabu cha Mwanafunzi ulichonacho. Ikiwa una swali lolote kuhusu kile kinachohitajika kuhusiana na kazi hizi au muda wa kuzikusanya, tafadhali muulize mkufunzi wako. Ni muhimu kwa kila mwanafunzi kusoma maeneo yote ambayo inampasa kusoma katika vitabu husika vya kozi hii au katika Maandiko Matakatifu ili kujiandaa kwa ajili ya mijadala darasani. Tafadhali hakikisha unajaza na kukabidhi kwa Mkufunzi wako “Fomu ya Ripoti ya Usomaji” iliyomo katika Kitabu cha Mwanafunzi, kila wiki. Kutakuwa pia na fursa ya kupata alama za ziada endapo utasoma zaidi ya ulivyoagizwa. Mwishoni mwa kozi, Mkufunzi wako atakupa mtihani wa mwisho utakaofanyia nyumbani. Katika mtihani huo hautaruhusiwa kutumia vitabu vyako vya kozi hii isipokuwa Biblia. Utaulizwa swali ambalo litakusaidia kutafakari juu ya yale uliyojifunza katika kozi na namna yanavyoathiri mfumo wako wa fikra na utendaji wako katika huduma. Utakapokabidhiwa mtihani wa mwisho, mkufunzi wako atakupa taarifa zaidi kuhusu tarehe za kukamilisha na kukabidhi mtihani wako na kazi nyinginezo.
Kazi ya Huduma
Kazi za Darasani na za Nyumbani
Kazi za Usomaji
Mtihani wa Mwisho wa Kufanyia Nyumbani
Gredi za Ufaulu
Mwishoni mwa kozi hii, gredi zifuatazo zitatolewa na kuhifadhiwa kwenye mbukumbu za kila mwanafunzi: A – Bora D – Inaridhisha B – Nzuri sana F – Hairidhishi (Feli) C – Nzuri I – Isiyokamilika
1 0 /
U O N G O F U & W I T O
Matokeo ya mwisho wa kozi yatatolewa katika mfumo wa gredi kwa kutumia skeli ya kutunuku matokeo kwa mtindo wa herufi zenye alama chanya na hasi, kisha alama za gedi yako ya ufaulu katika kazi mbali mbali zitajumlishwa na kugawanywa kwa idadi ya kazi na vipimo vingine husika ili kupata wastani wa matokeo yako ya mwisho. Kuchelewesha au kushindwa kabisa kukabidhi kazi zako kutaweza kuathiri matokeo yako. Hivyo, ni vyema kupangilia shughuli na muda wako mapema na kuwasiliana na mkufunzi wako endapo kutakuwa na changamoto yoyote. Kama sehemu ya ushiriki wako katika mafunzo ya moduli hii ya Uongofu na Wito, utahitajika kufanya kazi ya ufafanuzi wa kina ( eksejesia ) wa mojawapo ya vifungu vifuatavyo katika Neno la Mungu: Zaburi 19:7-11 Isaya 55:8-11 1 Wakorintho 2:9-16 2 Timotheo 3:15-17 1 Petro 1:22-25 2 Petro 1:19-21 Madhumuni ya kazi hii ya ufafanuzi ni kukupa fursa ya kufanya utafiti wa kina wa kifungu kimojawapo muhimu juu ya asili na kazi ya Neno la Mungu. Unaposoma mojawapo ya maandiko yaliyo hapo juu (au andiko ambalo wewe na Mkufunzi wako mtakubaliana ambalo huenda halipo kwenye orodha), tunatumaini kwamba utaweza kuonyesha jinsi kifungu hicho kinavyoangazia au kuweka wazi umuhimu wa Neno la Mungu kwa hali yetu ya kiroho na kwa maisha yetu pamoja katika Kanisa. Pia tunatamani kwamba Roho akupe utambuzi wa jinsi unavyoweza kuhusisha maana yake moja kwa moja na mwenendo wako binafsi wa ufuasi, pamoja na jukumu la uongozi ambalo Mungu amekupa kwa sasa katika kanisa na huduma yako. Hii ni kazi ya kujifunza Biblia, na ili kufanya kazi ya eksejesia, ni lazima udhamirie kuelewa maana ya andiko husika katika muktadha wake. Ukishajua andiko lilimaanisha nini kwa wasomaji wake wa kwanza, unaweza kupata kanuni zinazotuhusu sisi sote leo, na kuzihusianisha na maisha. Mchakato wa hatua tatu rahisi unaweza kukuongoza katika jitihada zako binafsi za kujifunza kifungu cha Biblia: 1. Je, Mungu alikuwa akisema nini kwa watu katika muktadha wa asili wa andiko husika? 2. Ni kanuni gani ambazo andiko hili linafundisha ambazo ni kweli kwa watu wote kila mahali, ikiwa ni pamoja na sisi leo? Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko (Eksejesia)
Dhumuni
Mpangilio na Muundo
/ 1 1
U O N G O F U & W I T O
3. Ni kitu gani Roho Mtakatifu ananiagiza kufanya kupitia kanuni hii, leo, katika maisha na huduma yangu? Baada ya kuwa umeyajibu maswali haya katika kujifunza kwako kibinafsi, hapo sasa utakuwa tayari kuendelea kuandika ulichokigundua katika kazi uliyopewa . Angali hapa chini mfano wa muhtasari wa kazi yako: 1. Eleza kile unachoamini kuwa ndio mada kuu au wazo kuu la andiko ulilochagua. 2. Eleza kwa muhtasari maana ya andiko hilo (unaweza kufanya hivi katika aya mbili au tatu, au, ukipenda, kwa kuandika ufafanuzi mfupi wa mstari kwa mstari juu ya kifungu husika). 3. Eleza kanuni kuu moja hadi tatu au maarifa ambayo kifungu hiki kinatoa kuhusu Yesu Kristo na kazi yake. 4. Eleza jinsi kanuni moja, kadhaa, au zote zinaweza kuhusiana na yafuatayo: Kwa msaada au mwongozo, tafadhali uwe huru kusoma vitabu vya rejea vya kozi hii na/au vitabu vya mafafanuzi ( commentaries ), na kutumia maarifa yaliyomo katika vyanzo hivyo katika kazi yako. Unapotumia maarifa au mawazo ya mtu mwingine kujenga hoja zako, hakikisha unatambua kazi za waandishi husika kwa kutaja vyanzo vya taarifa hizo. Astahiliye heshima apewe heshima yake. Tumia marejeleo ya ndani ya maandishi ( in-text-refences ), tanbihi ( footnotes ), au maelezo ya mwisho ( endnotes ). Njia yoyote utakayochagua kutaja rejea zako itakubalika, ilimradi 1) utumie njia hiyo moja katika kazi nzima, na 2) uonyeshe pale unatumia mawazo ya mtu mwingine, na umtambue mwandishi husika kwa kumtaja. (Kwa maelezo zaidi, angalia katika Kiambatisho cha Namna ya Kuandika Kazi Yako: Mwongozo wa Kukusaidia Kutambua Waandishi wa Vitabu vya Rejea ). Kabla hujakabidhi kazi yako, hakikisha inasifa zifuatazo: • Imeandikwa au kuchapwa vizuri na inasomeka na kueleweka. a. Kiroho chako binafsi na namna unavyotembea na Kristo b. Maisha na huduma yako katika kanisa lako la mahali pamoja c. Hali au changamoto katika jamii yako kwa ujumla.
