Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

1 0 /

U O N G O F U & W I T O

Matokeo ya mwisho wa kozi yatatolewa katika mfumo wa gredi kwa kutumia skeli ya kutunuku matokeo kwa mtindo wa herufi zenye alama chanya na hasi, kisha alama za gedi yako ya ufaulu katika kazi mbali mbali zitajumlishwa na kugawanywa kwa idadi ya kazi na vipimo vingine husika ili kupata wastani wa matokeo yako ya mwisho. Kuchelewesha au kushindwa kabisa kukabidhi kazi zako kutaweza kuathiri matokeo yako. Hivyo, ni vyema kupangilia shughuli na muda wako mapema na kuwasiliana na mkufunzi wako endapo kutakuwa na changamoto yoyote. Kama sehemu ya ushiriki wako katika mafunzo ya moduli hii ya Uongofu na Wito, utahitajika kufanya kazi ya ufafanuzi wa kina ( eksejesia ) wa mojawapo ya vifungu vifuatavyo katika Neno la Mungu:  Zaburi 19:7-11  Isaya 55:8-11  1 Wakorintho 2:9-16  2 Timotheo 3:15-17  1 Petro 1:22-25  2 Petro 1:19-21 Madhumuni ya kazi hii ya ufafanuzi ni kukupa fursa ya kufanya utafiti wa kina wa kifungu kimojawapo muhimu juu ya asili na kazi ya Neno la Mungu. Unaposoma mojawapo ya maandiko yaliyo hapo juu (au andiko ambalo wewe na Mkufunzi wako mtakubaliana ambalo huenda halipo kwenye orodha), tunatumaini kwamba utaweza kuonyesha jinsi kifungu hicho kinavyoangazia au kuweka wazi umuhimu wa Neno la Mungu kwa hali yetu ya kiroho na kwa maisha yetu pamoja katika Kanisa. Pia tunatamani kwamba Roho akupe utambuzi wa jinsi unavyoweza kuhusisha maana yake moja kwa moja na mwenendo wako binafsi wa ufuasi, pamoja na jukumu la uongozi ambalo Mungu amekupa kwa sasa katika kanisa na huduma yako. Hii ni kazi ya kujifunza Biblia, na ili kufanya kazi ya eksejesia, ni lazima udhamirie kuelewa maana ya andiko husika katika muktadha wake. Ukishajua andiko lilimaanisha nini kwa wasomaji wake wa kwanza, unaweza kupata kanuni zinazotuhusu sisi sote leo, na kuzihusianisha na maisha. Mchakato wa hatua tatu rahisi unaweza kukuongoza katika jitihada zako binafsi za kujifunza kifungu cha Biblia: 1. Je, Mungu alikuwa akisema nini kwa watu katika muktadha wa asili wa andiko husika? 2. Ni kanuni gani ambazo andiko hili linafundisha ambazo ni kweli kwa watu wote kila mahali, ikiwa ni pamoja na sisi leo? Kazi ya Ufafanuzi wa Maandiko (Eksejesia)

Dhumuni

Mpangilio na Muundo

Made with FlippingBook flipbook maker