Uongofu na Wito, Swahili Module 1 Mwongozo wa Mkufunzi
2 0 6 /
U O N G O F U & W I T O
na wa jumuiya, wa kibinafsi na wa kijamii, wa kimwili na wa kiroho, wa kumjia Mungu na wa kumjia Kristo. Utajiri wa wito huu kwa Kristo na Ufalme wake ndiyo ambao lazima ueleweke na kuthibitishwa, na mjadala wako juu ya dhana kuu unapaswa kutafuta kuunganisha maarifa haya pamoja kwa uwazi na kibiblia.
Unapozingatia mifano hii, hakikisha kwamba unawasaidia wanafunzi katika majadiliano yao kuunganisha nyuzi mbalimbali za wito wa Mungu katika ushauri na matumizi yao ya maarifa haya. Kwa mara nyingine tena, ni muhimu kutokuona wito wa Mungu kama aina tofauti za wito – japokuwa tunaweza kuzungumza juu ya “wito” wa ufuasi, jumuiya, uhuru, na utume – haiwezekani kutenganisha vipengele hivyo katika maisha yetu binafsi na ya jumuiya. Uwezo huu wa kuona kiujumla, kuunganisha nyanja zote tofauti za kiroho, ni sehemu muhimu ya kuandaa viongozi. Kwa kutumia mbinu inayomlenga Kristo katika ukuzaji wa viongozi, tunaweza kuona sifa mbalimbali ambazo tumezibainisha katika utu wa Yesu na tunaweza kufanya Kristolojia kuwa fundisho kuu la ukuzaji wa viongozi. Katika kuelewa utu na kazi ya Yesu, tunaelewa yote ambayo Mungu anakusudia kutufundisha kuhusu kusitawisha uongozi, angalau katika maana ya kile anachokusudia tuwe wakati kazi yake kwetu inapokamilika kikamilifu. Kama Mshauri, ni lazima sasa ujikite katika jukumu lako la usimamizi kama mwezeshaji wa moduli hii ya Capstone. Sasa, kazi yako kama mtathmini na msahihishaji itapaswa kuanza kwa bidii. Tafadhali hakikisha kuwa umepokea mapendekezo ya wanafunzi wote kuhusu kazi zao za huduma, kazi za Ufafanuzi wa Maandiko na taarifa nyingine kwa pamoja kwani hili litakuwezesha kubainisha jumla ya maksi za mwanafunzi. Tena, busara yako kuhusu kazi zitakazochelewa inaweza kuamua kwa urahisi ikiwa unakata alama za wanafunzi, na kusababisha mabadiliko ya daraja la ufaulu, au kuwapa wanafunzi alama ya “Haijakamilika” hadi kazi ikamilike. Vyovyote utakavyotekeleza kanuni zako kuhusiana na kazi zao, kumbuka kwamba kozi zetu kimsingi hazihusu maksi ambazo wanafunzi wanapata, bali ile lishe ya kiroho na mafunzo ambayo kozi hizi zinatoa. Pia, hata hivyo, kumbuka kwamba kuwasaidia wanafunzi wetu kujitahidi kupata matokeo bora ni sehemu muhimu ya masomo yetu.
13 Ukurasa 126 Mifano Halisi
14 Ukurasa 128 Kazi
Made with FlippingBook flipbook maker