• Ni uchambuzi wa mojawapo ya vifungu hapo juu. • Imekusanywa kwa wakati (si kwa kuchelewa). • Ina urefu wa kurasa 5.
1 2 /
U O N G O F U & W I T O
• Inafuata muhtasari au mpangilio uliotolewa hapo juu, na imeandikwa kwa namna ambayo msomaji ataweza kuelewa. • Inaonyesha jinsi kifungu husika kinavyohusiana na maisha na huduma leo. Usiruhusumaagizo haya yakuogopeshe; hii ni kazi ya kujifunza Biblia! Unachohitaji kuonyesha katika kazi hii ni kwamba ulisoma andiko husika, umeeleza kwa muhtasari maana yake, ukaweza kupata kanuni chache muhimu kutoka katika andiko hilo, na kuzihusianisha na maisha na huduma yako mwenyewe. Kazi ya ufafanuzi inabeba alama 45 na inawakilisha 15% ya jumla ya maksi zako, hivyo hakikisha kwamba unaifanya kazi yako kuwa bora na yenye maarifa ya kutosha ya Neno la Mungu. Uongozi wa Kikristo sio tu kujua kile ambacho Biblia inasema; unahusisha uwezo wa kutumia Neno la Mungu kwa njia ambayo wengine wanajengwa na kukamilishwa kwa ajili ya kazi ya huduma. Neno la Mungu li hai na linafanya kazi, na hupenya hadi kwenye kiini cha maisha yetu na mawazo ya ndani kabisa (Ebr. 4:12). Mtume Yakobo anaweka msisitizo zaidi juu ya kuwa watendaji wa Neno la Mungu, na si wasikiaji tu, tukijidanganya wenyewe. Tunahimizwa kulifanyia kazi, kulitii. Anaongeza kusema kwamba kupuuza nidhamu hii ni sawa na sisi kujitazama sura zetu za asili katika kioo na mara tunapoondoka tunasahau asili yetu (sis ni nani) na tulichokusudiwa kuwa. Katika kila hali, mtendaji wa Neno la Mungu atabarikiwa katika kila atendalo (Yak. 1:22-25). Shauku yetu ya dhati ni kwamba uweze kutumia maarifa unayojifunza kwa vitendo, ukiihusianisha elimu hii na masuala na mahitaji halisi katika maisha yako binafsi, na huduma yako ndani ya kanisa lako na kupitia kanisa lako. Kwa hivyo, sehemu muhimu ya kukamilisha moduli hii ni wewe kubuni kazi ya huduma kwa vitendo ili kukusaidia kuwashirikisha watu wengine baadhi ya maarifa ambayo umejifunza kupitia kozi hii. Kuna njia nyingi ambazo unaweza kutumia kutimiza takwa hili la kujifunza kwako. Unaweza kuchagua kuwa na muda wa kujifunza na mtu binafsi, kutumia madarasa ya Shule ya Jumapili, vikundi vya vijana au watu wazima, au hata kwa kupata nafasi ya kuhudumu mahali fulani. Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unajadili na hadhira baadhi ya maarifa uliyojifunza kutoka darasani. (Bila shaka, unaweza kuchagua kuwashirikisha baadhi ya maarifa kutoka katika kazi yako ya eksejesia ya moduli hii). Kazi ya huduma
Utoaji Maksi
Dhumuni
Mpangilio na Muundo
/ 1 3
U O N G O F U & W I T O
Uwe huru na tayari kubadilika na kuendana na mazingira yoyote unapofanya kazi yako. Ifanye iwe yenye ubunifu na inayoruhusu kusikiliza mitazamo tofauti kwa nia ya kujifunza. Fanya uchaguzi mapema kabisa kuhusu aina ya muktadha ambao unatamani kutumia kushirikisha watu wengine maarifa haya na kisha mshirikishe Mkufunzi wako juu ya maamuzi hayo. Panga hayo yote mapema na epuka kusubiri dakika za mwisho kuamua na kutekeleza kile unachotaka katika kazi yako. Baada ya kutekeleza kazi yako, andika kwa ufupi (ukurasa mmoja) tathmini ya kazi yako na umkabidhi mkufunzi wako. Mfano wa muhtasari wa Kazi ya Huduma ni kama ifuatavyo: 1. Jina lako 2. Eneo ulilolitumia na hadhira uliyowashirikisha. 3. Muhtasari wa namna muda wako ulivyoenda, namna ulivyojisikia na namna watu walivyoitikia. 4. Ulijifunza nini kupitia mchakato mzima wa kazi yako. Kazi ya huduma inabeba alama 30 ambazo zinawakilisha 10% ya jumla ya maksi zako, hivyo hakikisha unashirikisha yale uliyojifunza kwa ujarisi na ripoti yako iwe yenye kueleweka vizuri.
