Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi

1 3 4 /

U O N G O F U & W I T O

K I A M B A T I S H O C H A 2 Tuna amini: Tamko la Kanuni ya Imani ya Nikea (8.7.8.7. Mita*) Mch. Dkt. Don L. Davis, 2007. Haki zote zimehifadhiwa. *Uimbo huu umetengenezwa kutoka katika Kanuni ya Imani ya Nikea na unaweza kuimbwa katika ala hizi 8.7.8.7. Mita, kama: Shangwe, shan gwe, tuna kuabudu wewe, nitamwimbia Mtetezi wangu; Yesu kwetu ni rafiki; njooni, wenye kumngoja Yesu.

Mungu Baba anatawala, yeye aliyezifanya mbingu na nchi. Vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana, kwa yeye, viliumbwa na kwa yeye, vilitolewa.

Tuna amini katika Yesu Kristo, Bwana, Mwana pekee wa Mungu, Aliyetolewa, sio kuumbwa, yeye na Mungu Baba ni wamoja!

Aliyetolewa toka kwa Baba, mwenye asili moja naye, kama Mungu na kama nuru; Kwa yeye vitu vyote viliumbwa na Mungu, katika yeye vitu vyote vilipewa uzima. Yeye aliye kwa ajili yetu sote, kwa ajili ya wokovu wetu, alikuja hapa duniani kutoka mbinguni, akafanyika mwili kwa uweza wa Roho, kupitia kuzaliwa na Bikira mariamu Ambaye kwa ajili yetu pia, alisulibiwa na utawala na mkono wa Pontio Pilato Akateseka, na akazikwa, lakini siku ya tatu, akafufuka. Kama Maandiko matakatifa yalivyosema, yote yaliyotokea yalikusudiwa kuwa hivyo. Akapaa juu katika mkono wa kuume wa Mungu, akikaa katika utukufu mbinguni. Kristo atakuja tena katika utukufu kuwahukumu walio hai na wafu. Utawala wa ufalme wake hautakuwa na mwisho, kwa kuwa atatawala na kuongoza kama kichwa. Tuna mwabudu Mungu, Roho Mtakatifu, Bwana na mpaji wa uzima; Pamoja na Baba na Mwana ametukuzwa, yeye ambaye amesema mara zote kwa njia ya manabii. Na tuna amini katika Kanisa moja, watu watakatifu wa Mungu kwa nyakati zote, Katoliki kwa mipaka na upana wake, lililojengwa katika msingi wa mitume! Tukitambua kwamba ubatizo mmoja, kwa ajili ya msamaha wa dhambi zetu, Na tukitazamia ufufuo, kwa kuwa wafu wataishi tena. Tukitazamia siku zisizokuwa na mwisho, maisha ya nyakati njema zijazo, Pale ambapo utawala wa Kristo utakuja duniani, mapenzi ya Mungu ndipo yatakapo fanyika. Sifa kwa Mungu, na kwa Kristo Yesu, kwa Roho-Bwana katika utatu. Tuna kiri mafundisho ya Kale, tuking’ang’ania kwenye Neno takatifu la Mungu!

Made with FlippingBook flipbook maker