Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
1 2 /
U O N G O F U & W I T O
• Inafuata muhtasari au mpangilio uliotolewa hapo juu, na imeandikwa kwa namna ambayo msomaji ataweza kuelewa. • Inaonyesha jinsi kifungu husika kinavyohusiana na maisha na huduma leo. Usiruhusumaagizo haya yakuogopeshe; hii ni kazi ya kujifunza Biblia! Unachohitaji kuonyesha katika kazi hii ni kwamba ulisoma andiko husika, umeeleza kwa muhtasari maana yake, ukaweza kupata kanuni chache muhimu kutoka katika andiko hilo, na kuzihusianisha na maisha na huduma yako mwenyewe. Kazi ya ufafanuzi inabeba alama 45 na inawakilisha 15% ya jumla ya maksi zako, hivyo hakikisha kwamba unaifanya kazi yako kuwa bora na yenye maarifa ya kutosha ya Neno la Mungu. Uongozi wa Kikristo sio tu kujua kile ambacho Biblia inasema; unahusisha uwezo wa kutumia Neno la Mungu kwa njia ambayo wengine wanajengwa na kukamilishwa kwa ajili ya kazi ya huduma. Neno la Mungu li hai na linafanya kazi, na hupenya hadi kwenye kiini cha maisha yetu na mawazo ya ndani kabisa (Ebr. 4:12). Mtume Yakobo anaweka msisitizo zaidi juu ya kuwa watendaji wa Neno la Mungu, na si wasikiaji tu, tukijidanganya wenyewe. Tunahimizwa kulifanyia kazi, kulitii. Anaongeza kusema kwamba kupuuza nidhamu hii ni sawa na sisi kujitazama sura zetu za asili katika kioo na mara tunapoondoka tunasahau asili yetu (sis ni nani) na tulichokusudiwa kuwa. Katika kila hali, mtendaji wa Neno la Mungu atabarikiwa katika kila atendalo (Yak. 1:22-25). Shauku yetu ya dhati ni kwamba uweze kutumia maarifa unayojifunza kwa vitendo, ukiihusianisha elimu hii na masuala na mahitaji halisi katika maisha yako binafsi, na huduma yako ndani ya kanisa lako na kupitia kanisa lako. Kwa hivyo, sehemu muhimu ya kukamilisha moduli hii ni wewe kubuni kazi ya huduma kwa vitendo ili kukusaidia kuwashirikisha watu wengine baadhi ya maarifa ambayo umejifunza kupitia kozi hii. Kuna njia nyingi ambazo unaweza kutumia kutimiza takwa hili la kujifunza kwako. Unaweza kuchagua kuwa na muda wa kujifunza na mtu binafsi, kutumia madarasa ya Shule ya Jumapili, vikundi vya vijana au watu wazima, au hata kwa kupata nafasi ya kuhudumu mahali fulani. Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unajadili na hadhira baadhi ya maarifa uliyojifunza kutoka darasani. (Bila shaka, unaweza kuchagua kuwashirikisha baadhi ya maarifa kutoka katika kazi yako ya eksejesia ya moduli hii). Kazi ya huduma
Utoaji Maksi
Dhumuni
Mpangilio na Muundo
Made with FlippingBook flipbook maker