Utoaji Maksi
/ 1 5
U O N G O F U & W I T O
Neno Linaloumba
S O M O L A 1
ukurasa 177 1
Karibu katika Jina lenye nguvu la Yesu Kristo! Baada ya kusoma, kujifunza, kushiriki katika mijadala, na kutendea kazi yaliyomo katika somo hili, utakuwa na uwezo wa: • Kutetea wazo kwamba Maandiko Matakatifu ni Neno la Mungu, rekodi iliyoandikwa ya Neno la Bwana lenye uzima na la milele. • Kuonyesha kutoka katika Maandiko kwamba Mungu wa Biblia, Mungu wa Utatu, anatoa uhakikisho kwamba Neno la Mungu ni la kweli, jambo ambalo linalifanya liwe na sifa ya kutegemeka kabisa. Vitu vyote katika ulimwengu viliumbwa kupitia Neno la Mungu linaloumba na kutoa uhai. • Kueleza jinsi Bwana Mungu anavyojihusianisha kikamilifu na Neno la Mungu, hasa katika Yesu Kristo, Nafsi ya Pili ya Utatu, ambaye kupitia kwake Mungu amejifunua, anaukomboa ulimwengu, na ataurudisha ulimwengu chini ya utawala wake wa haki. • Kuthibitisha kwa kutumia Maandiko kwamba Neno la Mungu, likiwa limeingiziwa uhai wa Mungu mwenyewe, ni njia ambayo Roho Mtakatifu anaumba maisha mapya kwa wale wanaoamini. • Kufafanua ukweli kwamba kupokea Neno na kudumu katika Neno hili la Mungu lililopandikizwa ndani yetu ni ishara ya kweli ya ufuasi na kufanywa wana wa kweli katika familia ya Mungu. Kama watakatifu wa Mungu, tunapokea Neno la Mungu pamoja katika jamii yake ya agano. • Kuonyesha jinsi Neno linavyofunua kusudi kuu la ulimwengu ulioumbwa, ambalo ni utukufu wa Mwenyezi Mungu. • Kunukuu kwa moyo kifungu kinachohusiana na nguvu ya uumbaji ya Neno la Mungu.
Malengo ya Somo
ukurasa 177 2
1
Kutamanika kwa Neno Hai la Mungu
Ibada
Soma Zaburi 19:7-11 . Zama zetu zinajulikana zaidi kama zama za shauku. Watu wanajibidiisha kwa nguvu kubwa kupata vitu, kupata raha, kupata vyeo, na kutimiza malengo yao, huku nyakati fulani wakijitaabisha sana kwa ajili ya mambo wanayotamani. Labda janga la kusikitisha zaidi katika maisha ya mamilioni ya watu
ukurasa 177 3
1 6 /
U O N G O F U & W I T O
ni kwamba wanajitaabisha kwa mambo ambayo, mwisho wa siku, hayatakuwa na umuhimu wowote. Wanaishi kwa ajili ya raha za muda mfupi, mali, na mambo ya kibinafsi ambayo ndani ya miaka mia moja hayatakuwapo au hayatakuwa na umuhimu wowote. Ili kuishi vizuri kweli hatupaswi kuwa na shauku kubwa tu, bali lazima tuelekeze shauku na matamanio yetu katika mambo yatakayodumu, na mambo ya maana zaidi. Kwa mujibu wa Neno la Mungu, kuna vitu vichache sana vyenye sifa ya kuwa vitu vya maana sana, na kwa sababu hiyo, kuna vitu vichache tu vinavyostahili kutamanika na kutafutwa. Mojawapo ya hazina ya maana sana inayotajwa katika Maandiko ni Neno la Mungu lenyewe. Mungu anatangaza kwamba Neno lake, Neno lililoandikwa, yaani Maandiko Matakatifu, ni hazina ambayo inastahili jitihada zetu za unyoofu na bidii zaidi katika kulipata. Hakuna kitu duniani kinachodumu kama hicho; hakuna kinachoweza kutupatia hekima, ufahamu, tumaini, na shangwe ambayo Neno linatoa. Neno la Mungu ni mali yenye utajiri mwingi, hutiamacho nuru, hufurahishamoyo, huhekimisha nafsi, na kuleta tumaini katika maisha ya mtu. Mtunga-zaburi hapa anaonyesha wazi jinsi Neno lililo hai la Mungu linavyostahili kutamanika kwetu. Hakuna kitu ambacho tunamiliki au ambacho tunaweza kumiliki chenye thamani na umuhimu kama Neno la Mungu kuhusu Mwanawe, mpango wake, na tumaini letu. Katika kulishika tunaonywa, na katika kushikamana nalo kuna thawabu kubwa. Je, unatafuta Neno la Mungu kama vile unavyotafuta pesa, au raha, au muda huru wa kujiburudisha, au nafasi kubwa? Hakuna kitu katika ulimwengu huu chenye thamani au umuhimu kama ujuzi wa kina wa Neno la Mungu. Haja ya moyo wako iko wapi leo? Baada ya kutamka na/au kuimba Kanuni ya Imani ya Nikea (katika kiambatisho), sali sala ifuatayo: Mungu wa Milele, Baba yetu, tunakusifu kwa nia yako ya kujidhihirisha kwetu kupitia Neno lako. Umetubariki kwa kuhifadhi ahadi yako ya neema na matamko yako kwa njia ya Maandiko, ambayo uliyavuvia kwa Roho wako Mtakatifu. Na sasa, kwa njia ya Roho huyohuyo, unatufundisha kuhusu Mwanao, na mpango wako mtukufu wa kurejesha vitu vyote katika yeye. Tunalibariki jina lako kuu na takatifu kwa Neno lako lililo hai na la kudumu, na tunakuomba utujalie hekima yako tunapojifunza pamoja nguvu na ukuu wa Neno lako. Mungu mwenye rehema, Baba wa mbinguni, umetuambia kwa kinywa cha Mwanao mpendwa, Bwana wetu Yesu Kristo, “Mwombeni Bwana wa mavuno,” juu ya agizo lako hili la kimungu, tunaomba kutoka mioyoni mwetu, kwamba umtoe Roho Mtakatifu kwa
1
Kanuni ya Imani ya Nikea na Maombi
ukurasa 178 4
/ 1 7
U O N G O F U & W I T O
wingi kwa watumishi wako hawa, pamoja nasi na wale wote walioitwa kulitumikia neno lako. Amina. ~ Martin Luther . Devotions and Prayers of Martin Luther . Trans. Andrew Kosten. Grand Rapids: Baker Book House, 1965. Uk. 77.
Hakuna jaribio katika somo hili.
Jaribio
Mazoezi ya Kukariri Maandiko
Hakuna maandiko ya kukariri katika somo hili.
1
Hakuna kazi za kukusanya katika somo hili.
Kazi za Kukusanya
MIFANO YA REJEA
Swala la Utaalamu
Katika jamii kwa ujumla leo ni jambo la kawaida kwa watu wengi walio na matatizo ya kitaaluma au ya kibinafsi kuyashughulikia wao wenyewe, au kushauriana na «wataalamu» - wanasayansi, madaktari, washauri, au wengine ambao wanachukuliwa kuwa wao wanaweza kuwawezesha kukabiliana na matatizo yao au kuyatatua. Neno la Mungu lina nafasi gani leo katika kutatua matatizo ya watu? Je, ni kwa njia gani unaona au kushindwa kuona kuheshimiwa kwa mafundisho ya Neno la Mungu katika jamii leo?
1
ukurasa 178 5
Mamlaka Iko Wapi?
Fikiria kwamba suali tata linaibuka katika kundi la huduma ya vijana ya kanisa lako la mahali kuhusu ngono kabla ya ndoa. Watoto wengi wanafundishwa katika shule zao za sekondari kwamba kujihusisha na ngono ni jambo la kawaida na linalotarajiwa, na ni sawa ilimradi wachukue tahadhari dhidi ya magonjwa ya zinaa na hatari ya kupata mimba. Hoja zinazotolewa katika shule za sekondari zinaonekana za kuvutia kwa baadhi ya wanafunzi katika kikundi chako cha vijana, ambao wanashangaa na kuhoji ni kwa namna gani viwango na kanuzi za kitabu cha kale kama Biblia zinaweza kuhusiana nao kama vijana leo. Je, unaweza kusema nini kwa watoto hao ambao wanaelekea hatua ya kukataa mamlaka ya Maandiko juu ya maisha yao, wale ambao wanazidi kusadikishwa kwamba mambo yako sawa ikiwa tutayashughulikia kwa kuwajibika na kwa uwazi?
2
1 8 /
U O N G O F U & W I T O
Yesu – Ndiyo; Biblia – Hapana!
Kuna watu wengi wanaokiri utii wa kina kwa Yesu na mafundisho yake, lakini wana shida na ukweli wa Biblia. Yesu alifundisha upendo, unyenyekevu, na nia njema miongoni mwa watu; Biblia, hata hivyo, imejaa mafundisho ya ajabu kuhusu malaika, mapepo, na miujiza, mambo ambayo watu wengi wa sasa wanaona kuwa magumu au kwamba hayawezekani kuamini. Je, unafikiri inawezekana kumkubali Yesu Kristo huku, wakati huohuo, tukitilia shaka mambo fulani ya Biblia? Unaweza kusema “Ndiyo!” kwa Yesu, lakini “Hapana!” au “sina uhakika” kwa mambo mengi katika Maandiko? Je, ni lazima uamini kila kitu ambacho Biblia inafundisha ili kudai kuwa na uhusiano wa kweli na imani katika Yesu? Ikiwa jibu ni ndiyo, kwa nini? Ikiwa jibu ni siyo kwa nini?
3
1
Neno Linaloumba Sehemu ya 1
YALIYOMO
Mch. Dkt. Don L. Davis
Maandiko Matakatifu ni Neno la Mungu, kumbukumbu ya maandishi ya Neno la Bwana lenye uzima na la milele. Mungu wa Biblia, Mungu wa Utatu, anatoa uhakikisho kwamba Neno la Mungu ni la kweli, jambo ambalo linalifanya liwe na sifa ya kutegemeka kabisa. Vitu vyote katika ulimwengu viliumbwa kupitia Neno la Mungu linaloumba na kutoa uhai. Bwana Mungu anajihusianisha kikamilifu na Neno la Mungu katika Yesu Kristo, Nafsi ya Pili ya Utatu, ambaye kupitia kwake Mungu anajifunua, anaukomboa ulimwengu, na atarudisha ulimwengu chini ya utawala wake wa haki. Lengo letu la sehemu hii ya kwanza ya Neno Linaloumba ni kukuwezesha kuona, kutambua, na kuelewa maana ya jinsi ambavyo: • Maandiko Matakatifu, Neno la Mungu lililo hai na la milele, yanahusianishwa moja kwa moja na nafsi ya Mungu na kazi yake. Kwa hiyo, ni ya kutegemewa kabisa na yenye mamlaka katika yote yaliyomo ndani yake. • Ulimwengu wote mzima na uhai wote uliomo uliumbwa kupitia nguvu zinazotoa uhai za Neno la Mungu. • Mungu anajihusianisha kikamilifu na Neno la Mungu, hasa katika nafsi ya Pili ya Utatu, ambaye kupitia kwake Mungu amejifunua, anaukomboa ulimwengu, na ataurudisha ulimwengu chini ya utawala wake wa haki.
Muhtasari wa Sehemu ya 1
/ 1 9
U O N G O F U & W I T O
I. Maandiko ni Neno la Mungu Aliye Hai, Limevuviwa kwa Pumzi Yake na Kuhusishwa na Nafsi na Kazi Yake.
Muhtasari wa Sehemu ya 1 ya Video
A. Maandiko ni Neno lililo hai na la milele linaloishi na kudumu milele.
1. Neno la Mungu ni la milele, lina sifa ya Mungu ya ukweli kamili na mamlaka, 1 Pet. 1:23-25.
1
2. Maandiko yamevuviwa kwa “pumzi” ya Mungu Mwenyezi.
a. 2 Tim. 3:16-17
b. Mungu alipulizia uhai wake wa uumbaji katika Neno lake.
3. Si lazima kuamini kwamba Mungu alielekeza kila kilichopaswa kuwekwa katika Maandiko ili yawe yamevuviwa na Yeye. Badala yake, tunaamini kwamba Roho Mtakatifu alitumia misamiati, uzoefu, na uwezo wa waandishi kwa njia mahususi aliyokusudia ili matokeo ya uandishi wao yawe ni kazi yake mwenyewe. Roho alivuvia maandiko kwa namna ambayo anaweza kuitwa mwandishi wa nyaraka husika. Ni kwa msingi huu Kanisa limeyahesabu Maandiko kuwa kiwango chenye mamlaka na mwongozo unaotegemeka kwa habari ya imani na utendaji (maisha).
a. 2 Pet. 1:19-21
b. Watu walinena yaliyotoka kwa Mungu huku wakiongozwa na Roho Mtakatifu mwenyewe.
2 0 /
U O N G O F U & W I T O
B. Kwa sababu yamevuviwa na Mungu, haiwezekani, kwa msingi huo, Maandiko kumrudia bure, tupu, au bila matokeo. Kwa kila njia, Neno la Mungu linaonekana kuwa lenye kutegemeka kabisa na lenye mamlaka kabisa, linalostahili kutumainiwa na kujifunza.
1. Isa. 55:8-11
a. Njia za Mungu ziko juu kabisa ya njia zetu, yaani, zaidi ya utafiti au ugunduzi wetu.
1
b. Neno la Mungu linafaa kabisa katika yote ambayo Mungu analiagiza na kuliamuru lifanye.
2. Mungu anathibitisha uhakika kamili wa Neno lake takatifu, Isa. 44:26-28.
a. Mungu anatangaza kwamba atalithibitisha neno la mtumishi wake na kutimiza shauri la wajumbe wake. Neno lake ni kweli.
b. Mungu huthibitisha Neno lake kwa uhakika na uaminifu wa kweli. Kama Yesu alivyosema katika Yohana 10:35, “Maandiko hayawezi kutanguka.”
C. Kwa sababu ya kutegemeka kwake kikamilifu, Neno linaadhimishwa na kusifiwa kila mahali katika Biblia.
1. Linasifiwa kwa umilele wake kamili, Mt. 5:18.
2. Linasifiwa kwa namna ambayo Mungu analitukuza Neno lake, Isa. 42:21.
/ 2 1
U O N G O F U & W I T O
3. Linasifiwa pamoja na jina lake takatifu, Zab. 138:1-2.
4. Linasifiwa kwa uhalisi wake wa milele, Mt. 24:35.
5. Ukamilifu, nuru, kuaminika na uaminifu wa Neno la Mungu unakubaliwa na kuthibitishwa, Zaburi 19 & 119.
ukurasa 178 6
II. Mungu Mwenyezi, Akitenda Kupitia Nguvu ya Uumbaji ya Neno Lake, Aliumba Vitu Vyote Ulimwenguni.
1
A. BWANA, Mungu wa Israeli, ndiye Muumba wa mbingu na nchi; ulimwengu haukujisababisha wenyewe wala haujitegemei.
1. Mwanzo 1:1
2. Mithali 16:4
3. Waebrania 1:10
B. Pili, Mungu aliumba ulimwengu “ ex nihilo ,” yaani pasipo chochote.
1. Ebr. 11:3
2. Zab. 33:6
3. Zab. 33:8-9
2 2 /
U O N G O F U & W I T O
4. 2 Pet. 3:5
C. Mungu aliumba ulimwengu kupitia Logos , Neno la Mungu, ambaye ni Yesu Kristo.
1. Yohana 1:1-3
2. Kol. 1:16
1
3. Neno la Mungu lina nafasi ya juu katika kazi ya uumbaji ya Mungu katika ulimwengu – Neno la Mungu ni Neno linaloumba!
ukurasa 178 7
III. Kuna Uhusiano wa Karibu kati ya Mwenyezi Mungu na Neno Lake, yaani, “Neno.”
A. Mungu amejidhihirisha kupitia ufunuo wa jumla. Ufunuo wa jumla ni ule ufunuo wa Mungu ambao unaweza kupatikana kwa watu wote kila wakati.
1. Mungu amejidhihirisha kwa ujumla katika mpangilio wa uumbaji asilia, katika utukufu wa uumbaji na asili, Zab. 19:1.
2. Mungu amejidhihirisha kwa ujumla katika historia ya wanadamu: watu wa Israeli.
3. Mungu amejidhihirisha kwa ujumla katika asili ya mwanadamu, Zaburi 8.
a. Akili
/ 2 3
U O N G O F U & W I T O
b. Dhamiri
c. Sifa za kiadili na kiroho
B. Mungu pia amejidhihirisha kupitia ufunuo maalum. Kwa ufunuo maalum tunamaanisha kujifunua kwa Mungu kwa watu mahususi kwa nyakati na mahali mahususi kwa makusudi yake mwenyewe.
1
1. Mungu amejidhihirisha katika ufunuo maalum kupitia matukio ya kihistoria.
a. Maisha ya mababa wa Imani
b. Tukio la Kutoka
c. Ujenzi wa Hekalu
2. Mungu amejidhihirisha katika ufunuo maalum kupitia usemi wa kiungu.
a. “Neno la Bwana,” liwe limetolewa kwa sauti, katika ndoto, au katika maono.
b. Njia hii ilikamilishwa katika Neno “kauli,” Maandiko Matakatifu.
3. Mungu amejidhihirisha mwenyewe katika ufunuo maalum kupitia umwilisho wa Neno katika nafsi na kazi ya Yesu Kristo.
2 4 /
U O N G O F U & W I T O
a. Mungu alijitambulisha moja kwa moja na Neno katika nafsi ya Yesu Kristo, Yohana 1:1-2.
b. Yesu Kristo ni Neno la Mungu aliyefanyika mwili (Yohana 1:14). (1) Kudhihirishwa kwa Mungu katika mwili ulimwenguni. (2) Ufunuo maalum kwa ajili ya wanadamu wote kuuona.
c. Hakuna mtu mwingine au kitu kinachoweza kutangaza utukufu wa Mungu kama Neno aliyefanyika mwili. (1) Yohana 1:18 (2) 1 Yohana 1:1-3
1
d. Jina la Yesu linaloitwa waziwazi “Neno la Mungu,” Ufu. 19:13.
C. Aina mbili muhimu za Neno la Mungu: Neno-kauli na Neno-mtu.
1. Aina ya 1: Neno la “kauli” la Mungu – Neno la Mungu lililoandikwa kwa uvuvio
a. Neno la Mungu lililovuviwa, Maandiko ya Kiebrania ya Agano la Kale, na Maandiko ya Kikristo ya Agano Jipya.
b. Maktaba, iliyovuviwa na Roho na kuandikwa kwa zaidi ya miaka 1500, na waandishi 40.
2. Aina ya 2: Neno la Mungu “mtu” - Bwana Yesu Kristo
/ 2 5
U O N G O F U & W I T O
a. Yesu ndiye Neno-mtu la ufunuo wa Mungu, akitoa ushahidi wa mwisho wa nafsi ya Mungu, Mt. 11:27.
b. Yesu ndiye Neno-mtu la ukombozi ambalo linaturudisha kwa Mungu (Yohana 14:6).
Hitimisho
» Maandiko Matakatifu ni Neno la Mungu la uumbaji; kumbukumbu iliyoandikwa ya Neno la Bwana lenye uzima na la milele. Maandiko yanategemeka kabisa na hayakosei. » Mungu aliumba ulimwengu wote kupitia Neno lake la uumbaji na linalotoa uhai.
1
» Mungu anajitambulisha kikamilifu na Neno katika nafsi ya Yesu Kristo.
Tafadhali chukua muda wa kutosha kujibu maswali haya na mengine yaliyoibuliwa katika video kuhusu uwezo wa uumbaji wa Neno la Mungu. Jibu kwa uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana, tumia Maandiko! 1. Ni kwa njia gani Maandiko yanadai kwamba yenyewe ni Neno la Mungu? Sentensi ya kwamba Maandiko yamevuviwa kwa pumzi ya Mungu mwenyewe inamaanisha nini? 2. Ni nini maana ya fundisho la Biblia kwamba Neno la Mungu “linaishi na linadumu milele”? 3. Je, inawezekanaje kwamba Mungu alivuvia tu Neno lake bila kuamuru Neno la Mungu kwa waandishi (yaani kuwaelekeza neno kwa neno), au kuwaweka katika ndoto na kuchukua akili zao? Biblia ina maana gani inaposema kwamba waandishi “waliongozwa” na Roho Mtakatifu? 4. Kwa nini mwamini anaweza kujua kwamba Maandiko ni yenye kuaminika na kutegemeka kabisa? 5. Nini maana ya: Neno la Mungu linaadhimishwa na kusifiwa kila mahali katika Maandiko Matakatifu?
Sehemu ya 1
Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
ukurasa 179 8
2 6 /
U O N G O F U & W I T O
6. Kuna uhusiano gani kati ya uumbaji wa ulimwengu na Neno la Mungu? Nini maana ya maneno ya Kilatini, « ex nihilo ,» na dhana hii inahusiana vipi na mada ya Mungu ya uumbaji? 7. Maandiko yanasema nini kuhusu uhusiano wa uumbaji wa Mungu wa ulimwengu wote mzima na Logos , au Neno la Mungu (yaani, Yesu Kristo)? 8. Nini maana ya “ufunuo wa jumla”? Je, ni njia zipi mahususi ambazo Mungu amejidhihirisha kwa ujumla kwa wanadamu wote? 9. Nini maana ya maneno “ufunuo maalum?” Je, ni njia zipi mahususi ambazo kwazo Mungu amejidhihirisha kwa watu mahususi kwa nyakati na mahali maalum? 10. Je, kuna tofauti gani kati ya Neno la Mungu la “kauli” na Neno “mtu”? Je, dhana hizi zinahusiana vipi? Je, moja inachukua nafasi ya kwanza (yaani, ni muhimu zaidi) kuliko nyingine? Eleza.
1
Neno Linaloumba Sehemu ya 2
Mch. Dkt. Don L. Davis
Neno la Mungu ni njia ambayo kwayo Roho Mtakatifu anaumba maisha mapya ndani ya wale wanaoamini. Kwa hiyo, kupokea Neno na kudumu katika Neno hili la Mungu lililopandikizwa ndani yetu ni ishara ya kweli ya ufuasi na kufanywa wana wa kweli katika familia ya Mungu. Kama watakatifu wa Mungu, tunapokea Neno la Mungu pamoja katika jamii yake ya agano. Hatimaye, kwa sababu ya kutegemeka kwa Neno, ndilo pekee linaloweza kututangazia kusudi kuu la ulimwengu ulioumbwa, ambalo ni utukufu wa Mungu Mwenyezi. Lengo letu la sehemu hii ya pili ya Neno Linaloumba ni kukuwezesha kuona kwamba: • Neno la Mungu limetiwa uzima wa Mungu mwenyewe, na kwa hiyo, hakuna hali ya kiroho au dini ya kweli inayowezekana bila nguvu zinazotoa uhai za Neno la Mungu. Mungu huumba maisha mapya kwa waamini kupitia Neno lake, likiangaziwa na Roho Mtakatifu.
Muhtasari wa Sehemu ya 2
/ 2 7
U O N G O F U & W I T O
• Ishara ya kweli ya ufuasi ni kukaa ndani ya Neno na kuendelea katika upokeaji endelevu wa Neno la Mungu kama roho na kweli. Ukomavu wa kiroho unahusishwa moja kwa moja na kusikia na kutii Neno la Mungu katika Kanisa. • Kwa sababu ya mamlaka yake isiyoweza kukosea, ni Neno la Mungu pekee linaloweza kutupatia kusudi kuu la ulimwengu ulioumbwa, ambalo ni kumletea Mungu heshima na utukufu katika mambo yote.
I. Neno la Mungu Limetiwa Uzima wa Mungu Mwenyewe, na Kwa sababu hiyo Linaumba Maisha Mapya ndani ya Wale Wanaoamini.
Muhtasari wa Sehemu ya 2 ya Video
1
A. Neno hujenga maisha ya kiroho kama matokeo ya imani katika kazi ya Yesu Kristo.
1. Neno la Mungu ni la msingi katika kuumba maisha mapya ya kiroho ndani ya mwamini.
a. Yakobo 1:18
b. Yakobo 1:21
2. Neno la Mungu ndilo chombo, mbegu isiyoharibika, ambayo huzaa maisha mapya ndani yetu kupitia imani yetu katika Yesu Kristo, 1 Pet. 1:22-23.
3. Injili inayomhusu Yesu na Ufalme wake haitokani na mwanadamu, bali “yenyewe ni Neno la Mungu,” 1 Thes. 2:13.
B. Uhai wa kiroho unaumbwa na Neno la Mungu lililo hai: tunaishi kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
2 8 /
U O N G O F U & W I T O
1. Tunashikilia mtazamo huu juu ya mamlaka ya Yesu Kristo.
a. Majaribu ya Yesu
b. Nukuu ya Kumbukumbu la Torati: jukumu la pekee la Neno la Mungu, Kumb. 8:3, taz. Mt. 4:4
2. Neno la Mungu lina uzima wa ajabu wa kiroho na uwezo wa kiuumbaji wa kuangaza rohoni, Zab. 19:7-11.
1
3. Hakuna sehemu yoyote ya Neno la Mungu inayopaswa kuchukuliwa kuwa haina maana au iliyopitiliza; kila nukta itatimizwa, wala haitapita hata moja.
4. Mungu anakataa kabisa kuvunja ahadi yake ya agano: Maandiko ni ya kuaminiwa kwa sababu Mungu ni mwaminifu.
a. 2 Wafalme 13:23
b. 1 Nyakati 16:14-17
C. Mungu hutoa ufahamu wa Neno lake kwa kumtuma Roho wake Mtakatifu kwa waamini, 1 Kor. 2:9-16.
1. Asiyeamini (yaani, “mtu wa asili”) hana Roho Mtakatifu, na kwa hiyo hawezi kuelewa ujumbe au mafundisho ya Neno.
/ 2 9
U O N G O F U & W I T O
2. Mtu wa kiroho, (yaani, yule ambaye ana Roho Mtakatifu na anaongozwa naye), sio tu kwamba anaelewa kile ambacho Neno la Mungu linasema, lakini pia huepuka hukumu ya wale wanaoshindwa kuelewa.
3. Roho yule yule aliyevuvia Neno ndiye anayelifasiri, 2 Pet. 1:21.
II. Ishara ya Kweli ya Uanafunzi ni Kuendelea Ndani ya Neno na kukaa katika Neno la Mungu kama Lishe.
1
A. Dalili ya ufuasi wa kweli ni kuendelea na kudumu katika Neno la Kristo.
1. Yohana 8:31-32
2. “Kukaa” ni kuendelea kuwepo, mtu kufanya makao yake ndani ya-, kukaa ndani ya-, Zab. 1:1-3.
3. Maana ya kudumu ni sawa na dhana ya AK ya kutafakari.
a. Zab. 1:1-3
b. Yos. 1:8
B. Ukuaji na ukomavu wa kiroho unategemea kujilisha kweli za Neno la Mungu linaloumba na kuleta uzima.
3 0 /
U O N G O F U & W I T O
1. Waamini wanapaswa kutamani maziwa yasiyogoshiwa ya Neno la Mungu ili waweze kukua wanapojilisha, 1 Pet. 2:2.
2. Paulo, katika changamoto yake kwa wazee wa Efeso, aliwaweka katika mikono ya Mungu, na kwa Neno la neema yake “ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliotakaswa,” Mdo 20:32.
3. Wakolosai wanahimizwa kuruhusu Neno la Mungu likae kwa wingi ndani yao, Kol. 3:16.
1
4. Paulo anampa Timotheo agizo lenye mamlaka la kujifunza ili kujionyesha kuwa mtenda kazi aliyekubaliwa na Mungu anapokuwa akilitumia (kuligawa) Neno la kweli kwa usahihi, 2 Tim. 2:15.
5. Kuna njia nyingi za kudumu katika Neno la Mungu.
a. Tunapaswa kulisoma . Ufunuo 1:3 inaahidi baraka kwa wale wanaosoma Neno la Mungu.
b. Tunapaswa kulikariri . Katika Zaburi 119:11 Daudi anasema amelificha Neno la Mungu moyoni mwake ili asije akamtenda Bwana dhambi.
c. Tunapaswa kulitafakari . Zaburi 1:3 inasema kwamba mcha Mungu hutafakari na kutafuna Neno la Mungu mchana na usiku.
d. Tunapaswa kulichunguza . Waberoya wanaitwa “watu waungwana zaidi” kuliko Wathesalonike katika Matendo 17:11 kwa sababu hawakusikia tu maneno ya Mtume Paulo, bali walichunguza Maandiko kila siku ili kuthibitisha Injili ya Paulo.
/ 3 1
U O N G O F U & W I T O
e. Tunapaswa kulisikia likihubiriwa na kufundishwa katika Kanisa. Hatupaswi kudharau unabii, bali lisikie Neno kwa maana, kama Warumi 10:17 inavyodokeza, “imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa Neno la Kristo.”
f. Tunapaswa kulijumuisha katika maisha na mazungumzo yetu yote . Neno linaloumba lazima liwe nguvu inayotawala maishani mwetu kama inavyosemwa katika maneno ya Shema, Kum. 6:4-9.
1
C. Neno hili la uumbaji la Mungu lazima lisikike na kupewa utii katika mazingira ya jumuiya ya Kikristo.
1. Msidharau unabii, wala msimzimishe Roho Mtakatifu; 1 Thes. 5:19-22.
2. Neno litakuja katikati ya kusanyiko, 1 Kor. 14:26.
3. Mungu amelipatia Kanisa wanaume na wanawake waliopewa vipawa maalum na Roho Mtakatifu ili kufundisha Neno la Mungu, Efe. 4:11-13.
III. Neno Hufunua Kusudi la Milele la Mungu kwa Ulimwengu: Ili Vitu Vyote Vipate Kumpa Utukufu na Heshima kama Bwana.
A. Kuna pigo moja muhimu zaidi kutoka kwenye moyo wa Hadithi ya Kiungu: Vitu vyote viliumbwa ili kuleta utukufu, heshima, na sifa kwa Bwana na Jina lake tukufu.
1. Vitu vyote viliumbwa kwa kusudi la Mungu lililokusudiwa, Mit. 16:4.
3 2 /
U O N G O F U & W I T O
2. Vitu vyote mbinguni na duniani, vinavyoonekana na visivyoonekana, malaika wote, viumbe vyote, wanadamu na wanyama, na vyote vilivyoko viliumbwa na Mungu kwa utukufu wake.
a. Kol. 1:16
b. Ufu. 4:11
1
c. Zab. 150:6
3. Taifa la Israeli, watu waliochaguliwa na Mungu, walichaguliwa kwa ajili ya utukufu wake mkuu.
a. Isa. 43:7
b. Isa. 43:21
c. Ona Isa. 43:25; 60:1, 3, 21
4. Mungu huwaokoa wanadamu ili kujiletea utukufu na heshima, Rum. 9:23; Efe. 2:7.
5. Huduma zote na kazi ambazo watu wa Mungu hutimiza mwisho wa yote zinapaswa kufanywa kwa utukufu wa Mungu, 1 Kor. 10:31; Yoh. 15:8; Mt. 5:16.
6. Kusudi kuu la mwamini: ushuhuda binafsi kwa utukufu wa Mungu katika Kristo, na kushiriki katika utukufu huo wakati wa kufunuliwa kwake.
/ 3 3
U O N G O F U & W I T O
a. Yoh. 17:22
Ikichukuliwa katika ujumla wake, Biblia inatofautiana katika ujumbe na kusudi lake na kitabu kingine chochote ulimwenguni. Inasimama juu kabisa katika kuakisi na fursa [yake] ya wokovu, tabia kuu na kazi ya Yesu Kristo kama Mwokozi wa pekee, na inatoa kwa undani utukufu usio na kikomo ambao ni wa Mungu mwenyewe. kwake nafasi ya [mwanadamu] kiumbe na kufunua mpango ambao kwa huo [wanadamu] wote katika kutokamilika [kwao] wote wanaweza kupatanishwa katika ushirika wa milele na Mungu wa milele. ~ Lewis Sperry Chafer. Major Bible Themes . Grand Rapids: Zondervan, 1974. uk. 29. Ni kitabu kimoja kinachomfunua Muumba kwa
b. Kol. 3:4
B. Tunapojinyenyekeza chini ya Neno la Mungu linaloumba, tunapata nguvu na mwelekeo ili kutimiza kusudi hili la kumheshimu na kumtukuza.
1. Linafunua nia na matamanio yetu ya ndani, Ebr. 4:12.
1
2. Linaiweka mioyo yetu inayoyumba-yumba katika mstari sanjari na ukuu wa kusudi la milele la Mungu.
a. Maandiko kama furaha na shangwe ya mioyo yetu, Yer. 15:16.
b. Neno la Mungu huleta mguso mkubwa ndani kabisa ya mioyo yetu tunapojisalimisha chini ya nguvu zake, Yer. 20:9.
3. Linatugeuza kwa kufanya upya nia zetu kuyaelekea mapenzi kamili ya Mungu, Rum. 12:1-2.
Hitimisho
» Neno la Mungu limebeba uzima wa Mungu mwenyewe na ni njia ambayo kwayo Roho Mtakatifu anaumba maisha mapya ndani ya wale wanaoamini. » Wanafunzi wa kweli wa Yesu Kristo hukaa katika Neno hili lililopandikizwa ndani yao. » Roho Mtakatifu anatufundisha kwamba kusudi kuu la ulimwengu ulioumbwa ni kumtukuza Mungu Mwenyezi. » Maandiko, Neno linaloumba, hutuwezesha kumtukuza Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu tunapoishi chini ya utawala wa Mungu.
3 4 /
U O N G O F U & W I T O
Maswali yafuatayo yalikusudiwa kukusaidia kufanya mapitio ya maudhui yaliyomo katika video ambayo ililenga sifa za uzima wa Neno la Mungu maishani mwetu. Jibu kwa uwazi na kwa ufupi, na inapowezekana, jenga hoja zako kwa kutumia Maandiko! 1. Je, Biblia inaelezeaje jukumu ambalo Maandiko hutimiza katika kutoa maisha mapya kwa yule anayemwamini Kristo? Je, imani ina jukumu gani pamoja na Neno ili kuumba maisha mapya? 2. Ni kwa njia gani jaribu la Yesu linatufundisha kuhusu nguvu ya Neno la Mungu juu ya maisha yetu? Yesu alitaja kweli gani alipokabiliana na shetani na madanganyo yake nyikani? 3. Roho Mtakatifu ana jukumu gani katika kumsaidia mtu wa kiroho aelewe maana ya Maandiko Matakatifu? Vipi kuhusu mtu wa asili – anaweza kuyaelewa? Ikiwa jibu ni ndiyo, kwa nini; ikiwa jibu ni hapana, kwa nini? 4. Ishara ya kweli ya ufuasi katika Yesu Kristo ni ipi? Eleza uhusiano uliopo kati ya kukua kiroho na kujilisha Neno la Mungu. 5. Ni zipi baadhi ya njia ambazo Maandiko yanafundisha ambazo mtu anaweza kudumu katika Neno la Mungu? Je, kudumu katika Neno kuna uhusiano gani na kuishi katika jumuiya ya Kikristo? 6. Ni watu gani hasa ambao Mungu amelipatia Kanisa ili kulisaidia kuelewa na kutumia Neno la Mungu? Jukumu lao ni lipi katika kusaidia kuwakamilisha Wakristo kwa ajili ya kazi ya huduma? 7. Kulingana na Maandiko, kusudi la milele la Mungu kwa ulimwengu ulioumbwa ni lipi? 8. Hatimaye, ni kusudi gani kuu ambalo Mungu ameweka kwa waamini, na ni kwa jinsi gani wanapaswa kutimiza kusudi hilo maishani mwao? 9. Ni kwa njia gani Maandiko (Biblia) ni ya pekee na yanapita vitabu vingine vyote ulimwenguni? 10. Tunaweza kutazamia nini kutokea katika mioyo yetu na maishani mwetu tunapojitiisha chini ya Neno la Mungu linaloumba? Elezea.
Sehemu ya 2
Maswali kwa Wanafunzi na Majibu
ukurasa 179 9
1
Made with FlippingBook flipbook maker